Wednesday, October 24, 2012

HIVI LINI UMECHEKA AU KUTABASAMU BASI UNGANA LEO NAMI KUHUSU HILI: Maongezi ya Mtoto na Baba'ke

Baba: We mtoto hebu niletee soda...
Mtoto: Cola au Pepsi?
Baba: Pepsi.
Mtoto: Kopo au Chupa?
Baba: Kopo.
Mtoto: Baridi au moto?
Baba: Baridi.
Mtoto: Ndogo au Bonge?
Baba: Aaa! Basi niletee tu maji.
Mtoto: Ya bombani au dukani?
Baba: We mtoto nitakupiga?
Mtoto: Na mti au chelewa?
Baba: N'takuua nakwambia!
Mtoto: Kwa kudu au bunduki?
Baba: Bunduki.
Mtoto: Kichwani au kifuani?
Baba: Mbaff, toka nje!
Mtoto: Sasa hivi au baadaye?
Baba: Sasa hivi.
Mtoto: Kwa hiyo maji hutaki tena?
Baba: (kimoyomoyo) "nilimwambia mke wangu tukilewa tusifanye, yeye anang'ang'ania, haya ndiyo matokeo yake..."
Source: http://www.wavuti.com

11 comments:

  1. Hahaha hivi kweli ukilewa unazaa vichaa, wenye akili za kipombe?

    ReplyDelete
  2. Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,

    Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.

    Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana_Waefeso 6:1-3

    ReplyDelete
  3. @Yasinta;
    Asante kwa kidokezo chenye ladha ya vichekesho lakini ikihanikizwa na changamoto katika malezi yanayojali madaraka,haki,wajibu na nafasi baba mwenye utambuzi katika nafasi ya kichwa na mhimili wa familia.

    ReplyDelete
  4. emu-3! nami nilikuwa najiuliza hivyo hivyo kunywa pombe ndio kunafanyisha mtoto awe hivyo?
    Usiye na jina hapo juu! basi tupo wengi mie nimecheka na nikasema ngoja niwashirikishe.

    Kaka Ray! Hiyo amri hiyo wengi sana wanaisahau maana wanawajibu wazazi wao majibu ya ovyo mpaka huruma...Ahsante kwa neno pia.

    ReplyDelete
  5. Wazazi pia wamepewa mamlaka na Mungu. Biblia inashauri hivi: “Akina baba, msiwe mkiwasumbua watoto wenu, bali endeleeni kuwalea katika nidhamu na rekebisho la akilini la Yehova.” (Waefeso 6:4) Katika Biblia, neno “nidhamu” linaweza kumaanisha “malezi, mazoezi, mafundisho.” Watoto wanahitaji nidhamu; wanafurahi na kufanikiwa wanapopewa maagizo yaliyo wazi, na wanapowekewa mipaka na vizuizi. Kulingana na Biblia, nidhamu au mafundisho huhusisha upendo. (Mithali 13:24) Kwa hiyo, “fimbo ya adhabu” haipaswi kamwe kuwaumiza watoto kihisia-moyo au kimwili._ (Mithali 22:15; 29:15) Mzazi anayetoa nidhamu kwa ukali bila upendo anatumia vibaya mamlaka yake. Kufanya hivyo kunaweza kumvunja moyo mtoto. (Wakolosai 3:21) Kwa upande mwingine, kutoa nidhamu kwa usawaziko na kwa njia ifaayo kunawathibitishia watoto kwamba wazazi wanawapenda na wanapendezwa na utu wanaositawisha.

    ReplyDelete
  6. Kutegemea Vitabu Vyenye Mashauri ya Kulea Watoto

    Hata hivyo, wataalamu hao wametimiza nini? Je, leo wazazi wana mahangaiko machache na wanaweza kuwalea vizuri zaidi watoto wao kuliko wazazi wa miaka iliyopita? Uchunguzi uliofanywa hivi majuzi nchini Uingereza unaonyesha kwamba sivyo ilivyo. Uchunguzi huo ulionyesha kwamba karibu asilimia 35 ya wazazi bado wanatafuta mashauri yenye kutegemeka. Wazazi wengine hawana la kufanya ila kufuata fikira zao wenyewe.

    Katika kitabu chake (Raising America: Experts, Parents, and a Century of Advice About Children), Ann Hulbert anachanganua vitabu vya kitaalamu kuhusu kulea watoto. Hulbert, ambaye ni mama mwenye watoto wawili, anasema kwamba kauli chache za wataalamu zilitegemea sayansi iliyothibitishwa. Kwa kweli, yaelekea kwamba mashauri yao yanategemea mambo waliyojionea maishani mwao badala ya mambo yaliyothibitishwa. Leo, tunapofikiria mashauri ambayo yaliandikwa zamani, mara nyingi mashauri hayo huonekana kuwa yenye kubadilika-badilika, kupingana, na nyakati nyingine ya kiajabu-ajabu.

    Basi, wazazi wa leo watafanya nini? Kwa wazi, wengi wamechanganyikiwa, kwa sababu kuna mashauri, maoni, na ubishi mwingi kuliko wakati mwingine wowote. Hata hivyo, si wazazi wote ambao wanahisi kuwa hawana mwongozo. Wazazi ulimwenguni pote wanafaidika kutokana na chanzo cha zamani cha hekima ambacho bado kinatoa mashauri yenye kutegemeka.

    ReplyDelete
  7. dah ccta hapo univunja mbavu,take care pia mzee akiwa amelewa usimgeukie mkawaongeza akina hao wa maswal tu.siku njema dadaa.

    ReplyDelete
  8. Asante Yasinta nimecheka kweli na msongo wa mawazo umeondoka safi kabisa ila hiyo nilimwambia tukilewa tusifanye nayo mhhhhh!!!

    ReplyDelete
  9. Habari.
    Du hiyo kali.

    Nyoka huzaa nyoka au?

    Kila la kheri

    ReplyDelete