Wednesday, July 11, 2012

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMATANO NJEMA NA UJUMBE HUU!!!

HAYA NDUGU ZANGUNI NI ILE JUMATANO YA KIPENGELE CHA MARUDIO YA MATUKIO MBALIMBALI. KWA HIYO LEO NIMEONA NIWEKE PICHA HII AMBAYO NILISHAWAHI KUIWEKA. KARIBUNI....

Macho ya huruma hufurahisha moyo, habari huburudisha mwili. Kuchukiana huendekeza fitina, kupendana husitiri makosa yote. Nilikuwa mgonjwa ukaja kuniona .Nilikuwa na njaa ukanilisha. Kumhudumia mgonjwa ni wito. JUMATANO NJEMA KWA WOTE . NA KUMBUKENI WOTE MNAPENDWA!!! NA PANAPO MAJALIWA BASI TUONANE TENA WAKATI MWINGINE.

12 comments:

  1. @Yasinta;
    Ujumbe huu wa marudio kikumbusha chenye manufaa kifamilia na kijamii kwa ujumla.Asante na salamu kwako na familia yako kwa ujumla wake.

    ReplyDelete
  2. Mwanamke khanga bwana! Ila hicho kilemba cheusi kinaashiria majonzi na huzuni ... otherwise, pamoja na huzuni inayoonekana bado umependeza sana.

    Salaam nyingi kutoka Ludewa na Manda (Ziwani). Kachiki Muke ya Mubena, nilipita Kidugala na Ilembula nikapata ulanzi (ulasi) wa kutosha.

    ReplyDelete
  3. Asante kwa ujumbe mzuri Yasinta. je unaweza kutukumbusha tukio kuhusiana na hiyo picha yako? siku njema.

    ReplyDelete
  4. Ahsante kwa ujumbe, siku nyingi sijapita hapa kijijini.

    ReplyDelete
  5. Kaka Ray! Ahsante na wewe na salamu zimefika.
    Mtani! Ushukuriwe kwa yote...unamwambia Kachiki mambo ya ulasi unataka aanze kutimka na kuufuata?

    Usiye na jina, hii picha nakumbuka ilikuwa tu kujaribu kuvaa khanga kivihi ninakuwaje?..na ilikuwa muda kidogo kama nakumbuka vizuri 1992-93 Matetereka/Wilima.

    Kadoda Nafurahi kusoma kuwa ni ujumbe mwanana. Uwe na Jumatano njema nawe pia.

    Kaka Yusuf karibu sana, ni kweli ni siku nyingi ila sasa umerudi na naamini utakuwa nasi kawa kawaida.

    ReplyDelete
  6. Asante kwa ujumbe mzuri, j'5 njema kwako na familiapia.

    Mtani; niwekee kilita beeh!!!!Mkangafu na Mtogwa..

    Wenu Kachiki Muke ya Mubena.

    ReplyDelete
  7. @Yasinta;
    Asante sana kwa asante nyingi zilizobebwa na mkao wa kiafrika zaidi hadi Simon kaibuka hukoooooo!!!

    ReplyDelete
  8. Mchungaji Ray.. Unajua lakini we.. wee... ni Mchokozi aisee Mangi ?@Mtani wangu Ray Njau ...Papaa wa Kichaga... KICHAGA AISEE... asiyeku.. asiyekunywa Mbege aisee!:-(

    ReplyDelete
  9. Jumatano njema pia...Mungu akutunze na familia yako.

    ReplyDelete
  10. @Simon;
    Mtu anapoamua kutumia vema silaha yake ya utani wa jadi muache aitumie kwa angalizo la kivulini kwa zamu.

    ReplyDelete