Wednesday, September 5, 2012

VAZI HILI LA KITENGE NIMELIPENDA SANA..MAMA SALMA KIKWETE NA DKT ASHA-ROSE MAIGIRO

Ndugu zangu waTanzania hasa akina dada/akina mama hebu angalieni vazi/mavazi haya. Kwanza ni la heshima, pili wanapendeza yaani hata kuangalia tu kwa macho. Mara nyingi nimekuwa nikijiuliza kwa nini kupoteza pesa nyingi kununu nguo kama mitumba nk. Wakati kuna vitenge vizuri ajabu ambavyo twaweza kushona na kupendaza kama akima mama hao hapo juu. Angalia mishono yao ni rahisi rahisi tu si ya ajabu. Hakika mwenzenu niMEPENDA SANA HII.
---------------------------------------------------------------------------------------------------------
Hapa ni wote mnawafahamu hawa akina mama ila nitasema tena ni:- Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akiwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt Asha-Rose Migiro baada ya Mama Kikwete kuzindua Mpango wa Kasi ya Uwezeshaji wa Wanawake na Wasichana Agosti 24, 2012 katika ukumbi wa Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es salaam.

JUMATANO NJEMA KWA WOTE!!!!




8 comments:

  1. Vivyo hivyo natamani wanawake wajipambe kwa mavazi yenye mpangilio mzuri,pamoja na kiasi na utimamu wa akili,si kwa mitindo ya kusuka nywele na dhahabu au lulu au mavazi yaliyo ghali sana,bali kwa njia inayowafaa wanawake wanaodai kumheshimu Mungu, yaani, kupitia matendo mema._1Timotheo 2:9,10.

    ReplyDelete
  2. kitenge ni vazi tamu sanaaaaaaa
    uwe na jumatano njema dada

    ReplyDelete
  3. Kaka Ray ! Ahsante kwa kutukumbusha hilo sisi akina dada/mama.

    Dada Mdogo Ester! Yaani watu hatuji tu hili halafu kuna vitenge vizuri vyenye rangi nzuri za kuvutia na bei yake si mbaya...Tana ni nguo nzuri zaidi kuliko zote...halafu ukimpata fundi anayejua kukipamba kama hivyo hapo juu ww itakuwa bonge la kupendeza... Ahsante Ester..

    ReplyDelete
  4. Kuvaa nguo ndefu ni heshima? mavazi yana uhusiano na heshima kweli? kama ndiyo ni kwa kiasi gani,tafadhali nijulishei waungwana,dada Yasinta!. kaka s

    ReplyDelete
  5. Kaka Sam! Ndiyo kuvaa nguo ndefu ni heshima..nimesema hivi kutokana na mtu unakotoka na ni malezi gani umelelewe inawezekana wengine wanaona nguo fupi ni heshima pia.

    ReplyDelete
  6. Vazi mali sana sema mmojawapo wa waliolivaa hovyo. Ni fisadi atumiaye madaraka ya mumewe kutuibia. Ni zuri kweli kweli ila alipokuwa akilivaa Anna Mkapa au Mama Tamaa lilikuwa kama limemvaa.

    ReplyDelete
  7. emu3! ni furaha kuona upo pamoja nasi:-)
    Mwl. Mhango! Nakubaliana nawe kuwa ni vali mali sana. Na kweli anatumia nguvu kupata madaraka...na wananchi wamekaa tu kimya hawasemi kitu..

    ReplyDelete