1. Chini chakula, juu chakula, katikati kuni. Nini hicho
2. Nimefika ugenini, ameniamkia mtoto. Mtoto huyu ni nani?
3. Mtu anabadilika badilika
4. Watoto wawili wanapigana kila wakati. Watoto gani hao?
5. Ndege wangu ametagia kwenye miiba. Ndege gani huyyo?
6. Shamba langu nimelima kubwa, nimepanda mbegu zangu tatu: Mbegu hizo ni nini?
7. Mgeni yupo ndani nyumbani, hasemi, mimi simwogopi
8. Nje kukavu, ndani maji. Nini hicho?
9. Nyumba yangu ina nguzo mbili, kama zinaanguka siwezi kuzisimamisha.
10. Nimekata tete, nimevuka mto mkubwa. Tete hili ni nini?
11. Natoka kwa mama, naenda kufa.
12. Ugonjwa wa watu wote ni nini?
NAWATAKIENI KILA LA KHERI KWA KILA JAMBO...!!!!!!!
UUuuuuwiii....hapo ntapata moja tu! Nambari 5 tu...ambalo ni NANASI
ReplyDeletemengine yote mwalimu nipe yai tu bana!
mmmhhh! jaribu tena kaka Wambura maana hilo jibu si lenyewe...
ReplyDelete1. Muhogo.
ReplyDeleteBy Salumu
Makofi kwa kaka Salumu wa wa wa..umapata ....
ReplyDeleteayyaaaaaaa! NAFWAA
ReplyDeleteHakika ya kale ni dhahabu!
ReplyDeleteAsante sana Da Yasii.
5. Nanasi
ReplyDelete8. Yai
12. Njaa
3. Kinyonga
ReplyDeletehehehehe
naona wengi mmejaribu mnastaili zawadi kwa kweli ...au naona nitoa majibu yake..Ester umepata ya 12 na 3 makofi wa wa waaaaaa... hivi ni vitendawili vya kingoni kwa taarifa yenu na majibu yake ni:-
ReplyDelete1. Muhogo
2. Miba ya nyasi(luhano)
3. Kinyonga
4. Miguu
5. Ulimi
6. Jua na mwezi
7. Kunguni
8. Tikitimaji
9. Matiti
10. Utandu wa buibui
11. Jani
12. Njaa
Asante sana kwa majibu dada maana vilikuwa vigumuuuuuuuu
ReplyDeleteJibu hiyo kitendawili
ReplyDelete1.hachelewi wala hakosei safari zake
1 muhogo
ReplyDelete