Friday, February 1, 2013

IJUMAA YA LEO NAPENDA KUTOA SHUKRANI KWA WAFANYAKAZI WENZANGU KWA YOTE MEMA NA HASA SIKU HII JINSI WALIVYOIFANYA KUWA SIKU YA FURAHA KWANGU!!!

Leo napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wafanya kazi wenzangu kwa kuikumbuka siku yangu ya kuzaliwa kwa keki ila haipo kwenye piacha na pia haya maua...ingawa ilikuwa tarehe 5/1.tarehe hii nilikuwa nyumbani TZ.Kwa hiyo ilikuwa ilikuwa mshtuko kwangu kidogo maaana siku zilikuwa zimepita. Ni furaha ilioje kuona kuwa kuna watu wanakuthamini, wanakujali na wanakupenda kihivyo. Ahsanteni sana na mwenyezi Mungu awajalia upendo zaidi..
Na hapa ndio wao wafafanyakazi wenzangu isipokuwa katika picha anakosekama mmoja...hawa ni kama familia yangu ya pili..ahsanteni sana.....

10 comments:

  1. HONGERA SANA DADA....PIA MMEPENDEZA KWELI NA MAVAZI YENU

    ReplyDelete
  2. Ester! Ahsante sana..yaani walinistukiza kweli mpaka nikalia kwa furaha ..

    ReplyDelete
  3. "Hakika urafiki washinda undugu"
    Hongera sana Yasinta kwa kuweza kupata marafiki wenye fadhili zenye upendo na rehema kwako na familia yako.
    ------------------------------------
    Fikiria mfano wa Ruthu na Naomi. Wanawake hao walijenga urafiki ambao ni kati ya urafiki wenye kuvutia zaidi katika Biblia. Kwa nini urafiki wao ulikuwa wenye nguvu na wenye kudumu? Ruthu alifunua sababu alipomwambia Naomi hivi: “Watu wako watakuwa watu wangu, na Mungu wako Mungu wangu. . . . Yehova na anitende hivyo na kuzidi ikiwa chochote isipokuwa kifo kitatutenganisha mimi na wewe.” (Rut. 1:16, 17) Ni wazi kwamba Ruthu na Naomi wote wawili walimpenda sana Mungu, na waliacha upendo huo uongoze jinsi walivyotendeana. Kwa sababu hiyo, wanawake hao wawili walibarikiwa na Yehova.
    =================================

    ReplyDelete
  4. kaka Ray! yaaani umesema rafiki ni zaidi ya ndugu tena yule ndugu wa kuzaliwa tumbo moja ...Rafiki ni bora zaidi kuliko mwanasesele.

    ReplyDelete
  5. Raha na Tamu ya kuishi vyema na watu...Hongera KADALA..

    ReplyDelete
  6. A very Happy and belated Happy Birthday wishes from Nairobi Kenya.
    May you live loooooooooooong and healthy and happy years ahead.

    Happy Birthday Jacinta

    ReplyDelete
  7. Kwani umefikisha miaka mingapi Yasinta?

    Hongera sana....

    swali usilitupie kapuni pleeeeaase...

    Baraka kwako na familia yote.

    ReplyDelete
  8. Kachiki! Ahsante sana....

    Brother John Kanene! Thank you very much!!

    Dada mkuu msaidizi! nadhani unajua ni miaka mingapi!!:-) Ahsante kwa kupita hapa na kuuliza pia ila jibu walijua...

    ReplyDelete
  9. @Yasinta unaombwa utaje miaka yako kibarazani.
    [Blogger Mija Shija Sayi said...Kwani umefikisha miaka mingapi Yasinta?]

    ReplyDelete