Saturday, August 11, 2012

TUMALIZE JUMAMOSI HII KWA MLO HUU:- UGALI KWA MLENDA/BAMIA HALAFU KUKU!!!


UGALI WA MAHINDI
MLENDA /BAMIA AMBAYO HUPIKWA KWA KUCHANGANYA NA MBOGA YA MABOGA..Msiogope,,,yaani ugali na mletu tu ....hapana
atachinjwa na huyu jogoo akijitokeza mchinjaji kwani mwenyewe naogopa...Kwa hiyo jitokezeni ...
KARIBUNI SANA..KWA WENGINE SASA NI ASUBUH, WENGINE MCHANA , WENGINE WANAENDA KULALA NA HAPA SASA NI MUDA WA KUPIKA CHAKAULA CHA JIONI KWA HIYO KARIBUNI SANAAAAA....

9 comments:

  1. Da'kadala mimi nimeshakaribia,Mmmmhh Tamu saana!!duh umenitia hamu ya chakula wacha kabisa.Mimi huyo kuku simuhitaji dada yangu Mlenda/lift tuu Watosha!!!!!

    ReplyDelete
  2. Kachiki! nimekuelewa hata mie wala huyo jogoo sitamchovya hata kidogo maana huo mlenda matonge yatakavyotelemka sina hata maelezo..Ila labda akina Kadoda na wengine hawakuli mulenda inabidi kujiandaa unajua:-)

    ReplyDelete
  3. Huo msosi jamani....huwa nakula hadi nanyoosha miguuu...asante hata walau kwa picha tunakula

    ReplyDelete
  4. Ester! umenichekesha kweli eti unakula mpaka unanyoosha miguu...una vituko wewe. Vyakula vyetu bwana vitamu na rahisi..hii ndio mimi napenda.

    ReplyDelete
  5. Yasinta na Da Rachel nazielewa hamu zenu...kwa kweli poleni sana..

    ReplyDelete
  6. Dada Mkuu msaidizi! Ahsante basi kula na kwa ajili yetu pia au turushie nasi vya huko nyumbani...yaani mpaka wivu...LOL

    ReplyDelete
  7. Hahahaahahha MONITA DA'Mija wakati wako huuu dada...mimi chichemi wala chitemi na chimung'unyiiii

    ReplyDelete
  8. Heee Da Rachel nishakuwa monita???...Aisee nimekipenda sana cheo...

    Dada Mkuu nimekusikia dada, na ni kweli una haki ya kupata wivu maana huku ni neema tupu...

    Pamoja daima.

    ReplyDelete
  9. Dada mkuu msaidizi! zamu yangu ikija nami nitakuwa na hizo neema nawe itakuwa zamu yako kuona WIVU:-)

    ReplyDelete