Tuesday, January 17, 2012

TAREHE 17 YA MWEZI WOWOTE ULE INANIFANYA NIMKUMBUKE SANA MAMA YANGU!!


Sijui nina nini kila mwezi ifikapo tarehe 17 huwa ninakosa raha sana. Kwa hiyo leo mtaniwia radhi kama sitakuwa mtembezi katika vibaraza vingine pia kama nitamjibu mtu ovyo, Yasinta/kapulya

15 comments:

  1. Yasinta,pole sana , na hongera kwa kuwa na siku maalumu na muhimu katika maisha yako, ambayo ni 17 na hii ni kwa sababu zako. Dada yangu tarehe kuminasaba, umeichaguawa kuwa siku ya kumbukumbu ya mama yako kipenzi,nakatika kumbukumbu hiyo ume weza kupata nguvu ya kuweza kutu shirikisha nasisi akina sam ili tuwe pamoja kimawazo na hata kifikra,hilo nalikubali.mama nikiungo ama ni mtu mmoja muhimu katika kuwepo kwetu hapa duniani.hapa duniani kila kitu ambacho kwa uwezo wa binaadamu ukitaka kukifanya kina wezekana,ilimradi ukiwa nadhamira.hivyo basi maamuzi mengine yanaweza yakatujengea tija,ama yaka endelea kuku fanya mtumwa wa hicho ukiaminicho,ukijiwekea utaratibu nibudi uhakikishe una udumisha,iwekatiaka raha nashida,huo ni uamuzi ambao ni wakibinadamu. sasa katika kumbukumbu hii wewe pia kama mama igeuze kuwa ni siku ya furaha kwako na familia yako, na wala si siku ya kuku fanya kuwa mtu wa huzuni amakukosa raha,nasema hivyo kwa sababu wewe ndo unajuwa kwanini tarehe hii ni muhimu kwako,ili usiwe mtumwa wa tarehe na kutosababisha mikwaruzo isiyo na lazima,ishi kwa uhuru zaidi, hapa duniani kwa kukubali kuwa kilajambo lililo kukuta kimaisha limepita na lilitokea/kuja kwa wakati wake hivyo maisha nikusonga mbele siyo kuhifadhi matukio ambayo yako nje ya uwezo wako,kuwa na kumbukumbu moja kwa mwaka, na siyo kila mwezi utakuwa huru na mwenye amani daima,kubali matokeo. naomba radhi kama nimekukwaza dada yangu,kaka s

    ReplyDelete
  2. Asante kwa taarifa hiyo na acha siku hii iwe njema kwako japo kihisia siyo njema kwako.

    ReplyDelete
  3. Kaka Sam!Nimekuelewa kila neno uliloandika na wala hujanikwaza kabisa..Kama nisemavyo kila siku panapokuwa na wengi kuna la kujifunza. Kwa hiyo nami leo hapa nimejifunza mambo mengi sana na labda mambo ambayo yanaweza kuyageuza maisha yangu. AHSANTE SAM.

    Kaka Ray! usikonde nitaifanya iwe siku njema na kama ulivyosema ingawa si kihisia. Ahsante.

    ReplyDelete
  4. Asante ,kwa kuwa sija kukwaza.kuna mambo mengi ninge weza kuyaweka humu lakini kitaaluma yangu,nashindwa,ila huamini sikuzote ipo siku kutakuwa na njia nzuri ya kuwasilia,twende taratibu time ikifika itawezekana.leo uko nyumbani nini? hujaenda kubeba kaboksi!? kaka s

    ReplyDelete
  5. Maisha na mafanikio ni darasa la wote na mwenye kiu ya elimu na maarifa asikose kupitia hapa na kuacha madokezo chanya au hasi kwa manufaa ya wadau wa kibaraza cha mama maisha.
    "ELIMU NI SEHEMU YA MAISHA NA MAFANIKIO"

    ReplyDelete
  6. Kaka Sam! Pamoja daima...Namshukuru Mungu leo nipo off..Usiwe na shaka siku moja tutasema milima haikutani ...

    Kamala ntafuata ushauri wako Ahsante. Ila sio kusahau bali kupunguza machungu..

    Ray kwa mara nyingine ahsante kwa yote na hasa kwa kuona Maisha na Mafanikio ni darasa.

    ReplyDelete
  7. Pole sana dada yangu,Mungu akupe Nguvu na Atawale juu yako na familia pia,Pamoja ndugu yangu.

    ReplyDelete
  8. Nataka ni we pamoja nawe umekuwa mkweli kwa hilo ndo kisa watu wamekupa ushauri jitahidi kuwa mtulivu hasa unapokuwa na jambo moyoni jaribu kupata ushauri kama huu waliokupatia wana maisha kwani maisha si kukwazika maisha ni kufurahi ,ila wewe unachokifanya ni kizuri ila si kila tarehe ya mwezi ebu fikiria miezi mingapi katika mwaka jaribu kuweka siku moja kwa mwaka ya kukumbuka na kutafakari tunajuwa mtoto kwa mama hakuwi hasa wa kike na wewe sasa ni mama unatakiwa uwe mvumilivu pole kwa hilo dada Yasinta
    Che Jiah

    ReplyDelete
  9. Haya yasinta ushauri umeusikia huo...

    ReplyDelete
  10. Rafiki yangu nipo pamoja na wewe daima! Nimependa sana pia ushauri wa kaka Sam, nami nimeokota langu moja hapo - kukubali matokeo! Leo ni siku mpya rafiki yangu natumaini umeamka na hisia njema.

    ReplyDelete
  11. Mungu azidi kukuimarisha ,

    ReplyDelete
  12. kWA MARA NYINGNE TENA AHSANTE WOTE WOTE KWA KUWA NAMI KATIKA TAREHE HII NA NA KWA USHAURI WETU KILICHOBAKI NI MIMI KUTEKELEZA. HAKIKA PALIPO NA WENGI PANA MENGI. NAWAPENDENI WOTE.

    ReplyDelete