HIVI KWANINI WANAPOJENGA/TENGENEZA HIZI BARABARA HAWATENGENEZI NA BARARA ZA BAISKELI.....
.....Maana hii ni hatari kwa wananchi kuendesha baiskeli hivi fikiria sasa hapa magari mawili yanakutana je huyu kijana maisha yake yataweza kuokolewa kweli? Ni wazo tu la leo.....
Kaka Mcharia! uwepo wa barabara za baiskeli ni muhimu sana kwani ungepunguza vifo vingi tu vya waendesha baiskeli na watembeaji pia. Kama umewahi kufika Songea/Bombambili pale kwenye ule mlima wamekufa watu wengi sana kwa kuendesha baiskeli katikati ya barabara....
Kule Unguja swali hili halina majibu kwa kuwa barabara moja ni kwa ajili ya wote. Lakini sina hakika sana iwapo tunafahamu gharama za ujenzi wa kilomita moja ya barabara ya lami.Hapa uwezo wa nchi yetu kiuchumi unafanya tukubaliane na usemi huu:"KATA KOTI LAKO KULINGANA NA KITAMBAA CHAKO".Hapa tushukuru kwa tulichopata na tuwe waanaglifu katika matumizi ya barabara zetu.
Sio tu barabara za waendesha baiskeli, pia parking katika barabara zetu, hamna kabisa. Kwamfano Barabara kuu ya Dar - Dodoma, ambayo mimi hupita kila mara...ina karibu KM 500, pia ile ya Morogoro - Mbeya, lakini hauoni Parking kabisa, je ukichoka kuendesha gari, unajisikia usingizi unapaki wapi?au kuharibikiwa na gari... Yaani kama una busara lazima utafute sehemu uliingize gari porini, ambapo wengi hawafanyi hivi,wanayaacha magari yao barabarani ovyo tu ndipo unaona ajali nyingi zinatokea karibu kila siku...kutokana watu wanapaki ovyo ovyo magari yao...hakuna Parking, na wengine wanayavamia kwa kuyagonga. Tanzania yetu bado sana elimu ya barabarani, ndio maana unaona hata wanapojenga barabara hawaweki vitu muhimu kama hivyo, sijui viongozi wetu hawaoni na kujifunza wanapokuja nchi za wenzetu au makusudi tu? Kila siku lazima watu wafe kizembe zembe barabarani bila sababu yoyote.
Sisi tumefuata mfumo wa UK. Yasinta siku ukijanitembelea utasema, barabara ndogo ndogo na wote humo humo. Ukikaa nchi zingine halafu ukaja Uingereza utalia...
HIVI KUNA LESENI ZA KUENDESHA BAISKELI? KAMA HAKUNA NI KWA NINI.
ReplyDeleteInabidi kujiuliza ili tuwe na uhakika wa kuwepo barabara za baiskeli.
Kaka Mcharia! uwepo wa barabara za baiskeli ni muhimu sana kwani ungepunguza vifo vingi tu vya waendesha baiskeli na watembeaji pia. Kama umewahi kufika Songea/Bombambili pale kwenye ule mlima wamekufa watu wengi sana kwa kuendesha baiskeli katikati ya barabara....
ReplyDeleteKule Unguja swali hili halina majibu kwa kuwa barabara moja ni kwa ajili ya wote.
ReplyDeleteLakini sina hakika sana iwapo tunafahamu gharama za ujenzi wa kilomita moja ya barabara ya lami.Hapa uwezo wa nchi yetu kiuchumi unafanya tukubaliane na usemi huu:"KATA KOTI LAKO KULINGANA NA KITAMBAA CHAKO".Hapa tushukuru kwa tulichopata na tuwe waanaglifu katika matumizi ya barabara zetu.
Sio tu barabara za waendesha baiskeli, pia parking katika barabara zetu, hamna kabisa. Kwamfano Barabara kuu ya Dar - Dodoma, ambayo mimi hupita kila mara...ina karibu KM 500, pia ile ya Morogoro - Mbeya, lakini hauoni Parking kabisa, je ukichoka kuendesha gari, unajisikia usingizi unapaki wapi?au kuharibikiwa na gari... Yaani kama una busara lazima utafute sehemu uliingize gari porini, ambapo wengi hawafanyi hivi,wanayaacha magari yao barabarani ovyo tu ndipo unaona ajali nyingi zinatokea karibu kila siku...kutokana watu wanapaki ovyo ovyo magari yao...hakuna Parking, na wengine wanayavamia kwa kuyagonga. Tanzania yetu bado sana elimu ya barabarani, ndio maana unaona hata wanapojenga barabara hawaweki vitu muhimu kama hivyo, sijui viongozi wetu hawaoni na kujifunza wanapokuja nchi za wenzetu au makusudi tu? Kila siku lazima watu wafe kizembe zembe barabarani bila sababu yoyote.
ReplyDeleteSisi tumefuata mfumo wa UK. Yasinta siku ukijanitembelea utasema, barabara ndogo ndogo na wote humo humo. Ukikaa nchi zingine halafu ukaja Uingereza utalia...
ReplyDeleteWote nafurahi kila mara mtoapo michango yetu. Mija nitakuja we ngoja tu:-)
ReplyDelete