Wednesday, May 23, 2012

BWANA MATATA HAJUI KUSOMA+KUMBUKUMBU


Mada hii nilishawahi kuiweka hapa kibarazani, lakini jana katika pitapita nimekukta picha kwa prof. Matondo nikakumbuka  kitabu cha bwana Matata na nimeona si mbaya kama tukijadili tena kwa pamoja . NA UKIZINGATIA LEO NI KILE KIPENGELE CHA JUMATANO YA MARUDIO YA MAMBO MBALIMBALI..Haya soma haabari yenyewendiyo hii

Kwanza naanza na kusema NAMSHUKURU  babangu kwa kutunza kitabu hiki leo nimefurahi sananwaeza kuwasomea hata wanangu. Nadhani hata wenzangu mtafurahi pia kukumbuka hadithi hii:-
Bwana Matata yupo mjini, anauliza uliza njia ya hospital. Kuna kibao hapo njiani, lakini haui kusoma kibao.Bwana Matata anaona aibu kuuliza njia tena, anaona aibu kwa sababu hajui kusoma. Sasa anafuata njia ya bomani
Bwana Matata amechoka sana. Amechoka na safari, pia amechoka kuuliza uliza njia. Amelala kwenye kibao, kibao kinasema HATARI. Lakini Bwana Matata hajui kusoma, tena amechoka mno. Amelala njiani kwenye kibao

Bwana Polisi anapita, anamwona Bwana Matata amelala kwenye kibao. Bwana polisi anamwita, mzee vipi? Kwa nini unalala hapa? Huoni kibao? Lakini Bwana matata amechoka sana amelele kama gogo. Polisi amawita tena, kwa nini unalala hapa kama gogo? Kuna hatari hapa. Lakini bwana matata hana habari ya hatari hajui kusoma.

Bwana Matata akaamka, akasimama na kumwambia polisi, nataka kwenda hospitali. Mtoto wangu yupo hospitali ni mgonjwa sana, lakini nimepotea njia. Bwana polisi akasema, umepotea njia? Fuata hii Bwana Matata akafuata njia ile. Kinachoendelea naadhani mnajua 
JUMATANO NJEMA........

7 comments:

  1. Asante sana kwa ujumbe huu, jumatano njema pia na kwako

    ReplyDelete
  2. Ujumbe umefika.Asante sana dada Yasinta.

    ReplyDelete
  3. Ester! Ahsante kwa kuupokea ujumbe bbinafsi namshukuru sana baba yangu kwa kuwapa wanangu hiki kitabu na sasa nao wanakisoma kama nilivyokisoma mimi. Jumatano iwe njema pia kama nilivyosema.
    RAy! kaka wangu, Nawe ahsante kwa kuupokea ujumbe hii..

    ReplyDelete
  4. yani nimecheka hadi basi! hivi unajua dada yasinta enzi zile za utoto kuna mambo tuliyokuwa tunafanya mashuleni au baada ya masaa ya shule kama vile michezo, kusoma vitabu mbAlimbali (TUJIFUNZE LUGHA YETU) siku hizi yamebadilika kwa kiasi kikubwa sana? yani hizi za mzee matata sijui mpinga shughuli za kisomo, ilikuwa so fun and real educative! i miss those days and i think the new generation with invasion of new technology, they miss the opportunity the previous decade generation had! mdako, rede, mama na mwana....yani alot! siku hizi watoto utawaleeza nini, ni tv, computer games & social networking, atasoma saa ngapi Sikiri na Sadiki au related books zilizo kwenye syllabus zao? kina heri mimi sijasema??? kiukweli i miss those days na najiona we were very lucky. mana honestly mfumo ule wa elimu ulitufanya hata tuwe creative zaidi bila kutegemea GOOGLE! pia ilikuwa inatujengea maadili flani kwani vitabu vingi vya Lugha kiingereza na kiswahili vilikuwa na mafunzo tena makubwa mno (maudhui) toka level ya msingi hadi advanced level...mana akina Ngoswe, sijui the river between, things fall apart.....mine boy, song of Lawino!!! dah..ntaendelea hadi kesho......sisemi kama technogia ni mbaya, ila nasema upande wa pili wa shilling inafanya tuwe wavivu sana..mana kila unachotaka uta google...na kama ndo wale wenzangu na mimi, una copy na ku paste! mchezo umeisha....je tunaelekea wapi? idle mind?? am?

    ReplyDelete
  5. Yaani ukimsoma mzee Matata lazima utakumbuka ulivyokuwa na sare za shule enzi hizo...

    Kwani Yasinta baba alikitunza hiki kimoja tuu...

    ReplyDelete
  6. Dorothy! yaani hiyo michezo we acha tu mie unajua bado naicheza mwenzenu kwani si unajua si lazima kua mtoto...

    Mija unamaanisha nini kama baba alikitunza kimoja tu?

    ReplyDelete
  7. Kama kuna kingine nikuombe...hahahahaa!!!!

    ReplyDelete