Hapa ni maandalizi ya kuaandaa pilau/chakula yanaanza
Baadhi ya wageni wamewasili
Tupo mezani tunalichapa pilau kwa raha zote
Msosi na hadithi zinaendelea ,......kila kitu kilikuwepo
Mpishi na mwenyeji anaonekana hapa pia ...maana ndiye alikuwa mpiga picha za hapo juu
Na mwisho akatokea mpiga picha na tukapiga picha ya pamoja. Waliokaa chini kwanza Yasinta, anayefuatia ni Marlene, waliosimama nyuma yangu ni Pernilla, anayefuatia mwenye batiki ni Ylva na halafu Elizabeth na mwisho ni Maria. Nilifurahi sana kuwa walikubali kuvaaa nguo zangu angalia utadhani walipima wao:-) Na jioni ikaishia hapa. Hakika kwangu na kwa wo pia tulikuwa na siku nzuri sana naweza nikasema tulikuwa nusu ya Afrika/Tanzania. JUMATATU NJEMA.
Kweli ukijithamini utathaminiwa, Inapenda sana da'Kadala, Mtu kwao@
ReplyDeletevipi dada Yasinta Marlene ameolewa?kama bado basi nifanyie mpango
ReplyDeleteKachiki! Ahsante ndugu wangu..nakuambia hii siku ilikuwa moja ya siku ambazo nilikuwa na furaha sana.
ReplyDeleteBatamwa! Bahati mbaya umechelewa Marlene ameolewa na ana mtoto tayari. Ila ntamwambia:-)
@Yasinta;
ReplyDeleteHongereni sana kwa tafrija ya ubunifu iliyohanikizwa na upendo mchangamfu kutoka katika sakafu za mioyo yenu.Hakika hiki ni kitu adimu katika orodha ya vitu adimu.
hiyo inaitwa B2A...BACK TO AFRICA... nimepipenda sana hiyo sister Yasinta.. du..wazungu wa watu na host mmependazaje? mavazi yetu mazuri sana..ila mmoja hapo kama hana furaha, kulikoni wifi? hahahahahahaha (shangtazi ya Camilla huyo!
ReplyDeletemmependeza,na nguoza kitz safi. mwanamke vitenge!? kaka s
ReplyDeleteViko vitu vya kawaida sana ambavyo vinaweza kufanya mtu akayafurahia maisha na kila nukta ya uhai ikawa na maana. Huu siyo tu ubunifu, lakini ishara za wazi za UPENDO ambao hauhesabu gharama. Hapa kwetu TZ ili uwape watu pilau lazima kwanza uwachangishe halafu ndo uwaite kuja kula pilau, tena huku ukihakikisha kwamba katika vile walivyochanga, kuna vingine vingine vinabaki kwa ajili ya watoto wako. Huo ni upendo au wizi? Unawezeja kuwapenda watu kwa gharama zao wenyewe. Hapo umewapenda au umejipenda? Dada Yasinta naamini hawa wazungu wa watu hukuwachangisha. Kama vile haitoshi, ukawagawia na vitenge vyako wajimwage navyo. WHAT A WONDERFUL LOVE.
ReplyDeletesafi sana hii na wenyewe wamependeeza na hayo mabatiki kama wamezaliwa nayo vile
ReplyDeleteyasinta endelea na moyo huu wa kujitoa, umetoa mavazi na vyakula.Mungu akuzidishie pale ulipotoa na akubariki sana.Nimependa huo ubunifu, keep it up.
ReplyDeleteBaaaaab kubwa Ysinta!! Mimi sina hata la kusema.
ReplyDeleteNimeikagua sana nyumba yako yaani ni Utanzania mtindo mmoja...nimekipenda kitambaa cha meza.
Hongera sana dada mkuu..
umebarikiwa mkono utoao kuliko mkono upokeao
ReplyDeletewooooou! fantastic! mbona umealika weupe tu jaman,dah! hilo bonge la msos.duh kumbe wazungu wanapendeza sana wakivaa kiafrica! ahsante kwa kututangazia utamadun wa muafrica.gud day dadaa.
ReplyDeleteNimewapenda mno hawa ladies, kwanza walivyovaa inaonyesha upendo wao kwetu, hv nani aliwashonea hizo vitenge? na wamependezaje jamani!!!!!, wafikishie salaam zangu, i love u all, mwaaa mwaa mwaa,
ReplyDeleteShukrani kwa wote na salamu nyingi sana kutoka kwa hao akina dada. Siku hii kwa kweli ilinifanye nijione nipo nyumbani kabisa. Napenda kuwashukuru sana akina dada hawa kwa kuifanya siku hii ikawa ni kati ya siku ambazi sitazisahau maishani. Ilikuwa safi kwa kweli kuwa Tanzania/Afrika ndogo:-)
ReplyDelete‘Upendo huvumilia mambo yote. Upendo haushindwi kamwe. ’—1 KOR. 13:7, 8.
ReplyDelete=================================================================
Mambo mengi yameandikwa na kuchapishwa kuhusu upendo. Sifa hiyo imetukuzwa na kutungiwa nyimbo za mahaba. Upendo ni uhitaji wa msingi wa wanadamu. Lakini mara nyingi vitabu na sinema zimeonyesha hadithi za uwongo kuhusu upendo, na kuna habari nyingi kama hizo zinazouzwa kwa wingi. Hata hivyo, inasikitisha kwamba watu wengi hawampendi kikweli Mungu na jirani yao. Tunaona mambo ambayo Biblia ilitabiri kwamba yangetukia katika siku hizi za mwisho. Watu ‘wanajipenda wenyewe, wanapenda pesa, wanapenda raha badala ya kumpenda Mungu.’—2 Tim. 3:1-5.
==============================================================
Nafsi yenye ukarimu hiyo yenyewe itanoneshwa,naye anayenywesha wengine kwa ukarimu yeye mwenyewe pia atanyweshwa kwa ukarimu,_Methali 11:25
asante dada Yasinta ninasubiri jibu kwa hamu sana lolote lile
ReplyDelete