Tuesday, February 12, 2013

PAPA BENEDICT WA 16 ATANGAZA KUJIUZULU FEB 28 MWAKA HUU 2013!!!

 Baba Mtakatifu ameelezea kwamba matatizo
ya kiafya yamemfanya kutangaza kujiuzulu

Jana jioni nilipatwa na mshituko niliposikia katika habari, uwamuzi na hatua ya Papa Benedict XVI wa kujiuzulu mwishoni mwa mwezi huu baada ya takriban miaka minane akiongoza Kanisa Katoliki kwa hoja kuwa umri wake wa miaka 85 ni mkubwa kiasi kwamba hawezi kuendelea kuhudumu zaidi ya umri huo.

Makao makuu ya Kanisa Katoliki huko Vatican yanasema yanatarajia Papa mpya atachaguliwa kabla ya mwisho wa mwezi wa tatu, na sherehe za Pasaka.





3 comments:

  1. Ngoja nianze hapa...hakika ni mshtuko mkubwa kwa dunia nzima kwamba baba mtakatifu anajiuzulu...nina jiuliza je kweli anajiuzuli kwa sababu hiyo ya afya au kuna kitu kingine kimetokea ambacho kinamfanya afanye hivyo?...lakini pia anafanya vizuri kama kweli ni afya maana kama mtu unaona hujiwezei ni afadhali kuacha mapema...Halafu mimi nilijua ya kwamba watu kama papa hastaafu/kujiuzulu.....

    ReplyDelete
  2. Italia ilikuwa na maonyesho ya kwanza kwa ajili ya waliotalikiana. Waliohudhuria walitembelea mashirika ya ndoa ili kupata wenzi wapya, mashirika ya huduma za usafiri ili kupanga likizo kwa ajili ya waseja, na mashirika ya kupanga talaka ili kupata mawakili, wahasibu, wanasaikolojia, na wapatanishi wa familia.—CORRIERE DELLA SERA, ITALIA.

    Kanisa Katoliki limeacha kuaminika kwa sababu “halijashughulikia vizuri kashfa za makasisi wanaowatendea watu vibaya kingono” na hilo “limetokeza tatizo kubwa sana katika usimamizi wa kanisa, huenda tangu lilipoanzishwa.”—NATIONAL CATHOLIC REPORTER, MAREKANI.

    Wanasayansi waliochunguza chembe za urithi kutoka kwa nywele za mtu kutoka Greenland aliyekufa miaka 4,000 hivi iliyopita waligundua kwamba “inaonekana alikuwa mwenyeji wa Siberia.”—SHIRIKA LA HABARI LA REUTERS, MAREKANI.

    Watu Hawatumaini Sana Kanisa

    “Watu wengi hawatumaini tena Kanisa [Katoliki],” kinasema kichwa kimoja kikuu katika gazeti The Irish Times. Ripoti hiyo inaorodhesha Kanisa Katoliki katika kikundi kimoja na mashirika mengine ambayo watu wengi nchini Ireland wameacha kuyaamini, kama vile, serikali na benki. Katika nchi inayojulikana sana kwamba watu ni washikamanifu kwa kanisa, zaidi ya nusu ya watu waliohojiwa katika uchunguzi wa hivi karibuni walisema kwamba ama hawalitumaini kanisa “kabisa” (asilimia 32) ama hawalitumaini kanisa “kwa kiasi kikubwa” (asilimia 21). Kashfa ambazo zimekumba kanisa hilo hivi karibuni zinasemekana kuwa ndizo zimewafanya watu wengi ‘wasilitumaini sana.’

    ReplyDelete
  3. haya maamuzi yake nimeyaheshimu mnooooooooo

    ReplyDelete