Tuesday, May 8, 2012

TUMEPUMZIKA SONGEA KIDOGO INATOSHA! SASA NAONA TUENDELEE NA SAFARI YETU !TUNAELEKEA KULE ALIKOZALIWA KAPULYA!!!

 Sio kwingine tena ni hapa:- katika  pichani ni moja ya fukwe bora katika ziwa Nyasa eneo la Lundo. Na ndio alikozaliwa mdada huyu. Ni sehemu nzuri sana kwa kutalii ukitembelea maeneo haya siku moja usikose kutembelea na hapa.
Pomonda jiwe la ajabu lililopo ziwa nyasa.
Hili ni jiwe la Pomonda, moja ya vivutio adimu vya utalii ziwa Nyasa ..Kuna mambo mengi katika nchi yetu ambaye ni mazuri na ya kuvutia ebuliangalia jiwe hili  halafu angalia huo ufukwe hapo juu. Mweee mpaka raha kweli. 

3 comments:

  1. Kapulya umenikumbusha Senga Bay kule ng'ambo ya hapo kwenu. Hata hivyo naona wivu kwani mie huku niliko hakuna beach bali shield kwenye prairie Basi, enjoy mwanakwetu.

    ReplyDelete
  2. Umenikumbusha Mbambabay na dagaa wa Ziwa Nyasa wanene na watamu ile mbaya halafu unapata kwa ugali wa mhogo.

    MV Songea sijui bado ipo? Nilipita Ziwani mwaka 1986 na 1987 nikitokea Itungi Port - Kyela kwenda Mbambabay.

    Kilichonitisha miaka hiyo ni barabara ya kutoka Mbambabay - Mbinga ilikuwa ni mwendo wa mawe na vilima na mabonde kibao.

    Natumaini baada ya miaka zaidi ya 25 tangu nipite huko, sasa hivi wanaweza kuwa wameitengeneza na inapitika kirahisi.

    ReplyDelete
  3. Mwl. Mhango! pole kwa kutokuwa na beach..karibu sana hapa kwetu!!

    Mtani!Mwenzio niliwala hao mwaka jana tena wanatoka to ziwani we acha tu bwana..vidole navyo vilinusurika kutafunwa:-)
    MV Songea nadhani bado ipo
    Barabara si mbaya kama miaka ile kwa nilivyosafiri mara ya mwisho.
    Kwa hiyo usiwe na shaka inapita kirahisi ila nami mbamba bay mpaka Lundo nilifika 2007....

    ReplyDelete