Wednesday, February 29, 2012

UPENDO

LEO NI ILE JUMATANO YA KIPENGELE CHETU CHA MARUDIO YA MATUKIO MBALIMBALI NIMEKUTANA NA HII NA HAPA

Upendo ni ukweli wa ndani ya moyo. Upendo ni msukumo wa ndanina si nje. Maana ya upendo huanza ndani ya mtu na kila mtu anao uzuri wa ndani uliobeba upendo ; hata kama mtu huyo anafanya mabaya kiasi gani, au hata kama anaonekana mbaya kimatendo – mimi naamini kabisa kuwa kila mmoja wetu anayo mazuri ndani mwake, mazuri yaliyobeba upendo.

Upendo ni hali ya mmoja kujitoa kwa faida ya ampendaye bila kudai fidia au malipo. Kwangu mimi: Upendo huvumilia, upendo hufadhili; upendo hauna wivu au majivuno.Upendo hauna kiburi na haukosi kuwa na adabu. Upendo hautafuti kujipendeza nafsi; haukasiriki upesi, hauweki orodha ya mabaya.Upendo haufurahii mabaya, bali hufurahia kweli.Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote.Upendo hauna mwisho.








7 comments:

  1. Nikweli kama hakuna upendo wa dhati hasa kwenye familia zetu kama hutavumilia hakuna kitu kinaitwa upendo ,mkiwa wote mnavumiliana basi amani itakuwepo na uvumilivu bila huo upendo tusitegemee kuwa amani ,Ndoa nyingi zinavunjika kwa kukosa uvumilivu na hapo maja kwamoja inaonyesha hakukuwepo na upendo na ndipo amani ilipotoweka mwisho tunashuhudia wingi wa watoto wa mitaani hii ndiyo mavuno yake
    Asante na namalizia mchango wangu kwa mtizamo wangu ni huo
    DADA KAPULYA JM5 NJEMA
    CHE JIAH

    ReplyDelete
  2. Nikweli kama hakuna upendo wa dhati hasa kwenye familia zetu kama hutavumilia hakuna kitu kinaitwa upendo ,mkiwa wote mnavumiliana basi amani itakuwepo na uvumilivu bila huo upendo tusitegemee kuwa amani ,Ndoa nyingi zinavunjika kwa kukosa uvumilivu na hapo maja kwamoja inaonyesha hakukuwepo na upendo na ndipo amani ilipotoweka mwisho tunashuhudia wingi wa watoto wa mitaani hii ndiyo mavuno yake
    Asante na namalizia mchango wangu kwa mtizamo wangu ni huo
    DADA KAPULYA JM5 NJEMA
    CHE JIAH

    ReplyDelete
  3. Upendo huleta amani, upendo huleta baraka, ....

    ReplyDelete
  4. Ubarikiwe dada Yasinta,Upendo washinda yote!!!!!!!!Mungu tujalie Upendo wa kweli.

    ReplyDelete
  5. Hii naikubali kwa asimilia zote.Hongera na asante sana binti Ngonyani.

    ReplyDelete
  6. Wote mbarikiwe sana kwa kupita hapa na kuacha mchango...
    Upendo kweli ni kitu cha ajabu sana we anagalia mtu anamwacha baba na mama yake na kuishi na mtu ambaye amekutana naye tu...Ila kikubwa kuliko vyote ni uvumilivu na kusikilizana.TUVUMILIANE NA TUSIKILIZANE JAMANI KWANI UPENDO NI FUMBO LA AJABU.

    ReplyDelete
  7. Nikweli kama hakuna upendo wa dhati hasa kwenye familia zetu kama hutavumilia hakuna kitu kinaitwa upendo ,mkiwa wote mnavumiliana basi amani itakuwepo na uvumilivu bila huo upendo tusitegemee kuwa amani
    website design and development in canada ,
    web developer designer vancouver ,

    ReplyDelete