Tuesday, October 30, 2012

SIKU YA MAHAFALI KATIKA SEKONDARI YA WILIMA/MADABA/MATETEREKA=SONGEA!!!!

Kutoka kushoto ni Meneja wa shule ya sekondari Wilima mzee Lucas Mayemba, katikari ni Mwl.Paul Mgaya wakati sisi tunaishi hapa alikuwa  mkuu msaidizi.  Hapa wapo katika jengo la utawala katika shule hiyo na mwisho hapo ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Songea Bw. Rajabu Mtiula
 
 Mmoja wa Wahitimu akipokea Cheti cha kuhitimu kidato cha nne....Ni furaha ilioje kuweza kufika hapa tena ingwa kipicha. Nimefurahiiiiii sanaaaaa hasa kuwaona mzee Mayemba na  Mgaya PHD......Hapa ndipo nilipoanzia MAISHA YANGU. Picha http://mwambije.blogspot.se/ nakushukuru sana uliyepiga picha.

6 comments:

  1. Baada ya kuona hizi picha za sekondari hii ya Wilima nilirukaruka na nikajisikia kama nipo nao. Hapa ndipo nilipoanzia maisha yangu ya utu uzima..Ndio kiini. Hakika nimefurahi sana, pia nimefurahi kuona maendeleo, yaani kumekuwa kuzuri zaidi kweli panapendeza...Zaidi nimefurahi kuwaona mzee Mayemba na Mwl. PHD Mgaya....

    ReplyDelete
  2. Mh!!! sasa hao walimu nao walikuwa wakivishwa maua???

    ReplyDelete
  3. yasinta mpenzi hujambo? yani umenikumbusha mbali sana tena pale nilipomuona mgaya,yani sijui niseme nini machozi yamenitoka kwa furaha. rose ngittu uk.

    ReplyDelete
  4. Rose Ng´ttu! Yaasni we acha tu mie mzima kabisa sijui wewe..mwenyewe nilipoona hiyo picha nilitoa mchozi ulinitoka pia..

    ReplyDelete
  5. Shule yangu..shule yetu. Nafurahi kuona bado inaendelea kuwepo.

    ReplyDelete