Pale lugha inapokuwa ngumu basi mwokozi wangu ni hizi KAMUSI . Naweza nikasema haya ndio maisha yangu maana utakuta mara nyingine kuna neno na nashindwa kujua maana lakini ukiwa na hizi kamusi mambo poa kabisa. Umewahi kuisoma hii KAMUSI YA KISWAHILI? Kama hujasoma isome utaona utamu wake:-)
Kamusi ni sawa daraja.
ReplyDeleteKamusi,ukikwama neno unaikimbilia, sasa kumezuka maneno mapya mageni,...kwanini tusiyaendeleze hayo hayo yanayojulikana,kama zamani hayakuwepo, basi tuyaite majina hayo hayo ya kiingilishi, ilimradi yameshatua masikioni, maana ukisema `kiyoyozi, au runinga...'mtu mwingine inamuwia vigumu.
ReplyDeleteTukitunga maneno mapya, eti ili yawe tofauti na wenzetu, na ilihali ni mageni masikioni mwetu, tutakuwa na kamusii kuubwa isiyoeleweka,
Tuite tu, komputa, televisheni...kwasababu kiswahili kimejengwa na maneno mageni,...ni mawazo yangu tu jamani.
Kaka Ray! Si uwongo.
ReplyDeleteemu3! Yaani umenipa wazo nzuri kweli. kutunga kamusi ::Ahsante kwa wazo hili ntalifanyia kazi.
hiyo ya tatu kutoka kushoto mstari wa chini ya Thomas Zanzibar ilikuwa kiboko. Ya home niliisahau kwenye treni ya Tazara 1993. Baba hajui hata leo ilikopotelea. Nimejikausha tu.
ReplyDeletehiyo ya Thomas Zanzibar na hiyo ya kwanza kulia mstari wa chini imefanyiwa miendelezo na TUKI.hiyo ya kwanza 2001 na hiyo ya pili 2004. ni vema ukaitafuta au ukija bongo pitia bookshops mbalimbali au hata pale mlimani
nami pia kamusi ni misahafu yangu ya mara kwa mara. Inshalah siku moja najipanga kuandika ya kinyakyusa na kingereza
Kaka John ahsante kwa ushauri ntafanya hivyo. Ukiandika ya kinyakyusa...naahidi nitainunua na halafu nami nitaandiaka ya KINGONI:-)
ReplyDeleteUtamjua tu mpenda ufahamu...si kwa kujitangaza ila kwa matendo.
ReplyDeleteYasinta unaonekana ni mtafutaji ufahamu kwa sana..
Keep it up mwali wetu..
Mija! Ahsante sana kwa kunipa moyo nitafanya hivyo..
ReplyDeletevimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg
ReplyDelete