Wednesday, August 29, 2012

MTOTO/KIJANA AFUNGA NDOA NA MAMA YAKE MZAZI BAADA YA BABA YAKE KUFARIKI -SONGEA!!!



Mke na Mume, Bi Condorada Ngonyani (70) na Bw. Joseph Mapunda, ambao ni Mama na Mwanawe, wakiwa nje ya nyumba ya Mganga, wakati walipofikishwa kwa suala hilo la Mama Mzazi na Mwanawe kufunga ndoa.
*********************************************************************************

Na Mwandishi Wetu, Namtumbo Ruvuma
MARA kadhaa kumekuwa kukijitokeza matukio mbalimbali ya kustaajabisha, kusikitisha na kutisha na mengine yakihisiwa kuwa ni imani za kishirikina, ambapo mengi ya matukio hayo ambayo hutokea si kwingine ni hapa hapa nchini kwetu, huwaacha watu hoi na maswali mengi yasiyokuwa na majibu.
Kwa mara nyingine tena tukio la kushangaza na kutoaminika kama ni kweli ambalo huwezi hisi kuwa ni la imani za kishirikina, kwani wahusika wote wamefanya hivyo kwa malengo na kuweka wazi sababu za kufanya hivyo japo si sahihi kwa itikadi za kidini, mila na destuli za mtanzania.
Tukio hili ni Mama Condorada Ngonyani (70) mkazi wa mkoani Ruvuma, ambaye aliamua kufunga ndoa na mtoto wake wa tatu wa kiume wa kimzaa na kuishi naye kinyumba kama mke na mume, ambapo wameonekana wao kama wao kuwa wapo sahihi na kuwashangaa wanadam, majirani zao na Jamii kwa ujumla kuingilia mapenzi yao.

Wananchi wapatao 400, wa mkoa wa Ruvuma walijitokeza kushuhudia kimbwanga hii wakati uongozi wa Serikali ya Mtaa walipoamua kuwafuatilia na kuwahoji na kuitisha mkutano wa wanakijiji na kuwaweka hadharani, ambapo Wananchi wa Mkoa wa huo wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maendelo ya Jamii, Jinsia na watoto, kufuatilia kwa karibu suala hilo na kuwaondoa hofu wananchi kama kuna sheria inayomruhusu Mtoto na Mama Mzazi kuweza kuishi kindoa.

Alipohojiwa Mama huyo, Condorada Ngonyani, anasealisema kuwa mara tu baada ya kufariki mume wake, Mzee Mapunda, yeye aliamua kumchagua mtoto wake huyo Joseph Mapunda, ili amrithi baba yake katika kuumiliki mwili wake kama ambavyo alikuwa akifanya Baba yake mzazi, ili kuondokana na tamaa na vishawishi wa kiulimwengu.
Alisema kuwa baada ya uteuzi huo walifunga ndoa ya kimila japo kuna baadhi ya wanafamilia hawakufurahishwa na tukio ama jambo hilo, lakini yeye aliamua kufunga masikio na kuamua kuvunja amri ya sita na mtoto wake huyo wa kumzaa.
Tukio kama hili ni mara ya kwanza kutokea kwa mkoa wa Ruvuma na hata kwa Tanzania nzima, ambapo wakaazi wa Ruvuma wamekuwa wakibaki na maswali mengi juu ya tukio hilo na kuhoji Jamii sasa inaelekea wapi kwa baadhi ya Watanzania kuibomoa wenyewe mila na desturi zetu.
Kwa upande wake, Joseph Mapunda, yeye anasema kuwa upendo na mahaba anayoyapata kutoka kwa mkewe huyo ambaye ni mama yake mzazi, hajawahi kuyapata kokote na kusema kuwa wanapendana sana na wanaheshimiana kama mke na mume.
Josepha amehiji kulikoni wanadam kuwafuatilia katika mapenzi yao na kusema kuwa ''hawa watu wanaotufuatilia hadi leo hii kutuweka hadharani namna hii, wanataka nini kwetu?''.
Wananchi hao waliofurika kwa Mganga wa Jadi Flora Ndembo, wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma, wameiomba Serikali kuingilia kati suala hilo na kuchukua hatua kisheria ili iwe fundisho kwa wanatanzani wengine wenye akili kama hizo za kuharibu mila na desturi za kitanzania kirahisi kama hivyo. Picha na Songea Habari

Bi. Condorada Ngonyani. ''Nawashangaa wanadam kuingilia mapenzi yangu, mtuache''.
Bwana, Joseph Mapunda, ''Wananchi mtatutakia nini na mapenzi yetu''?
CHANZO:HAPA  NA PIA UNAWEZA KUSOMA HAPA. ..
.................................................................................................................................................................
Habari hii imenigusa sana, jamani kumwoa mama yako mzazi /kuolewa na mtoto wako uliyemzaa  kweli? kwanini wasingeishi tu kama mama na mtoto ? huko tunakoenda sasa ni balaa tu. Dunia imekwisha jamani au nini hii sasa...mama ana miaka sabini ...nimeishiwa maneno ya kusema nimebaki natafakari bila kupata jibu....Maisha haya jamani .....

15 comments:

  1. mmmmmm mmmmm mmmmmmm....nitarudi baadae

    ReplyDelete
  2. Ester! najua umepata kiwewe kama nilivyopata mwenzio yaani najaribu kufikiria mama kabeba mimba miazi 9, kamzaa mtoto wake wa kiume, kamlea na kuwa kijana mkubwa halafu...hiii itakuwa si haki kabisa ...Mau weee...

    ReplyDelete
  3. Mh jamani ni katika hali ya kawaida au ni wagonjwa wa akili hao mtu na mwanae, nadhani wanahitaji kupimwa hao. Pia kuombewa mana naona si hali ya kawaida. Labda wana mapepo. Shetani mbaya huyo aliyewaunganisha kuwa wanandoa mana hapo Mungu hayupo.

    ReplyDelete
  4. Kachiki! yaani na hiyo kazi ni KUBWA kwelikweli.

    Usiye na jina! Yaani uliyoyaseme ni ya ukweli kabisa kama vile ulikuwa mawazoni mwangu Mungu na awajie na kuwapa baraka ili wawe mama na mwana si mke na mume..

    ReplyDelete
  5. Kila jambo litokeapo hapa duniani lina sababu,watani zangu wangoni sasa inakuwaje bi mkubwa anaogopa kulithiwa na watu wengine na kumchagua mwanawe.....? lazima kuna jambo kuu lililo msababisha bibi atoe uamuzi huo.Yawezekana familia ilikuwa inammezea mate bi mkubwa ili wamuowe nayeye akawa hana njia nyingine nakumchagua mtoto wake kuepusha hao walio kuwa wana mnyemelea.simnajuwa baadhi ya mila zetu za kurithi mke? mimi ninauhakika hicho nikiinimacho tu ili bimkubwa asibuguthiwe.kaka s.

    ReplyDelete
  6. Haaa!ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni.Sasa wanadamu tunakoelekea tutakuwa hatuna tofauti na wanyama...au wana matatizo ya akili?

    ReplyDelete
  7. Acheni wivu jameni, khaaa! Mtimanyongo hata katika mapenzi?....lol

    ReplyDelete
  8. Ingekuwa Moshi ua Musoma siyo tatizo ni jambo la kawaida dada na kaka mkwe na mkamwana kujivinjari. Ila kwa jamaa zangu wangoni hii kali na mpya. Wambura naona hushangai kwa vile Musoma hiki ni kitu cha kawaida. Bado nangoja akina Kimaro kuja kutupasha kwa kuingilia mapenzi ya watu. Yethu huyu katuumbua kweli kweli. Yethu na Maria hii si ajabu ni fitu fya kawaida.

    ReplyDelete
  9. Hakika hapa hakuna wa kunyoosha kidole kwa mwenzake bali tumevuna tulichopanda.Hizi ndizo athari shirikishi katika mshuko wa maadili ndani ya jamii yetu.Salamu kwa wadau wote wa kibarazani.

    ReplyDelete
  10. Mie sitaki kusema. Ashakumsimatusi, hivi hizo hisia zinatoka wapi jamani kama siyo laana hii? Wengine wanasema wanaweza kufanya hivi kwa sharti la mganga ili kupata utajiri. Hawa wanaonekana hata kubadilisha mboga tu ni tatizo, sasa ni kitu gani hii?
    Mungu na atusaidie.

    ReplyDelete
  11. Hahahhahaahah kaka o"Wambura!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  12. Hiyo kali
    Hayo ni matokeo ya kukata tamaa na kutaoka mafanikio kwa njia ya mkato.

    Tunaangamia na tunakoelekea siko. Hata kama ni mapinduzi sasa hii imepitiliza.
    Tuombe mungu atuepushe na kasi hii kubwa ya kukengeuka kwa jamii tunayoishi

    ReplyDelete
  13. mpaka sasa sijapata jibu jamani.....kuna tatizo tu hapo si bure

    ReplyDelete
  14. HII NAYO MPYA AISEE YESU ANAKARIBIA KURUDI KABISA UKIONA HAYA.....HII NI KASHESHE SANA SIWEZI KUSEMA NI KABILA ILA NI HULKA HII KABISAAAA NA NINAWEZA KUIITA LAANA......MUNGU AWAREHEMU WAMETOA KALI...HAYA NDO MAMBO YANAYOMKASIRISHA MUNGU KABISA HAYA MWEEE NI AJABU SANA SANA

    ReplyDelete