Wednesday, August 15, 2012

WALALAMIKIA UBOVU WA MIUNDOMBINU YA STENDI SONGEA!!!

Katika KIPENGELE CHETU CHA JUMATANO YA MARUDI LEO NIPO SONGEA NA NINGEPENDA MUUNGANE NAMI...HABARI HII NIMEIPATA HAPA KARIBUNI....
Stendi ya Songea ikiwa katika hali mbaya.
Na Gideon Mwakanosya, Songea
BAADHI ya wakazi wa Halmashauri ya manispaa ya songea wakiwemo abiria wameulalamikia uongozi wa manispaa hiyo kwa kushindwa kukarabati miundombinu ya kituo kikuu cha mabasi cha mjini Songea na kusababisha adha kubwa abilia na baadhi ya magari kukwama hasa wakati wa kipindi cha masika.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana abiria hao wameeleza kuwa hali ya kituo cha mabasi cha Songea kwa muda mrefu kina hali mbaya ambapo kwa kipindi cha mvua kunakuwa na mashimo ambayo hujaa maji na kusababisha magari ya kubeba abiria kukwama katikati ya kituo hicho
Wameeleza zaidi kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakiulalamikia uongozi wa halmashauri hiyo kuhusu kuwepo miundombinu mibovu kwenye kituo hicho bila kuwepo mafanikio jambo ambalo limeonekana kuwa ni kero kubwa kwa wakazi wa songea wakiwemo abiria .
Mmoja kati ya wananchi hao John Komba mkazi wa Mbinga alisema kuwa hali ya kituo hicho ni mbaya sana hasa kwa wakati huu wa kiangazi ambapo kumekuwepo na vumbi ambalo limeonekana kuwa ni kero kwa watu wanaoingia na kutoka kwenye kituo hicho kwa miguu hivyo ameuomba uongozi wa Halmashauri kuona umuhimu wa kumwagia maji kwa lengo la kupunguza kero ya vumbi lililokithiri
Naye Sebastian Nombo mkazi wa kijiji cha Kihangimauka kilichopo wilayani Mbinga alisema kuwa ipo aja kwa uongozi wa Halmashauri ya manispaa ya Songea wakiwemo madiwani kuona umuhimu kwenda kujifunza jinsi mbinu wanazozitumia kuboresha miundombinu mbalimbali ya barabara za halmashauri ya wilaya ya mbinga pamoja na mikakati waliyonayo ya kukijenga kituo kipya cha kisasa cha mabasi cha mjini mbinga.
Nombo alieleza zaidi kuwa inasikitishwa sana kuona hali mbaya ya miundombinu ya kituo kikuu cha mabasi cha mjini songea ambacho kipo makao makuu ya mkoa wa Ruvuma hivyo ni vyema uongozi wa halmashauri hiyo ukachukua hatua za haraka kukifanyia ukarabati kituo hicho cha mabasi ambacho kinaonekana kuwa ni kero kwa wakazi wa Songea.
Mmoja wa wamiliki wa magari wa kusafirisha abiria kati ya Songea na Dar es salaam ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe alisema kuwa ushuru wa magari yakiwemo mabasi yanayoingia kwenye kituo kikuu cha mabasi cha manispaa hiyo umekuwa ukitolewa kila siku lakini Halmashauri hiyo imeshindwa kukifanyia matengenezo jambo ambalo limeonekana kuwa ni kero kwa abiria hasa wakati mvua zinaponyesha kunakuwa na madimbwi ya maji ambayo husababisha magari kupita kwa taabu katika kituo hicho.

Mmoja wa wafanyakazi wa mabasi ya SAJDA yanayosafirisha abiria kutoka songea kwenda Mbinga Oddo Nchimbi alisema kuwa magari madogo yanayoingia kwenye kituo hicho (TAXI) Halmashauri hiyo imekuwa ikiwatoza shilingi 500 kila siku wakati magari yenye uzito wa tan 1 nusu hadi tani 7 kila anapoingia kwenye kituo hicho hutozwa shilingi 1000 kila siku na magari makubwa yakiwemo ya kusafirisha abiria kuanzia tani saba na kuendelea kila yanapoingia hutozwa shilingi 2000 kila siku lakini hali ya kituo hicho cha mabasi ni mbaya.
Alisema kuwa abiria wanayoijua stendi hiyo hasa wakati wa masika wamekuwa hawapandii mabasi ndani ya kituo na badala yake wamekuwa wanapandia nje ya kituo kwa kukwepa adha ya tope .
Kwa upande wake kaimu wa mkurugenzi wa manispaa hiyo Naftari Saiyori alipoulizwa kuhusiana na kero hiyo alikiri hali ya kituo cha mabasi ni mbaya lakini alieleza kuwa halmashauri yake inampango kabambe wa kujenga kituo kikuu cha mabasi cha kisasa huko katika eneo la msamala ambapo alidai kuwa mpango huo uko katika hatua ya upembuzi yakinifu na kwamba kwa hivi sasa kutakuwa na gari la maji litakuwa linapita kwa wiki mara tatu kwa lengo ya kupunguza kero ya vumbi iliypo kwenye kituo hicho.
TUKUTANE TANA KATIKA KIPENGELE HIKI CHA MARUDIO JUMATANO IJAYO PANAPO MAJALIWA!!!!!

7 comments:

  1. Haya mambo wakati mwingine yanatufanya tukimbie kutoka nyumbani kwetu na kukimbilia kwenye miji ya watu hasa tunapokutana na vitu ambavyo hatuwezi kuvishughulikia wenyewe kama vile miunbombinu. Hii Stand tangu nimeifahamu miaka ya mwishoni mwa themanini ipo hivyo hivyo na nadhani hali inazidi kuwa mbaya kila kukicha. Sina hakika hao wenye mamlaka na huo mji wanapata wapi ujasiri wa kujitambulisha kuwa mimi ni Mkurugenzi au mkuu wa wilaya wa mji wa namna hii. Pamoja na yote, NYUMBNI NI NYUMBANI NA MKATAA KWAO MTUMWA!! Siku njema

    ReplyDelete
  2. emu3! Shukrani kwa kuupokea ujumbe.
    Kaka Mhagama! hapa umesema hata mie tangu nipate akili na kuijua Songea yangu hii stendi imekuwa hivyo hivyo hakuna mabadiliko na sasa imekuwa Manispaa mambo yaleyale..NI KWELI Polepole ni mwendo kweli?

    ReplyDelete
  3. BWANA MHAGAMA UKWELI UNACHOSEMA NI KWELI MIMI NAUNGANA NA WEWE KUWA KAMA STAND HII NILIIONA MWAKA 1980 JANUARY WAKATI NAINGIA FORM ONE PALE KIGONSERA BADO IPO VILE VILE WAKATI HULE TULIKUWA NA MAGARI YETU YALE KAURU,KAUMU NA KAMATA NA YALE MABASI YETU YA AKINA KOMBA NA YALE YA VIJIJI KAMA MUYOA,NDONGOSI,
    NK NAYAKUMBUKA MACHACHE KWELI STANDI HAIJABADILIKA MBONA SOKO LETU LIMEBADILIKA KASORO ZILE HOTEL HAZIWEZI KUHAMISHIKA KAMA DELUX MATALAWE NK SASA NYIE WAKUURUU GENZI MNAFANYA KAZI GANI UKWELI NDIYO MAANA SISI TUKIJA MJINI KAMA DAR HATUTAMANI KURUDI KWETU MPANDANGINDO ,NDUGU YANGU NDUNGURU KASEMA HAENDI NTYANGIMBOLE TENA KWANI AKIONA MAJI YA PALE FERY PANTONI ANAONA KAMA YUPO NYASA NA HIVI TENA MAMA BANDA ANATAKA KUCHUKUA TENA MBINGA YOTE MPAKA MATETEREKA NGOMBO MPAKA CHIULU AMESEMA HAENDI TENA, UKWELI WEWE MKURUGENZI SIJUWI UNAITWA KAPINGA AU MBAWALA ITAKUWA KOMBA TUU JITAHIDI KUTUBADILISHA MBONA USHURU UNACHUKUA KILA SIKU HAPO STAND KWANI MNAPELEKA WAPI TENA SI WA MABASI TUU MPAKA HAO WAFANYA BIA SHARA NA MACHINGA WOTE HAPO KWELI, JAMANI BADILIKENI DADA YANGU YUPO KULE MAJUU AKIJA NA SHEMEJI YETU NI AIBU ASHUKE PALE NA MATOPE NA VUMBI MTAMFANYA MWEKEZAJI ASIJE KWETU JAMANI HAPO UWANJA WA NDEGE HATUJUWI KUPOJE
    KWA HERI SIIJI, TEENA SONGER ILA RUVUMA KWETU NITAKUJA KWA WABABA NITAISHIA KWA MAMAA MASASIIIIIIIIIIII
    CHE JIAH

    ReplyDelete
  4. @Yasinta;
    Hakika kuna kigugumizi cha maamuzi na usimamizi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa jamii husika.
    Hapa wananchi na wadau kwa pamoja tunalazimika kulia kilio chenye sauti ya moja.

    ReplyDelete
  5. Asante Kadala kwa yoote.

    Lakini baba Chejiah hahhaaaha yaani Umesisisisisissiiiiiitizaaaaa Bahh.

    ReplyDelete
  6. Che Jiah,
    Tena nakubali kwamba kweli kufa kufaana. Unajua hata hilo Soko unalosema limebadilika ni kwa sababu ilibidi walijenge upya baada ya kuteketea kwa moto. Mie nadhani wangeweza kulirudishia kama mwanzo nadhani wangefanya hivyo, lakini hawakuwa na namna zaidi ya kulijenga upya. Lakini kama siyo moto, hapana shaka bado lingekuwa vile vile. Hiyo stand nayo ingeweza kuungua ilibidi iungue labda wangepata akili ya kujenga ya kisasa.

    ReplyDelete