Friday, May 11, 2012

HUU NI UCHAGUZI WA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO KUWA HII IWE PICHA YA MWISHO WA JUMA!!

DUH1 NIMECHOKA KWELI!!
Ndiyo! Mara nyingi wengi tunachoka sana ufikapo mwisho wa juma. Picha inatoka http://simon-kitururu.blogspot.se/. Haya  jioni njema binafsi bado nabeba maboxi:-)

24 comments:

  1. simonn kituru ni kijana mzuri kwa sura lakini saa nyingine ananiboa na kuandika matusi na yeye sasa ni mtu mzima mwambie akuwe kiakili zaidi sipendi ujinga wake anaouwandikaga ni hayo tu

    ReplyDelete
  2. Duuh si zitang'oka hizo jamani? box jema dadake na mwisho mwema wa wiki kwa wooote!!

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  4. @Anonymous: Asante kwa angalizo! Samahani miandiko yangu kwako nni MATUSI!

    Ngojea nijaribu kujieleza. Mie MAISHANI sijawahi kuandika MATUSI! Na naheshima kweli !

    Kwa hiyo labda ni MTAZAMO wa JAMII au WAKO ambao hugeuza NENO kuwa UKE au SEHEMU za UKE.... kwa kifupi labda ni MTAZAMO tu ambao tunajifunza wakati tunakua kuwa nini ni tusi na nini si TUSI kitu kifanyacho MIMI na WEWE tunatafsiri jambo moja MAISHANI kitofauti!.

    Ila nashukuru kwa kunikumbusha swala na kwa hilo NASHUKURU na UBARIKIWE sana.


    @Dada Yangu Yasinta: Asante kwa kutoacha kunikumbuka kijiweni kwako. @Dada yangu Rachel:Pamoja sana na nafikiri hata leo tumebadilishana mawaza mara kibao katika kijiwe kingine!

    MBARIKIWE SANA WOTE!

    ReplyDelete
  5. Pamoja kaka wa mimi Kitururu,Asante sana kwa mazungumzo ya kubadilishana mawazo!!!Ubarikiwe sana tuu.

    ReplyDelete
  6. Bonge la chaguo.. Kitururu yuko mbali kiupeo..

    ReplyDelete
  7. s.kitururu nimekuelewa kwa ulivyo mjibu anon hapo juu maana na mimi huwa ninashangaa watu uke ukiutamka kwa jina lake halisi wanasema ni matusi!mbona tunapolisema jicho kwa jina lake kuwa ni jicho sio tusi? hivyo huwa ninawashangaa bin adam?au labda angesema huongei kwa lugha ya staha kidogo ningemuelewa.......!!!!!!???

    ReplyDelete
  8. @Anony. : Ndio hapooo!:-(

    Ila tatizo hata USTAHA wa LUGHA nao LABDA ni tafsiri za watu tu!

    Ila naelewa watu wafikiriao asiyeita ``JEMBE´´ , jembe, maana yake ndiye ajiheshimuye na aheshimuye wengine , na kimatusi HATUKANI kisa anatumia TAFSIDA!

    Ila nahisi maswala ya kufichaficha ndio yajitokezayo hata kusiko... hata kule kwa MAJIRANI wamjuaye jambazi ni nani ... kuto MTAJA kisa anaheshimika KIFISADI na anaitwa MHESHIMIWA kwa USTAARABU wa JAMII.Kwa kifupi: USIRISIRI ndio SIRI kubwa ya UMASIKINI wa TANZANIA na WATANZANIA kwa mtazamo wangu.:-(


    Watanzania tuna tabia ya kukwepakwepa mambo mpaka kama kungekuwa hakuna washikao mimba kuna ambao wangeweza kuamini hatuvuliani nguo kisa kuna vyombo vya kuzalishia watoto tunavikwepa hata kuvitamka... ili tusije kujivunjia heshima tufikiriayo ndiyo JAMII inatuhukumu nayo.

    Ila ndio hivyo! Wengine kama mimi nikijisikia kuita UTOKO wa mbwa jike UTOKO, huwa siubadilishi jina na kuuita majimaji mazito ya mbwa jike -kitu ambacho kuna waaminio NATUKANA na sina HESHIMA! Ila naheshima sana tu KIVYANGU!


    Asante kwakunielewa lakini Mkuu!Kwa kuwa kirahisi sieleweki kwa MTAZAMO wa WENGINE!:-(

    ReplyDelete
  9. Asalaam aleykum wa bara na visiwani.Kwa ujumla kila mtu ana uhuru wa kutoa na kupokea habari.Lakini inapokuwa mazungumzo ni kawaida tu na umma hauguswi,hapa usanifu wa lugha na staha havipewi nafasi kubwa.Kwa upande mwingine tunapoingia kwenye mchakato wa kuwasiliana na hadhira ni jambo jema kuzingatia usanifu wa lugha,staha na kuzika maneno yote yenye ukakasi masikioni mwa hadhira.Kumbuka kuwa uhuru wako unaishia pale uhuru wa mwenzako unapoanzia.

    ReplyDelete
  10. Uhuru wa mtu mwingine unaanzia wapi? Na si inasemekana mfanyie mwenzio kama utakavyo kufanyiwa? Sasa Kipimo ni kipi kwa mfano kwako ... hata KITUSI?@Mkuu Ray Njau!

    ReplyDelete
  11. ha ha ha ha ha ha haaaaaaaaaaaaaaa!
    matusi....staha....heshima.....
    kaazi kweli kweli!

    sishangai hayo kutokea yaani!

    ReplyDelete
  12. @Simon;
    Huenda wewe ukahisi kuwa baadhi maneno ambayo wewe kutoka katika papachi za moyo unahisi ni masafi bila ukakasi,maneno hayo kwa mwenzako yakamfikia ndani ya mirindimo ya ukakasi.Huo ndiyo uhuru wake unapaswa kuheshimiwa na hapaswi kulazimishwa kula kitu ambacho anahisi kina ukakasi kwa kuwa kwa mapenzi yako binafsi umeamua kutafuna na kumeza.
    Ni hayo tu kwa sasa,hadi wakati ufaao mada bado ipo hewani.

    ReplyDelete
  13. @Papaa Ray Njau: Wakati tunasubiri wakati ufaao....: Si na mimi nijisikiavyo....ukakasi wangu nao uheshimiwe na sio tu kuonekana ni MATUSI kisa kwa wengine kiukakasi ni MATUSI? Kwani wao na mimi kuna tofauti? Si sie wote ni BINADAMU? Sasa kwanini mimi niheshimu yao na wao wasiheshimu yangu?. Na ungenijua ungejua naheshima kweli hata nisemayo. Kwa kuwa .....ok....ngojea nijinyime UHURU kusema nilichotaka kusema... na ni kwakuwa NHESHIMA na nafikiria wengine kama KAWAIDA YANGU.:-(

    ReplyDelete
  14. SIMONI Asante sana maana mimi nimmjowapo ninayependa lugha yako pamoja na wengine kusema eti inaukakasi lakini hapana sio ukakasi ndio maana kama ulivyosema,mimba zingekuwa hazionekani isingejulikana kama hivyovitu vipo.asante sana Simon pamoja na kaka Njau kwa maneno murua tupopamoja kwasana yaani

    ReplyDelete
  15. kila mtu ana kipaji chake cha kuandika, kusema nk. Na kaka Simon ni mmoja wa watu asemaye kama awazavyo na kuandika. Kitu ambacho wengi wanashindwa na pia kuogopa lakini ni NENO TU ambalo watu tumajijengea kuwa ni tusi.

    ReplyDelete
  16. mhhh hayo maneno mtomoto sana......???!!!

    ReplyDelete
  17. kweli dada Yasinta,hivyo wala si tusi ni mazoea tu mimi nilikuwa na babu yangu huyo ukikaanaye utafikiri wa unasaba na mkuu Simoni Kitururu ,yaani ilikuwa ni kukuvunja mbavu maana alivyokuwa anaisifia hiyo "ndude"utafurahi sana

    ReplyDelete
  18. kiukweli mimi huwa napenda sana Kitururu awazavyo kwa sauti, kwamgu mimi sioni kama ni matusi

    ReplyDelete
  19. Huyu ni jinsia gani? Duh kachoka kweli?

    ReplyDelete
  20. Simon. Kama nimekumisi vile!? Upo? Siku mingi sana mtani

    ReplyDelete
  21. Angalizo:
    Usianze kudadavua mada za mtani wangu Simoni kabla ya kutafakari kwa kina kirefu.Huyu ni mwanazuoni mahiri na makini katika fasihi ya Kiswahili akiwa na kipaji na ueledi katika Kiswahili sanifu wakati wengi wetu ni weledi katika Kiswahili mazungumzo.

    ReplyDelete