NINGEPATA MLO KAMA HUU JIONI HII INGEKUWA RAHA ...
Ndizi za kuchoma , ukipata na kachumbali hapa mambo si mabaya nazimezea mate kweli hapa nilipo...au sijui nikipata hawa senene ila sijawahi kula sijui ni watamu kama kumbikumbi au? Picha kutoka kwa mwenyekiti Mjengwa.
Ama kweli mlo huu ni wenye ladha asilia kwa jioni njema itakayohanikizwa na usiku mwanana wenye ndoto njema na usinginzi mnono.
ReplyDeleteumenikumbumbusha vyakula vyetu vya asili ingawa mara tu watu wafikapo mjini huvisahau tena ukimkumbusha anweza vomit!!!!!!!!
ReplyDeleteRay na Seleman...hakuna vyakula vitamu kama vya asili...bahati mbaya sijapata ndizi wala hao senene nimeishia kutamani tu...
ReplyDeleteyasinta senene ni watamu kuliko kumbikumbi ingawa wewe umeandika kumbukumbu,dar wanauzwa wengi siku ukija watafute
ReplyDeletebatwamwa! kama ni hivyo nimekosa uhondo...nitafuata ushauri wako...Ahsante nimerekebisha kumbikumbi....
ReplyDeleteSenene sijawahi kula sasa sijui kama nzuri, duuh hapo kwenye ndizi chomaaaa duuhh mamaaaaaaaaa ngoja nikimbie wewe dada ni mchokozi sana tuu!!!!!!!!
ReplyDelete