SWALI HILI LIMENISUMBUA SANA MUDA MREFU:- KWANINI WAIMBAJI WENGI WA AFRIKA MASHARIKI WAIMBAPO HUCHANGANYA LUGHA?...
Wimbo huu nimeusikiliza mara kadha pia waimbaji wengine wengi tu kuwataja wote itachukua muda. Hivi waingiziapo maneno ya kiingereza ndi wimbo unakuwa mtamu zaidi au? Kwanini kama huyu dada Amani asiseme tu NAKUTAMANI MPENZI WANGU, badala ya hiyo I MISSING MY BABY? Je? lugha yetu ya KISWAHILI haiimbiki?. Naomba msaada wenu/ tujadili kwa pamoja jamani...lugha yetu itapotea!!!!!
Yasinta, Nafikiri kiswahili chetu kina matatizo ya uchache wa maneno. Mfano mzuri ni tafsiri yako ya maneno "I am Missing You", unasema, "Anamtamani Mpenzi wake". Ukishaweka neno "tamani", maana yake inaenda mbali zaidi, anatamani afanye naye mapenzi?
Je, maana ya kum-miss mtu, ni kumtamani? kumkosa? au kumkumbuka? Kati ya hayo maneno lipi ambalo ni sahihi? Mzungu anaweza kusema amem-miss mama yake na ikaeleweka, lakini mswahili hawezi kusema anamtamani mama yake, ni matusi.
Love na Like, kwa kiswahili yana maana moja, PENDA. Mzungu akisema I LOVE YOU, anaonyesha uzito tofauti na akisema I LIKE YOU. Kwenye kiswahili yote utasema NINAMPENDA, kitu ambacho sio sahihi.
Nimalizie kwa kusema kwamba kuna siku tulikuwa na mjadala kuhusu matumizi ya lugha katika ulimwengu wa mapenzi. Dada mmoja alisema ana-enjoy sana akitongozwa kwa lugha ya asili, kwamba iko so romantic na maneno yanayotumika yana uzito unaotakiwa. Anachukia sana kutongozwa kwa kiswahili kwa kuwa maneno ya kiswahili mengi hayana uzito au hayabebi ujumbe unaotakiwa. Anasema ni heri akatongozwa kwa kizungu kuliko kiswahili. Hata anapokuwa kwenye mambo ya faragha, anasema kuna maneno ya kiingereza/kilugha ambayo yakisemwa yanamfanya msichana/mwanamke ajisikie ni Malkia na kwamba anabembelezwa. Kwenye kiswahili maneno hayo hayapo au hayana uzito anaoutaka yeye!
Yasinta usinikate masikio. Da Mija naomba fumba macho usisome.
MDAU,Mtani bado sikubaliani na wewe kwamba lugha yetu inaupungufu wa maneno hapana siokweli ila ni hiyo kasumba yetu ya kutaka kutukuza vya wenzetu na kudharau vyetu,vilevile DADA,Yasinta pamoja na hayo mbona wewe unatumia jina la Yasinta kwani hilo jina ni la asili ya Ruhuwiko?hivyo basi ni kasumba yetu ya kiafrika kuviona vya wenzetu ni safi kuliko vyetu
Watanzania tumeshindwa kuienzi na kuitetea lugha ya Kiswahili katika anga la kimataifa.Dhana iliyojengeka hapa kwetu ni iwapo mtu hawezi kuzungumza Kiingereza huyo siyo msomi katika jamii yake.Lakini jambo hapa ni hili:Taaluma inaweza kuwasilishwa kwa lugha ya yoyote na usomi haupomwi kwa uwezo wa mtu katika kuongea lugha ya Kiingereza.Kwa hiyo kinachoendelea hapa kwetu ni Kiswangereza/Kiswaengilishi na siyo Kiswahili wala Kiingereza.Wenye dhamana ya kusimamia na kuongoza katika jamii ndiyo vinara wa Kiswaengilishi."HUWEZI KUWA MAHIRI KATIKA LUGHA ZA KIGENI KABLA YA KUWA MAHIRI KATIKA LUGHA YAKO ASILIA."
Mtani wa mimi! Ahsante kwa uliyosema. Ila nataka kuwa tofauti kidogo nawe. Maneno: PENDA NA TAMANI...PENDA KWA MIMI NI ILE HALI YA KUMPENDA MTU/KITU YAANI KIKAKUINGIA MOYONI AU PIA KUTOKANA NA KUVUTWA NA UZURI WAKE. PENDA- PIA NI KULE KUKATA USHAURI KUFANYA JAMBO KWA KURIDHIKA MWENYEWE. tUJE HILI NENO TAMANI:- NI KUWA NA HAMU YA KUPATA KITU. Tatizo sisi tunapenda sana vya kuiga. Tunafikiri kusema hivi itachukuliwa uzito zaidi kuliko vyetu. Hivi babu zetu walikuwa wanasemaje hapo zamani? Batamwa! jina langu Yasinta na ndio sio asili ya Ruhuwiko kwa vile mimi si Mtu wa Ruhuwiko yaani sijazaliwa Ruhuwiko. Kwani Yasinta ni jina la wapi sijawauliza wazazi wangu.Je unajua wewe?
Kuchangaya lugha ni kuonyesha msisitizo,...na wengine kuonyesha kuwa `wamesoma' au sio....lakini kiujumla ni kutojiamini. Kuna mtu mmoja alisema; kama huthamini lugha yako wewe ni `mtumwa' kwahiyo sisi ni `watumwa'...sijui lini tutakuw huru.
Wandugu wapendwa ninakubaliana na hoja zenu zote, lakini ninarudi pale pale.
Kiswahili chetu ni lugha ambayo bado inakuwa na tunaendelea kutohoa maneno mapya kila siku. Wakati mwingine tunaishia kuchemsha.
Mwishoni mwa miaka 90, neno "Biodiversity" kwenye kiswahili lilikuwa likimaanisha "Bayo Anuai". Miaka michache baadaye likabadilishwa na kuitwa "Viumbe Anuai".
Tukubali au tukatae, kiswahili chetu kina maneno machache na wakati mwingine tunakosea au tunayatumia pale ambapo hayatoi uzito tunaoutaka.
Yasinta asante kwa uchambuzi. Naomba nifanyie uchambuzi kidogo wa kutafsiri sentensi hizi mbili
1. I like you 2. I love you
Ili kuzitofautisha, utatumia maneno gani ya kiswahili?
Jamani turudi kwenye swali la msingi. Kwanini wana muziki wafrika mashariki wana changanya kiswahil na kiingereza?. jibu ni kwasababu lugha zote zina tiririka vizuri kiuimbaji.kaka s
Kaka Ray nimeipenda nukuu ."HUWEZI KUWA MAHIRI KATIKA LUGHA ZA KIGENI KABLA YA KUWA MAHIRI KATIKA LUGHA YAKO ASILIA."mwisho wa nukuu.
emu3! nina swali moja hapa je usipochanganya lugha hakutakuwa na msisitizo? Mtani! haya maneno Ilike you na Ilove you kwa kiswahili ni neno moja tu zaidi ni kwamba usemapo I love you ikwa kiswahili inabidi useme NAKUPENDA NA KINAMNA GANI UNAMPENDA. Nadhani kama ukimwambia baba, mama, kaka bibi na watajua unawapenda kivipi na ukimwambia rafiki kwa vile ni rafiki yako atajua. kaka Sam! ni kweli kabisa hata mimi nimeliona ili kuwa lipo nje ya mada kiduchu. Kaka S. kama lugha zote zinatiririka vizuri kiuimbaji kwanini wasiimba lugha moja na sio kuchanganya?
Lugha ni sanaa,muziki ni sanaa, haina tatizo kimuziki kuchanganya lugha.nimoja ya ubunifu, kuimba kuchanganya lugha kwani,msananii anajaribu kuwasilisha ujumbe wa muziki kwa lugha azijuwazo na kwa wakazi wa afrika ya mashariki lugha hizi si ngeni na zinaimbika vizuri tu zikichanganywa. hebu tueleze tatizo hasa ninini lugha kuchanganywa,yaani kiswahili na kiingereza ,je ni kimaadili,kijamii,kitaifa,au kama mshabiki tu hupendi.kaka s.
kuna vitu viwili ama vitatu ama zaidi vinasababisha kuchanganya lugha (code switching/mixing)
1. Nia ya kufafanua 2. Kujionyesha 3. Kuwafikishia ujumbe wasiojua lugha moja kati ya unazoziongea 4. Upungufu wa maneno/istilahi sahihai katika lugha moja ya hizo mbili ama tatu
KUFAFANUA hapa ni wakati mzungumzaji anahisi hajaeleweka katika lugha moja. hivyo hutumia nyingine anayojiaminisha kuwa itafikisha ujumbe maridhawa.
KUJIONYESHA Hii ni sababu ya kilimbukeni tu. ni pale mzungumzajia anapotamani kujionyesa kuwa yu-mahili katika lugha zaidi ya moja ilhali wanamzikiliza hawajaonyesha kutomuelewa.
KUPELEKA UJUMBE WA WASIOJUA VEMA LUGHA MOJAWAPO Hapa ni pale mzungumzaji anapoongea wa wasikilizaji akijua fika kuwa sio wote wanajua lugha moja vema. Mzungumzaji huhama kutoka lugha moja hata nyingie kwa nia ya kuwasimulia na waelewe sawasawa. Nyimbo nyingi za dini huangukua sababu hii. Muimbaji atatumia kwa mfano neno Mungu katika lugha mbalimbali mfano, OMUKAMA, MALAFYALE,LESA, etc
UPUNGUFU WA ISTILAHI/MANENO Hapa ni kuwa lugha zinatofautiana katika uwingi wa maneno na ujazo wa maneno katika kufikisha ujumbe uleule. wataalamu wa kutafsiri wanasema hakuna fasili inayoweza kuwa asilimia 100. tafsiri zilizopo ni majaribio tu (attempts). Kwa hofu ya kutoeleweka vema mzungumzaji huamua kutumia neno katika lugha chanzo ama lugha lengwa katika hali ya kutaka kuufikisha ujembe katiaka hali anayoamini kuwa itafikisha ujembe kukamilifu. Baadhi ya wasomi na yes-no zao wanaangukia hapa
Ulimbukeni tu wa sisi tuliotawaliwa.Tunapenda kuiga wanavyoimba Wazungu.Kwanini Mmarekani au Mwingereza au Mwaustalia haweki msisitizo kwa kuyaweka maneno ya Kiswahili?
niliwahi kutembelea marekani. najaribu kumjibu anon wa mwisho swali lake.sisi wa mataifa mengine tulikuwa tukiwatanaia wamarekani kuwa sisi ni trilingual (lugha tatu)au bilingual (lugha mbili) au multilingua (lugha nyingi). tukawa tunaulizani sisi tusio wamarekani kiutani "who is monolingual?" atajibu mtu mwingine "americans" (jibu sahihi ni mzungumzaji wa lugha moja tu).
hii ilikuwa na maana kuwa wamarekani wengi hawana lugha zaidi ya kiingereza. sasa sio rahisi wao kuzungumza kwa kuchanganya na kiswahili au lugha nyingine.
@Mtani umekosea sana kuweka TAHADHARI mwisho wa hoja yako...Baada ya kusoma maoni yako ndo nashukia tahadhari ya Kufunga macho..Wenzio wanawekaga juu kabla ya Hoja...Loh!!!,
Hata hivyo nakubaliana na hoja yako, Lugha yetu haijitoshelezi kihivyo, Nakubaliana pia na Kaka S, na Mwalimu John Mwaipopo. 'Infact' Mwalimu Mwaipopo uko mbali kifasihi...
Nimepita mara moja tu, nitarudi kuendelea na mjadala..
lakini Mtani ukisema lugha yetu haijitosherezi mbona mfano kuna biblia ambazo zimetafsiriwa katika lugha ya kiswahili na hakuna ambapo wameingiza kiinglishi? nikiswahili mutupu?
@Yasinta; ============ Waulize hao wachanganya lugha kwa nini hatuwasikii wakichanganya maneno kutoka lugha zao asilia wakati wakizungumza lugha ya Kiswahili?Tunahitaji uwekezaji katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili lakini wawekezaji wengi wa ndani wanaowekeza katika sekta ya elimu hawaonyeshi nia ya kuchangia kwenye ukuzi wa lugha ya Kiswahili.Au tumesahau ule msemo wa kila mwenye kulia hushika kichwa chake mwenyewe?
Nafasi ya Kiswahili katika Ulimwengu wa Utandawazi 22 10 2009
Na Abeid Poyo
PAMOJA na baadhi ya watu kuibeza lugha ya Kiswahili, harakati za wadau kuikuza lugha hiyo kitaifa na kimataifa zimepamba moto. Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii cha Chuo Kikuu Huria Tanzania kimeongeza idadi ya watetezi wa Kiswahili wanaoamini lugha hiyo inakidhi mahitaji ya kitaaluma na kimawasiliano ndani na nje ya Tanzania.
Mwezi ujao, kitivo hicho kupitia idara yake ya Lugha na Fasihi kimeandaa Tamasha la Sauti za Kiswahili (Tasaki) ambalo pamoja na mambo mengine linalenga kutoa fursa ya kumulika na kutafakari mabadiliko na maendeleo ya Kiswahili katika dunia ya utandawazi ili kuleta uhuru na maendeleo ya kweli. Wasomi wa lugha wanaeleza kuwa lugha ya Kiswahili ni miongoni mwa rasilimali wanazoweza kutumia Watanzania ili kufikia maendeleo ya kweli.
Hata hivyo, mfumo mpya wa kimaisha ujulikanao kwa jina la utandawazi umekuja na upepo mkali ambao kama juhudi za makusudi hazitochukuliwa, upo uwezekano wa Kiswahili kuzolewa na kutupwa baharini na upepo huo. Ili kukumbatia lugha na utamaduni wetu, yatupasa kujenga ukuta imara ambao hautatikisika kwa upepo wa utandawazi. Ukuta huo basi ndio Tasaki ya Chuo Kikuu Huria. Kupitia Tasaki sauti ya Kiswahili itasikika ndani ya nchi, Afrika Mashariki, Afrika na ulimwenguni kote; anabainisha Mwenyekiti wa Tamasha Hadija Jilala.
Jilala na hata wenzake waliobuni wazo la tamasha, moja ya sauti muhimu za Kiswahili zinazopaswa kupazwa hewani na bila shaka kutiliwa maanani na jamii, ni ukweli kuwa lugha hiyo kwa sasa ina sifa ya kutumika kitaaluma shuleni na hata vyuoni. Kuna kasumba imejengeka kuwa hatuwezi kwenda mbele bila Kiingereza au huwezi kuwa umesoma bila kujua Kiingereza. Kuna nchi kama Japan zimeendelea kwa kutumia lugha zao, anaonyesha udhaifu wa hoja ya wanaokipinga Kiswahili kutumika kama lugha ya kufundishia.
Wapo wanaosema Kiswahili hakijitoshelezi kimsamiati. Tunataka tuwatumie wanafunzi katika madaraja mbalimbali kama sekondari na vyuo vikuu kuthibitisha namna wanavyoweza kuitumia lugha hii na ikatumika shuleni kama lugha ya kufundishia, anafafanua zaidi. Anasema kuwa laiti Watanzania wangejua thamani ya Kiswahili, wangejivunia nayo badala ya kushabikia lugha za kigeni hususan Kiingereza ambayo kwa hali ilivyo imeshawafanya kuwa watumwa wa utamaduni wake.
Ukweli wa mambo kwa sasa ni kuwa Kiswahili kinachobezwa na baadhi ya watu wenye mitazamo na kasumba za kikoloni tayari kimeshavuka mipaka ya kitaifa. Ni lugha inayoshuhudia mageuzi na kupiga hatua kubwa katika nchi kadhaa duniani. Watu wengi wanajifunza Kiswahili na vyuo vingi vikiifundisha lugha hiyo; kujivunia lugha yetu na utamaduni wake, tuipe nafasi na dhima maalum katika Nyanja zote za elimu, siasa, uchumi na utamaduni, anaeleza.
Kwa mujibu wa Jilala, tamasha hilo la wiki moja la kitaaluma na burudani linalochagizwa na kauli mbiu ya “Nafasi ya Kiswahili katika Ulimwengu wa Utandawazi” linakusudiwa kutangaza, kueneza, kuendeleza na kuinua lugha ya Kiswahili na utamaduni wake ndani ya zama hizi za mfumo wa utandawazi uliotamalaki duniani. Katika wiki ya sauti ya Kiswahili kutafanyika makongamano, mashindano ya uandishi wa kazi za kubuni kwa shule za sekondari, vyuo vikuu na watunzi wasio wanafunzi, anataja baadhi ya shughuli zitakazofanyika katika tamasha.
Anaongeza: “Kutakuwepo maonyesho ya sanaa na utamaduni, mavazi ya Kiswahili, vyakula vya Kiswahili, majigambo, ngoma, taarab, maigizo, utambaji wa hadithi, muziki wa kizazi kipya na ghani za mashairi mbalimbali”.
Jilala anasema nyanja zitakazoguswa katika tamasha kupitia mashindano ya uandishi wa kazi za kubuni au mada za kitaaluma ni pamoja na elimu, demokrasia, utandawazi, siasa, sayansi na teknolojia, utamaduni, mazingira, sheria, jinsia, ajira, ujasiriamali, Ukimwi, unyanyasaji wa kijinsia, watoto wa mitaani na masuala mengineyo ya kijami
yaani hata movie, utakuta MY WIFE, ndani kimejaa kiswahili, kwanini wasiseme MKE WANGU?
ReplyDeleteYasinta,
ReplyDeleteNafikiri kiswahili chetu kina matatizo ya uchache wa maneno. Mfano mzuri ni tafsiri yako ya maneno "I am Missing You", unasema, "Anamtamani Mpenzi wake". Ukishaweka neno "tamani", maana yake inaenda mbali zaidi, anatamani afanye naye mapenzi?
Je, maana ya kum-miss mtu, ni kumtamani? kumkosa? au kumkumbuka? Kati ya hayo maneno lipi ambalo ni sahihi? Mzungu anaweza kusema amem-miss mama yake na ikaeleweka, lakini mswahili hawezi kusema anamtamani mama yake, ni matusi.
Love na Like, kwa kiswahili yana maana moja, PENDA. Mzungu akisema I LOVE YOU, anaonyesha uzito tofauti na akisema I LIKE YOU. Kwenye kiswahili yote utasema NINAMPENDA, kitu ambacho sio sahihi.
Nimalizie kwa kusema kwamba kuna siku tulikuwa na mjadala kuhusu matumizi ya lugha katika ulimwengu wa mapenzi. Dada mmoja alisema ana-enjoy sana akitongozwa kwa lugha ya asili, kwamba iko so romantic na maneno yanayotumika yana uzito unaotakiwa. Anachukia sana kutongozwa kwa kiswahili kwa kuwa maneno ya kiswahili mengi hayana uzito au hayabebi ujumbe unaotakiwa. Anasema ni heri akatongozwa kwa kizungu kuliko kiswahili. Hata anapokuwa kwenye mambo ya faragha, anasema kuna maneno ya kiingereza/kilugha ambayo yakisemwa yanamfanya msichana/mwanamke ajisikie ni Malkia na kwamba anabembelezwa. Kwenye kiswahili maneno hayo hayapo au hayana uzito anaoutaka yeye!
Yasinta usinikate masikio. Da Mija naomba fumba macho usisome.
MDAU,Mtani bado sikubaliani na wewe kwamba lugha yetu inaupungufu wa maneno hapana siokweli ila ni hiyo kasumba yetu ya kutaka kutukuza vya wenzetu na kudharau vyetu,vilevile DADA,Yasinta pamoja na hayo mbona wewe unatumia jina la Yasinta kwani hilo jina ni la asili ya Ruhuwiko?hivyo basi ni kasumba yetu ya kiafrika kuviona vya wenzetu ni safi kuliko vyetu
ReplyDeleteWatanzania tumeshindwa kuienzi na kuitetea lugha ya Kiswahili katika anga la kimataifa.Dhana iliyojengeka hapa kwetu ni iwapo mtu hawezi kuzungumza Kiingereza huyo siyo msomi katika jamii yake.Lakini jambo hapa ni hili:Taaluma inaweza kuwasilishwa kwa lugha ya yoyote na usomi haupomwi kwa uwezo wa mtu katika kuongea lugha ya Kiingereza.Kwa hiyo kinachoendelea hapa kwetu ni Kiswangereza/Kiswaengilishi na siyo Kiswahili wala Kiingereza.Wenye dhamana ya kusimamia na kuongoza katika jamii ndiyo vinara wa Kiswaengilishi."HUWEZI KUWA MAHIRI KATIKA LUGHA ZA KIGENI KABLA YA KUWA MAHIRI KATIKA LUGHA YAKO ASILIA."
ReplyDeleteEster yaani wewe acha tu...sijui ndo kusemaje?
ReplyDeleteMtani wa mimi! Ahsante kwa uliyosema. Ila nataka kuwa tofauti kidogo nawe. Maneno: PENDA NA TAMANI...PENDA KWA MIMI NI ILE HALI YA KUMPENDA MTU/KITU YAANI KIKAKUINGIA MOYONI AU PIA KUTOKANA NA KUVUTWA NA UZURI WAKE.
PENDA- PIA NI KULE KUKATA USHAURI KUFANYA JAMBO KWA KURIDHIKA MWENYEWE.
tUJE HILI NENO TAMANI:- NI KUWA NA HAMU YA KUPATA KITU.
Tatizo sisi tunapenda sana vya kuiga. Tunafikiri kusema hivi itachukuliwa uzito zaidi kuliko vyetu. Hivi babu zetu walikuwa wanasemaje hapo zamani?
Batamwa! jina langu Yasinta na ndio sio asili ya Ruhuwiko kwa vile mimi si Mtu wa Ruhuwiko yaani sijazaliwa Ruhuwiko. Kwani Yasinta ni jina la wapi sijawauliza wazazi wangu.Je unajua wewe?
Kuchangaya lugha ni kuonyesha msisitizo,...na wengine kuonyesha kuwa `wamesoma' au sio....lakini kiujumla ni kutojiamini.
ReplyDeleteKuna mtu mmoja alisema; kama huthamini lugha yako wewe ni `mtumwa' kwahiyo sisi ni `watumwa'...sijui lini tutakuw huru.
Wandugu wapendwa ninakubaliana na hoja zenu zote, lakini ninarudi pale pale.
ReplyDeleteKiswahili chetu ni lugha ambayo bado inakuwa na tunaendelea kutohoa maneno mapya kila siku. Wakati mwingine tunaishia kuchemsha.
Mwishoni mwa miaka 90, neno "Biodiversity" kwenye kiswahili lilikuwa likimaanisha "Bayo Anuai". Miaka michache baadaye likabadilishwa na kuitwa "Viumbe Anuai".
Tukubali au tukatae, kiswahili chetu kina maneno machache na wakati mwingine tunakosea au tunayatumia pale ambapo hayatoi uzito tunaoutaka.
Yasinta asante kwa uchambuzi. Naomba nifanyie uchambuzi kidogo wa kutafsiri sentensi hizi mbili
1. I like you
2. I love you
Ili kuzitofautisha, utatumia maneno gani ya kiswahili?
Jamani turudi kwenye swali la msingi. Kwanini wana muziki wafrika mashariki wana changanya kiswahil na kiingereza?. jibu ni kwasababu lugha zote zina tiririka vizuri kiuimbaji.kaka s
ReplyDeleteKaka Ray nimeipenda nukuu ."HUWEZI KUWA MAHIRI KATIKA LUGHA ZA KIGENI KABLA YA KUWA MAHIRI KATIKA LUGHA YAKO ASILIA."mwisho wa nukuu.
ReplyDeleteemu3! nina swali moja hapa je usipochanganya lugha hakutakuwa na msisitizo?
Mtani! haya maneno Ilike you na Ilove you kwa kiswahili ni neno moja tu zaidi ni kwamba usemapo I love you ikwa kiswahili inabidi useme NAKUPENDA NA KINAMNA GANI UNAMPENDA. Nadhani kama ukimwambia baba, mama, kaka bibi na watajua unawapenda kivipi na ukimwambia rafiki kwa vile ni rafiki yako atajua.
kaka Sam! ni kweli kabisa hata mimi nimeliona ili kuwa lipo nje ya mada kiduchu. Kaka S. kama lugha zote zinatiririka vizuri kiuimbaji kwanini wasiimba lugha moja na sio kuchanganya?
Ahsanteni kwa shule, waungwana!!!!
ReplyDeleteAhsante da'Yasinta kwa kuanzisha hii kitu.
Lugha ni sanaa,muziki ni sanaa, haina tatizo kimuziki kuchanganya lugha.nimoja ya ubunifu, kuimba kuchanganya lugha kwani,msananii anajaribu kuwasilisha ujumbe wa muziki kwa lugha azijuwazo na kwa wakazi wa afrika ya mashariki lugha hizi si ngeni na zinaimbika vizuri tu zikichanganywa. hebu tueleze tatizo hasa ninini lugha kuchanganywa,yaani kiswahili na kiingereza ,je ni kimaadili,kijamii,kitaifa,au kama mshabiki tu hupendi.kaka s.
ReplyDeletekuna vitu viwili ama vitatu ama zaidi vinasababisha kuchanganya lugha (code switching/mixing)
ReplyDelete1. Nia ya kufafanua
2. Kujionyesha
3. Kuwafikishia ujumbe wasiojua lugha moja kati ya unazoziongea
4. Upungufu wa maneno/istilahi sahihai katika lugha moja ya hizo mbili ama tatu
KUFAFANUA
hapa ni wakati mzungumzaji anahisi hajaeleweka katika lugha moja. hivyo hutumia nyingine anayojiaminisha kuwa itafikisha ujumbe maridhawa.
KUJIONYESHA
Hii ni sababu ya kilimbukeni tu. ni pale mzungumzajia anapotamani kujionyesa kuwa yu-mahili katika lugha zaidi ya moja ilhali wanamzikiliza hawajaonyesha kutomuelewa.
KUPELEKA UJUMBE WA WASIOJUA VEMA LUGHA MOJAWAPO
Hapa ni pale mzungumzaji anapoongea wa wasikilizaji akijua fika kuwa sio wote wanajua lugha moja vema. Mzungumzaji huhama kutoka lugha moja hata nyingie kwa nia ya kuwasimulia na waelewe sawasawa. Nyimbo nyingi za dini huangukua sababu hii. Muimbaji atatumia kwa mfano neno Mungu katika lugha mbalimbali mfano, OMUKAMA, MALAFYALE,LESA, etc
UPUNGUFU WA ISTILAHI/MANENO
Hapa ni kuwa lugha zinatofautiana katika uwingi wa maneno na ujazo wa maneno katika kufikisha ujumbe uleule. wataalamu wa kutafsiri wanasema hakuna fasili inayoweza kuwa asilimia 100. tafsiri zilizopo ni majaribio tu (attempts). Kwa hofu ya kutoeleweka vema mzungumzaji huamua kutumia neno katika lugha chanzo ama lugha lengwa katika hali ya kutaka kuufikisha ujembe katiaka hali anayoamini kuwa itafikisha ujembe kukamilifu. Baadhi ya wasomi na yes-no zao wanaangukia hapa
Ulimbukeni tu wa sisi tuliotawaliwa.Tunapenda kuiga wanavyoimba Wazungu.Kwanini Mmarekani au Mwingereza au Mwaustalia haweki msisitizo kwa kuyaweka maneno ya Kiswahili?
ReplyDeleteMmmmh!
ReplyDeleteniliwahi kutembelea marekani. najaribu kumjibu anon wa mwisho swali lake.sisi wa mataifa mengine tulikuwa tukiwatanaia wamarekani kuwa sisi ni trilingual (lugha tatu)au bilingual (lugha mbili) au multilingua (lugha nyingi). tukawa tunaulizani sisi tusio wamarekani kiutani "who is monolingual?" atajibu mtu mwingine "americans" (jibu sahihi ni mzungumzaji wa lugha moja tu).
ReplyDeletehii ilikuwa na maana kuwa wamarekani wengi hawana lugha zaidi ya kiingereza. sasa sio rahisi wao kuzungumza kwa kuchanganya na kiswahili au lugha nyingine.
@Mtani umekosea sana kuweka TAHADHARI mwisho wa hoja yako...Baada ya kusoma maoni yako ndo nashukia tahadhari ya Kufunga macho..Wenzio wanawekaga juu kabla ya Hoja...Loh!!!,
ReplyDeleteHata hivyo nakubaliana na hoja yako, Lugha yetu haijitoshelezi kihivyo, Nakubaliana pia na Kaka S, na Mwalimu John Mwaipopo. 'Infact' Mwalimu Mwaipopo uko mbali kifasihi...
Nimepita mara moja tu, nitarudi kuendelea na mjadala..
hi.ni ili kuonesha kwamba wanajua sana!
ReplyDeletelakini Mtani ukisema lugha yetu haijitosherezi mbona mfano kuna biblia ambazo zimetafsiriwa katika lugha ya kiswahili na hakuna ambapo wameingiza kiinglishi? nikiswahili mutupu?
ReplyDelete@Yasinta;
ReplyDelete============
Waulize hao wachanganya lugha kwa nini hatuwasikii wakichanganya maneno kutoka lugha zao asilia wakati wakizungumza lugha ya Kiswahili?Tunahitaji uwekezaji katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili lakini wawekezaji wengi wa ndani wanaowekeza katika sekta ya elimu hawaonyeshi nia ya kuchangia kwenye ukuzi wa lugha ya Kiswahili.Au tumesahau ule msemo wa kila mwenye kulia hushika kichwa chake mwenyewe?
Nafasi ya Kiswahili katika Ulimwengu wa Utandawazi
ReplyDelete22 10 2009
Na Abeid Poyo
PAMOJA na baadhi ya watu kuibeza lugha ya Kiswahili, harakati za wadau kuikuza lugha hiyo kitaifa na kimataifa zimepamba moto. Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii cha Chuo Kikuu Huria Tanzania kimeongeza idadi ya watetezi wa Kiswahili wanaoamini lugha hiyo inakidhi mahitaji ya kitaaluma na kimawasiliano ndani na nje ya Tanzania.
Mwezi ujao, kitivo hicho kupitia idara yake ya Lugha na Fasihi kimeandaa Tamasha la Sauti za Kiswahili (Tasaki) ambalo pamoja na mambo mengine linalenga kutoa fursa ya kumulika na kutafakari mabadiliko na maendeleo ya Kiswahili katika dunia ya utandawazi ili kuleta uhuru na maendeleo ya kweli. Wasomi wa lugha wanaeleza kuwa lugha ya Kiswahili ni miongoni mwa rasilimali wanazoweza kutumia Watanzania ili kufikia maendeleo ya kweli.
Hata hivyo, mfumo mpya wa kimaisha ujulikanao kwa jina la utandawazi umekuja na upepo mkali ambao kama juhudi za makusudi hazitochukuliwa, upo uwezekano wa Kiswahili kuzolewa na kutupwa baharini na upepo huo. Ili kukumbatia lugha na utamaduni wetu, yatupasa kujenga ukuta imara ambao hautatikisika kwa upepo wa utandawazi. Ukuta huo basi ndio Tasaki ya Chuo Kikuu Huria. Kupitia Tasaki sauti ya Kiswahili itasikika ndani ya nchi, Afrika Mashariki, Afrika na ulimwenguni kote; anabainisha Mwenyekiti wa Tamasha Hadija Jilala.
Jilala na hata wenzake waliobuni wazo la tamasha, moja ya sauti muhimu za Kiswahili zinazopaswa kupazwa hewani na bila shaka kutiliwa maanani na jamii, ni ukweli kuwa lugha hiyo kwa sasa ina sifa ya kutumika kitaaluma shuleni na hata vyuoni. Kuna kasumba imejengeka kuwa hatuwezi kwenda mbele bila Kiingereza au huwezi kuwa umesoma bila kujua Kiingereza. Kuna nchi kama Japan zimeendelea kwa kutumia lugha zao, anaonyesha udhaifu wa hoja ya wanaokipinga Kiswahili kutumika kama lugha ya kufundishia.
Wapo wanaosema Kiswahili hakijitoshelezi kimsamiati. Tunataka tuwatumie wanafunzi katika madaraja mbalimbali kama sekondari na vyuo vikuu kuthibitisha namna wanavyoweza kuitumia lugha hii na ikatumika shuleni kama lugha ya kufundishia, anafafanua zaidi. Anasema kuwa laiti Watanzania wangejua thamani ya Kiswahili, wangejivunia nayo badala ya kushabikia lugha za kigeni hususan Kiingereza ambayo kwa hali ilivyo imeshawafanya kuwa watumwa wa utamaduni wake.
Ukweli wa mambo kwa sasa ni kuwa Kiswahili kinachobezwa na baadhi ya watu wenye mitazamo na kasumba za kikoloni tayari kimeshavuka mipaka ya kitaifa. Ni lugha inayoshuhudia mageuzi na kupiga hatua kubwa katika nchi kadhaa duniani. Watu wengi wanajifunza Kiswahili na vyuo vingi vikiifundisha lugha hiyo; kujivunia lugha yetu na utamaduni wake, tuipe nafasi na dhima maalum katika Nyanja zote za elimu, siasa, uchumi na utamaduni, anaeleza.
Kwa mujibu wa Jilala, tamasha hilo la wiki moja la kitaaluma na burudani linalochagizwa na kauli mbiu ya “Nafasi ya Kiswahili katika Ulimwengu wa Utandawazi” linakusudiwa kutangaza, kueneza, kuendeleza na kuinua lugha ya Kiswahili na utamaduni wake ndani ya zama hizi za mfumo wa utandawazi uliotamalaki duniani. Katika wiki ya sauti ya Kiswahili kutafanyika makongamano, mashindano ya uandishi wa kazi za kubuni kwa shule za sekondari, vyuo vikuu na watunzi wasio wanafunzi, anataja baadhi ya shughuli zitakazofanyika katika tamasha.
Anaongeza: “Kutakuwepo maonyesho ya sanaa na utamaduni, mavazi ya Kiswahili, vyakula vya Kiswahili, majigambo, ngoma, taarab, maigizo, utambaji wa hadithi, muziki wa kizazi kipya na ghani za mashairi mbalimbali”.
Jilala anasema nyanja zitakazoguswa katika tamasha kupitia mashindano ya uandishi wa kazi za kubuni au mada za kitaaluma ni pamoja na elimu, demokrasia, utandawazi, siasa, sayansi na teknolojia, utamaduni, mazingira, sheria, jinsia, ajira, ujasiriamali, Ukimwi, unyanyasaji wa kijinsia, watoto wa mitaani na masuala mengineyo ya kijami
vimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg
ReplyDelete