Monday, January 14, 2013

SIKU HIZI SITAZISAHAU ..HATIMAYE TUMEKUTANA USO KWA USO..

Yasinta na Kaka Albano Midelo Ruhuwiko/Songea Ilikuwa ni mwaka mpya huu 2013 kwa mara ya kwanza kaka Albano Midelo alikuja kututembelea kwetu Ruhuwiko yeye ni mmiliki wa blog ya Maendeleo ni vita
Yasinta na kaka Shaban Kaluse wakiwa Jangwani beach Dar es Salaam Haikuishia kukutana na kaka Midelo tu, pia kwa mara ya kwanza nikakutana na kaka yangu wa hiari kaka Shaban Kaluse Mzee wa utambuzi. Ilikuwa ni furaha ya ajabu sana kukutana na kaka huyu ...kwa kumfahamu zaidi unaweza kumsona hapa
Yasinta na Dada Ester Ulaya wakiwa wametulia ndani ya Savanah Lodge Sikuishia kukutana na hao akina kaka tu ..Nilipata bahati ya kukutana na Dada Ester Ulaya pia nadhani safari yangu safari hii ilikuwa yenye baraka sana kuweza kukutana na ndugu hawa..hapo tupo sehemu tuliyofikia Savanah Lodge ambayo ipo maeneo ya Banana..kuweza kumfahamu dada huyu ingia kwenye blog yake Rular and Urban
Na hapa ni picha ya pamoja hicho kiti kisicho na mtu ni cha mpiga picha ambaye ni mr. wangu, anayefuatia ni mmiliki wa hotel ya Savanh Lodge, halafu anafuatia kaka Kinunda, na halfu anafuatia ni mume wake dada Ester Cathbert Angelo Kajuna na ni mmiliki wa blog HABARI NA MATUKIO na pembeni yake ni mwenyewe dada Ester na halfu mimi nipo ila sijaonekana hapo na bila kusahau kaka Chacha naye tulikuwa naye ila alifika baadaye na katika kunogewa na hadithi tukasahau kupiga naye picha.Na halafu nisisahau tulikuwa na dada mkuu msaidizi katika maongezi yetu yaani kwa simu..si mwingine tena ni mwenyewe mwanamke wa shoka Dada Mija. Yeye anapatikana zaidi hapa. Tuulikuwa na wakati mzuri sana kwa ujumla.

9 comments:

  1. Nivizuri sana kukutana na watu mbalimbali hasa unapo kuwa likizo bongo. mmependeza picha ni nzuri, mwakani mimi nilikuwa huko ,hakika nikikumbuka ilikuwa safari nzuri na ya kufurahisha mimi na mwanangu,hasa tulipo tembelea hifadhi ya mbuga ya Katavi-mpanda. kaka s.

    ReplyDelete
  2. Hakika mlikuwa na wakati mwema, kukutana na kupeana 2-3 inapendeza sana.

    ReplyDelete
  3. Angalau hata nami nilikuwepo ki-simu, nilifurahi sana kuongea na group lote...

    Jamani naona mmerudi mapema au ni akili yangu sijui...

    karibuni tene na tena..

    ReplyDelete
  4. kaka Sam Katavi ni kwetu huko jamani, uje tenaaaaa..........Dada Yasinta mje tena.....hapa namsubiria tena Da Mija, Mungu azidi kutubariki na kutuweka hai Amen

    ReplyDelete
  5. Nitakuja tu dada yangu, huko ni nyumbani ninakupenda kupita kiasi,huwa dar na kaa wiki moja tu natimua kumpanda,tabora napo ninyumbani lakini sasa pamebaki siyo kama zamani mjomba na shangazi ndo walikuwa wamebaki sasa hawapo na walikuwa ,urambo na tabora sehemu ya ng'ambo. nitakutafuta tu blog yako simchezo huwa unaweka vitu ambavyo vina ni gusa. kaka s

    ReplyDelete
  6. Nitakuja tu dada yangu, huko ni nyumbani ninakupenda kupita kiasi,huwa dar na kaa wiki moja tu natimua kumpanda,tabora napo ninyumbani lakini sasa pamebaki siyo kama zamani mjomba na shangazi ndo walikuwa wamebaki sasa hawapo na walikuwa ,urambo na tabora sehemu ya ng'ambo. nitakutafuta tu blog yako simchezo huwa unaweka vitu ambavyo vina ni gusa. kaka s

    ReplyDelete
  7. Ukitembelea mitaa ya Canada usikose kunitafuta. Laiti mitaa ya kwa mama isingekuwa kushoto kwako ningeishakutafuta. Anyways ipo day!

    ReplyDelete
  8. Ni furaha kweli kweli...ona utamu wa maongezi kunoga mpaka kusahau kupiga pichaaa...baaah!

    Aksanteni kwa kuja!

    ReplyDelete