Unganeni nami ili tupata majibu ya VITANDAWILI HIVI HAPA CHINI. KARIBUNI SANA!!
1. Nyumbani mwangu mna shetani ambaye daima anakunywa maji yangu...
2. Mama nieleke.
3. Nenda huko na nikirudi nimshike ngómbe wa mama mkia.
4. kipo lakini hukioni.
5. Nilikuwa nikitembea njiani niliposimama nikasikia mtu akiniita "wifi! wifi!, lakini nilipogeuka sikumwona mtu.
6. Bibi mweupe ametupwa mibani.
7.Mzazi ana miguu bali mzaliwa hana.
8. Wanabgu wote wamevaa vizibao, wasiovaa si wanangu.
9. Ni nini hutupwa juu ya meza wakati watu wapo ndani?
10. Huku ngó na kule ngó.
JUMANNE NJEMA KWA WOTE!!!
Duh!! Vitendawili vigumuuuu!!
ReplyDeleteKaka Emanuel jaribu tena mlongo kimoja utakuwa unaweza tu nina imani haswaaa...
ReplyDeletePara
DeleteSawa
DeleteKitendawili tega ukishindwa nipe mji nata kwenda Ruhuwiko!
ReplyDeleteHih
Delete@Yasinta;
ReplyDeleteUmeamu kuturudisha kule shule ya msingi kwa vitendawili vigumu.
Nikikumba kule shule ya msingi darasani mkiona kitendawili cha mwenzenu ni kigumu mnampa mji ili awape jibu.
-------------------------------------
Kitendawili chako tega; nimeshindwa nakupa mji; nenda Ruhuwiko!
-----------------------------------
"Hakika umeamua kuturudisha kwenye zama zetu za elimu ya msingi."
ReplyDeleteAsante sana Yasinta.
Ndiyo kaka Ray,,Leo nimekumbuka na nimetamani sana kuwa mwanafunzi wa shule ya msingi. Na naona tusubiri kidogo labda kutakuwa na anayeweza angalao kitendawili kimoja tu...:-)
ReplyDeleteWifi wifi ni mbaazi hizo.Na vingine naendelea kuwaza zaidi.
ReplyDeletembona vitendawili rahisi sana, tupatie vingine vigumu ili tukupe mji.
ReplyDeleteKaka Ray hiyo umepatia...ila usiendelee kusiazea sana..
ReplyDeleteUsiye na jina! kama ni rahisi sana mbona hujatoa majibu yake?
ndugu zangu wapendwa naona vitendawili vilikuwa vigumu mno maana jibu limekuwa ni moja tu..kwa hiyo naona nitegue vitendawili hivi:-
ReplyDelete1. Mafuta ya taa.
2. Kitanda.
3. Kata ya maji
4. Kisogo
5. Mbaazi kavu.
6. Machicha ya nazi
7. Kuku na yai
8. Kunguru wenye mabawa meupe.
9. Kitambaa
10. Giza.
haya ndiyo majibu ya vitandawili vyetu. Ahsanteni kwa kuwa nami..
ahsante sana 🙏🙏
DeleteAsante sana mwalimu kwa somo la leo.
ReplyDeleteduuh! dadaa umenikumbusha mmmbaaaali sana ile miaka nipo mdogo zaidi ya wadogo daah!.gdday.
ReplyDeletehapana chakwanza sio mafuta ya taa ila ni koroboi ndio inakunywa mafuta kwahiyo KOROBOI NDIO SHETANI ANAKUNYWA MAFUTA
ReplyDeletehapana chakwanza sio mafuta ya taa ila ni koroboi ndio inakunywa mafuta kwahiyo KOROBOI NDIO SHETANI ANAKUNYWA MAFUTA
ReplyDeleteNaombeni jibu la kitendawili hiki
ReplyDelete‘Nyumbani kwangu hapakosekani unga’
Majivu
DeleteNaombeni jibu la kitendawili kinachosema jini mnywa damu haangazi bila damu.
ReplyDelete