Thursday, January 19, 2012

WAZO LA KUFUKIRISHA KWA ALHAMISI YA LEO KUTOKA KWA KAPULYA!!

Hivi ni mimi tu au nawe mwenzangu umewahi kufikiria ya kwamba:- Ni ajabu watu wengi wanajua vipi komputa au gari vinafanya kazi. Lakini HAWAJUI/HAWAJIJUI WENYEWE WAPOJE/WANAFANYA KAZI VIPI.
NAWATAKIENI ALHAMISI NJEMA NA FIKRA NJEMA!!!

6 comments:

  1. NI KWELI. HATUJIULIZI MENGI KUHUSU SISI HASWA. MTU ANAHISI NJAA ANABUGIA CHOCHOTE. AKIHISI SPHINTER ZINATAKA KUPANUKA ANAJIFUNGA CHOONI. BILA KUJUA MLOLONGO HUU. HATUJUI AKILI HUFANYAJE KAZI HATA MIFUMO MINGINEYO. ETI WEWE UNAJUA NI KWANINI UNAKUWAGA NA MIHEMKO YA KUFANYA TENDO LA NDOA NA KULIFANYA?

    ReplyDelete
  2. hayo yote ni maumbile hayana ujanja

    ReplyDelete
  3. Mimi tukiachana na ya WATU bado hata Gari na Komputa kwa bahati mbaya hata hivyo sijui vyafanyaje kazi!:-(

    Kwangu kilakitu na kila siku ni shule!

    ReplyDelete
  4. Nafikiri hii sanasana ni upande wetu sisi pande ya bongo/afrika vitu vingi huwa hatutaki kuingia kiundani kutaka kujuwa.mfano vifaa vya umakanika/ufundi kwa wenzetu havikosekani ndani.mimi niliumbuka sikumoja tumemtembeli bibi(upande wa mkewangu) yule bibi akaomba tumsaidie kurudishia kibao kilicho andikwa marufuku ku paki gari hapa. vikaletwa vifaa vya kazi mwanaume ni mimi,ja po wife ile kazi anaweza ila ilihitaji nguvu kidogo ya mwanaume,sasa kila nikichukua kifaa cha kutobolea mashimo ndugu yangu nilihangika sana.lakini nimuhimu kujiuliza kweli.asente mtoa hoja. kaka s

    ReplyDelete
  5. Habari
    Ni kweli wazo la kufikirisha.
    Hicho unachosema cha sisi binaadamu kutokua kuwa tunafanyaje kazi ndicho kinachaotusababishia tuliowengi kuhangahika huku na kule bila ya kufanikiwa.
    Tulio wengi hutfahamu tnataka nini na ndiyo maana siyo rahisi kujua tunafanyaje kazi.
    Tuna safari ndefu ya kufika huko hasa katika kipindi hiki cha ufahamu na maarifa tusijitahidi kujua sisi ni nanai na tunataka nini katika maisha tutaishia kulalamika ,kulaumu na kulani.

    Nadhaniitunatakiwa kufahamu kuwa maisha ni kujua nini unataka na kufanya kile unachaokitaka na ndipo unaweza kujua jinsi gani unafanyakazi.
    Kila la kheri na kazi njema.

    ReplyDelete
  6. Kamala, usiye na jina, Simon, kaka Sam na kaka Salehe wote nawashukuru kwa mchango wenu mbarikiwe sana kwa kupita hapa na wengine wote waliopita hapa.
    Maswali ni mengi lakini majibu ni kidogo. Naona nitaendeleza mada hii mwanzo wa juma kuna kitu nimejifunza hapa kuhusu kujijua...

    ReplyDelete