Thursday, May 31, 2012

SIJUI TUNAKOKWENDA NI WAPI? AU NI SHETANI ANATAWALA?

Najua wengi mtajiuliza mbona alisema AMEFUNGA MWEZI HUU WA TANO kama ilivyo hapo chini. Lakini baada ya pitapita nimeshindwa kuvumilia na habari hizi zimenisikitisha sana na ndio nikaona niziweka tu nazo kwani ni moja ya habari muhimu katika maisha yetu wanadamu.

 Mama mzazi wa Mtoto aliye nyongwa Mtotot wake kwa kumuvunjwa shingo akiwa chumba cha kuhifadhia maiti wakati mtoto akifanyiwa uchunguzi
Dakitari wa hospilata ya Mkoa Ruvuma Dakitari Mchirika akiuangalia mwili wa mtoto/malaika huyu.
Masikini mtoto mdogo mwenye umuri wa miaka mitatu akiwa amelala chumba cha kuhifadhia maiti baada ya mama yake mzazi akishirikiana na hawara yake ambao wana tuhumiwa kumua mtoto huyo ili asiwabuguzi wawapo kitandani. Na baada ya mauaji hayo waliahidi kuoana.  Hebu angalia watu walivyo hawana huruma akina mama, akina baba, wazee wetu utamaduni wa Mwafirika Mmeuweka wapi ? CHANZO CHA HABARI ni HAPA.  Halafu soma na hii  HAPA . INASIKITISHA SANA KWA KWELI....

11 comments:

  1. Mungu wangu, hivi hawa wana mashetani hawa, wala si akili zao, imenisikitisha sanaaaa

    ReplyDelete
  2. Ester yaani nimenungĂșnika hapa na mwisho nikaona lazima niweka habari hizi hapa. Yaani mama mzazi kabisa kabeba mimba miezi sita na kisha kumzaa mtoto wake na leo anamnyonga bila hata huruma kwa kutaka kuolewa. Je huyo atakayeoana naye hatazaa naye? Malaika kama huyo jamani. Huyu mama lazima atakuwa na shida katika ubongo wake.Nikiwa kama mama imeniuma sana. Na huyo mwingine kamalaika kamwaka na nusu halafu anakaacha mstuni peke yake mpaka mwili unaharibika nakubalina na da´Ester wameingiwa na mashetani hawa wadada/mama.

    ReplyDelete
  3. Siku za mwisho zimefika kama mambo ndio haya ,kwani kila siku mambo mapya yanaibuka ndugu zangu tuzidi kumwomba Mungu

    ReplyDelete
  4. Khaaaaaa siutani kaka Francis, mmhh Duniani kuna Maajabu!!!!!!

    ReplyDelete
  5. Yasinta yaani leo nimeona eti mama mzazi kamchoma moto mikono mtoto wa miaka 4 eti kisa kaiba boga akala. Fikiria mtoto ana njaa kaona mlo kaondoka nao ye anamchoma moto. Mungu tuhurumie

    ReplyDelete
  6. Hayuko sawa huyu mama...!! Na hapo ni mtoto wake, wa mwingine je?

    ReplyDelete
  7. mama na mtoto wanastahili ulizi katika jamii,ulinzi katika afya zao,ulinzi katika maisha yao,ulinzi katika malezi yao.kuna chombo kimoja zamani kili itwa UMATI,pia wizara ya Afya na ustawi wa jamii,wizara ya wanawake watoto na jiinsia.hizi nitaasisi na vyombo vinavyo weza kusaidia tatizo hili lilo tokea,kwani lina muhusu mama na mtoto.nikweli inasikitisha kwa mtoto mdogo kuuwawa hivyo. wahusika wawajibike siyo kuachia polisi tu na mahakama jamii inatatizo wahusika tokeni maofisini tumieni taalumazenu jamii ina wahitaji tekelezeni majukumu yenu.kaka s.

    ReplyDelete
  8. mhhhh !!??hii nayo ni hatari yaani mimi nikiwa fargha na mama watoto wangu mtoto akilia tunaacha kila kitu tunamwangalia kwanza mtoto huyo yeye anaamua kunyonga?nihatari na wala msimsingizie shatani bure ni akili ya kipimbavu sana maana nikiangalia roho inaniuma sana

    ReplyDelete
  9. Inatisha
    Haya ni matokeo ya kutoamini katika utu na ubinaadamu na kutanguliza tamaa na anasa
    Tuwasamehe kwa kuwa hatupaswi kuwahukumu,tumuombe mola amlaze mahali pema mtoto aliyekatishwa uhai wake.

    ReplyDelete