Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kunilinda salama mpaka kufika siku hii ya leo na kuongeza limwaka limoja zaidi. "AU uzee". Namshukuru kwa kuniepusha na mambo mabaya, magonjwa na pia vishawishi. Pia nawshukuru sana wazazi/walezi wangu kwa kunilea na kuwa kama nilivyo. Na halafu napenda kuwapa HERI YA KUZALIWA wote waliozaliwa mwezi huu walitimiza tayari miaka na watakaotimiza siku zijazo.
NAPENDA PIA KUSHEHEREKEA SIKU HII KWA WIMBO HUU:-)
NAMSHUKURU MUNGU KWA YOTE, FAMILIA YANGU PIA NINYI NDUGU ZANGU NA MARAFIKI WOTE NA NASEMA NAWAPENDENI SANA:-)
Heri nyingi sana Dada Yasinta kwa kuzaliwa upya: HAPPY BIRTHDAY...Kila laheri katika maisha yako.
ReplyDeleteMimi ni tarehe 05/02.
Hongera sana da'Yasinta Mungu akubariki sana katika yote yaliyo mema,Akuguse na Kutamalaki katika Kaya yako pia.
ReplyDeleteEpi besdei ya siku ya kuzaliwa kwako dada Yasinta. Mungu azidi kukulinda na kukupa afya njema wewe na familia yako. Amen na ahsante kwa yote..
ReplyDeleteHeri kwa siku yako ya kuzaliwa.Mungu akushushie kila baraka na mafanikio.Enjoy your big day
ReplyDeleteKheri kwa siku yako hii muhimu! Pamoja sana!
ReplyDeleteHongera sana mdada kwa kuongeza mwaka mmja zaidi,Mungu na akupe miaka mingi duniani.
ReplyDeleteheri yako umeifikia mapema mwaka huu
ReplyDeleteMimi nakupongeza kwa hilo na mwenyezi mungu akujalie uishi kama jiwe ila TUNATAKA KUJUWA UNATIMIZA MIAKA MINGAPI? Auunaogopa utaitwa bibi?
ReplyDeleteHongera sana,bibie,kwani maisha nimatamu lakini mafupisana.kula tano binti wa kingoni . unaanza mwaka vizuri kwa kusherhekea siku ya kuzaliwa hongera sana. kaka s.
ReplyDeleteHongera! Na ubarikiwe sana! Sehemu yako mioyoni yetu hachukui mtu mwingine hata siku moja!
ReplyDeletewish you all the happiness in the world! Happy Birthday!
ReplyDeleteDadangu mpeeeeenzi.
ReplyDeleteNI SIKU MUHIMU KWAKO.
Well!!! Si kwako tu, bali hata kwa "WAKO". Yaani wale wote ambao maisha yao huguswa ama kuathiriwa na uwepo wako.
Nami nakuombea kila jema katika maisha haya. Ili mafanikio yakuandame katika kila jema utendalo, busara itawale katika kila uwazalo na maamuzi ufanyayo na kisha watu wauone UKUU WA MUNGU NDANI MWAKO
Happy EARTHday Dada yangu
Haya ndiyo maisha na mafanikio.
ReplyDeleteSalamu kwako,familia,ndugu,jamaa na marafiki.
Kizuri kula na nduguzo na kichungu meza mwenyewe.
"SIKU NJEMA"
nami nakutakia heri na baraka tele za mwenyezi mungu
ReplyDeleteHongera kwa siku yako ya kuzaliwa Mungu akubariki, akuepushe na magonjwa, na vitu vyote vibaya akuzidishe na zaidi uishi miaka mingi kadiri ya yeye apendavyo
ReplyDeleteHappy birthday my love,
ReplyDeleteHongera sana Yasinta!Mungu akupe afya na hekima zaidi,ili uwezo kutujuza sisi wafuasi wako pamoja na kutufundisha!
ReplyDeleteHERI YA KUZALIWA DADA YANGU KAPUYLYA,NAKUOMBEA MAISHA MAREFU NA YENYE MAFANIKIO MAKUBWA SANA.HAPPY BIRTHDAY TO YOU KAPULYA...
ReplyDeletekutokufika kabisa ndio kitu kibaya lakini kuchelewa ni uafrika pia. nadhani sijachelewa kukupongeza kwa kutimiza miaka hiyo. uwe na wakati mujarabu
ReplyDeleteHongera, na kila la heri.
ReplyDeleteYasinta hongera sana dadangu, Mungu akuzidishie miaka na miaka, uzidi kupendeza nje na ndani daima na daima....Na..
ReplyDelete...Mbarikiwe wote mliomtakia heri dada yetu Yasinta.
Kila la heri Mrs K. usilewe sana.
Nachukua nafasi hii kuwashukuruni wote kwa jinsi mlivyokuwa nami siku hii ambayo ndo nilikuja hapa duniani. Mwenyezi Mungu azidi kuwapa moyo wa upendo na azidi kuwapa afaya njema. kuna mmoja ameuliza nimetimiza miaka mingapi? nimeona iwe ni kitendawili ila mwakani nitawaambia nimetimiza miaka mingapi...AHSANTENI SANA na mnakaribishwa kuendelea kutoa pongezi...NAWAPENDENI SANA:-)
ReplyDeleteHongera sana Mama Erick, nakuombea maisha marefu yenye furaha na afya tele
ReplyDeleteHappy belated birthday Yasinta. Endelea kuwa mrembo, mpole, mvumilivu na jasiri.
ReplyDeleteAngie Dodoma
Upole haufai wakati mwingine @da'Angie Dodoma..lol!!
ReplyDeletekila la kheri kwa kuanzimisha siku yako ya kuzaliwa
ReplyDeleteHongera sana Rafiki yangu kwa siku yako ya kuzaliwa. Natumaini siku yako ilienda vizuri. Napenda kukutakia Heri na Baraka tele, Mungu azidi kukubariki, akujalie na akutimizie kile unachokiomba kutoka kwake ukapate kuanza mwaka kwa mafanikio na uweze kutimiza malengo yako yote. Nakufurahia sana rafiki yangu wa hiari!
ReplyDeleteUpole wa ujasiri Da Mija, sio ule wa kuonewa... ha ha haa. unakua mpole lakini jasiri mpaka mtu anakuogopa, ntamuingiaje yule....
ReplyDeleteAngie
Sijachelewa........ nakupa hongera kwa kusherehekea siku yako ya kuzaliwa
ReplyDeleteKaka yako wa hiyari SHABAN KALUSE WA BLOG YA UTAMBUZI NA KUJITAMBUA
happy birthday! umri unaongezeka, nakumbuka miaka ya 80 wakati ule ukiwa mdogo kule mahenge songea.
ReplyDeleteDada M! ahsante sana nawe pia uwe na afya njema.
ReplyDeleteDa´Angie Dodoma! ahsante kwa yote na karibu sana hapa kibarani.
Mija! unataka niwe mkali?
Kaka Salehe! Ahasante sana kwa kuwa nami kwa siku hii.
Kaka yangu wa Hiari Shabani Ahsante sana na wala usiwe na shaka kuwa umechelewa kwani mwezi huu wote ni mwezi wangu..LOL
Wewe usiye na jina nwe nashukuru sana ingawa umenifanya nijiulize mara elfu wewe ni nani maana inaelekea unanifahamu..ningefurahi kujua. AHSANTE.
Aiiii....hata naona aibu kuchelewa namna hii. Ngoja nipige moyo konde tu.
ReplyDeleteHongera Da Yasinta. Ubarikiwe sana wewe pamoja na familia yako !!!
Hongera Yasinta!
ReplyDeleteKaka Matondo na kaka Simon AHSANTENI. uzee naukaribia:-) maana kuongeza mwaka ndo kuukaribisha uzee nasikia.
ReplyDelete