Thursday, February 23, 2012

BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO YATIMIZA MIAKA MINNE LEO!!!

Mmmmhh! miaka minne leo imefika kama mchezo!!!!

Blog ya maisha na Mafanikio kama mchezo leo yatimiza miaka minne (4) kamili. Napenda kuchukua nafasi hii na kusema:- Hii yote ni kutokana na uwepo wenu ulioambatana na upendo pia ushirikiano mzuri mlionao. Na kubwa zaidi ni kwa familia yangu kwa kuwa bega kwa bega nami. Pia napenda kusema kwa kupitia michango ya wasomaji na wanablog wenzangu nimeweza kijifunza mambo mengi sana. Na ndiyo kwa sababa hii napenda kusema:- AHSANTENI SANA KWA USHIRIKIANO WENU NASEMA TENA KWANI NAAMINI BILA NINYI, NISINGEFIKA HAPA LEO. KWA KWELI NAAMINI KUWA SISI SOTE NI NDUGU NA NI WATOTO WA BABA MMOJA.UPENDO NA UMOJA WETU UDUMU DAIMA NA PIA MILELE!!!!!

20 comments:

  1. Hongera sana jamani, endeleza libeneke letu hili, kwani inaleta mafanikio pia kwetu wasomaji

    ReplyDelete
  2. Hongera sikujua kwamba blog ya maisha na mafanikio imekwenda age kiasi hicho,kazi nzuri keep it up.

    ReplyDelete
  3. Hongera sana mama maisha kwa moyo wako wa kujitolea kwa ajili ya jamii yako.Moyo huo mwema ni kigezo maridhawa kwetu sote katika nafasi zetu ndani ya jamii yetu.Kwa huo nakusihi usilegeze mkono wako wala moyo wako usijikwae kwa kwikwi kutokana na moni hasi kutoka kwa hadhira.Hapa shukrani ni pongezi ni kwa familia yako kwa kukubali wewe utumie muda ambao ni stahili yao.Nakutakia afya njema,baraka tele,ufanisi bila nukta na kila jambo jema liandamane na michirizi ya nyayo zako njema sana.

    ReplyDelete
  4. Hongera sana da'Yasinta,Mungu azidi kukufunulia yote yaliyo mema na uzidi kutuelimisha,Mungu akubariki wewe na familia yako pamoja na sote tupitao hapa,Pamoja sana Mpendwa.

    ReplyDelete
  5. Hongera sana Maisha na Mafanikio!

    Happy Birthday.

    ReplyDelete
  6. congratulations sister. Keep on the good work.

    ReplyDelete
  7. Yataka moyo,kuwa na blog hongera sana . kaka s.

    ReplyDelete
  8. Kweli kabisa sijapata ona mtu mwenye nguvu ya kublogu kama wewe...Yaani nakupa kila hongera Yasinta. Yaani wakipatikana 50 kama wewe wanaume wamekwisha.

    Happy 4th birthdate Maisha na Mafanikio Blog.

    ReplyDelete
  9. Hongera sana MAISHA BLOG, chini ya dereva wake dada Yasinta, tunakutakia maendeleo mema na maisha mema pia, TUPO PAMOJA DAIMA

    ReplyDelete
  10. hongera sana si kwa vile ni mdada tunpongeza waelimishaji jamiimwanamke akiwa mwelimishaji taifa linaelimika kauli ya siasa ila kauli ya wanablog ni kuwa ukiwa na jambo mwelimishe mwenzio usikae nalo moyoni
    HONGERA SANA
    CHE JIAH

    ReplyDelete
  11. Happy birthday Maisha na mafanikio, Yasinta mungu akuzidishie hekima na kukupatia afya njema kila siku.

    ReplyDelete
  12. Hongera Yasinta kwa kutuhabarisha na kutufundisha, Mungu akupe umri mrefu na afya njema ili Blogu yetu ya maisha na mafanikio ifikishe miaka mingi zaidi!

    ReplyDelete
  13. Napenda kuchukua nafasi hii na kuwashukuruni wote kwa kuitakia blog hii mema na pia kumtakia Kapulya naye mazuri. Mwenyezi Mungu na awabariki na azidi kuwaongezea upendo. Ruksa kuandelea kusema lolote. Karibuni sana ...

    ReplyDelete
  14. Miaka minne???

    Blogu yako ingekuwa mtoto ingekuwa imeshajifunza matusi yote yaliyomo duniani...yaani uwezo wa lugha kamili!


    Hongera sana, Mdogo Wangu, Kapulya.

    Nakushukuru kwa kuwa blogu yako siyo kama mtoto. Haina matusi, bali yajenga tu, maadili mazuri.

    Pamoja nawe!

    ReplyDelete
  15. Better late than never! Hongera sana rafiki yangu tupo pamoja daima kuona na kufurahia mafanikio yako!

    ReplyDelete
  16. Nafikiri sijachelewa sana kukupongeza dada yangu Yasinta, hongera mno kwa hatua hii!

    ReplyDelete
  17. Pamoja na ugeni wangu hapa nimekula matunda mema,Ongeza bidii Dada usirizike na mafanikio uliyopata ili uzidi kufanikiwa zaidi.

    ReplyDelete