Tuesday, December 20, 2011

NIMEULIZWA SWALI HILI NA RAFIKI MMOJA!!!

Swali:- Hivi Yasinta kukoroma/kuforota (snoring) ni UGONJWA, URITHI au NI KWA AJILI YA UNENE? Maana mwenzio nina shida sana yaani silali kabisa mume wangu anakoroma sana. ....Nikakumbuka pia nilikuwa na rafiki mmoja akija kusalimia tulikuwa na taabu sana na ikabidi kumtenga na alale mbali kidogo nasi. JE? MNAWEZA KUNISAIDIA KUMJIBU RAFIKI YANGU HUYU? NATANGULIZA SHUKRANI....PIA NAWATAKIENI JUMANNE NJEMA...Kapulya

9 comments:

  1. Nashangaa sana mwenye kulalalmika sie yule anaekoroma bali ni mhanga wa makelele yake.


    Pole sana, Dada/Kaka! Lakini nafikiri cha kwanza kabisa MUAMBIE WAZIWAZI UNAVYOTESEKA kwa kutopata usingizi.


    Usipomuambia wewe YEYE KWANZA atajirekebishaje ikiwa anaekoroma hajielewi kwa kuwa kitendo ni cha usingizini mwake?


    Kwamba hayo yote yanasabishwa na unene, ulafi, urithi au nini MUACHIE YEYE AHANGAIKE NA MASWALI KAMA HAYO NA SIYO WEWE!


    Lakini MSINGI umuambie!!!


    Usipomuambia wewe YEYE KWANZA ni sawasawa tu na mtu anaechuckua vya ndoani kuvipeleka nje... MWIKOOO!


    Nimekufikiksha hadi hapo penye uzito katika maoni yangu kwa sababu moja tu. WATU WENGINE WANAPEWA AU KUOMBWA TALAKA KWA KUKOROMA!


    Mwisho namshukuru Kapulya kwa kulileta suala hili tena kibarazani. Kapulya huyo tumempewa na Mungu wetu na tunamshukuru Yeye tu.


    Hata mimi hapa nakoroma usiku kwani mke wangu aliniambia mwanzoni wa mwaka huu. Nimepata ukumbusho nimuulize VIPI MWENZANGU BADO NAKOROMA ili nitafute msaada kwa wa taalamu.

    Lamwisho KABISA: jichunguze nawe binafsi JE KWA NINI USIPATE USINGIZI MZITO USIKU KIASI CHA KUMSIKIA ANAEKOROMA? (labda unahitaji kumuona daktari juu ya STRESS, ANXIETY, DEPRESSION na mambo kama hayo)

    Asante NA pole tena!

    ReplyDelete
  2. Naibu mkurugenzi wa idara ya kupumua katika hospitali ya umma ya chuo kikuu cha Beijing Bw. Han Fang alisema,
    "kimsingi, kukoroma ni dalili muhimu ya tatizo la kupumua usingizini, lakini si kila mtu anayekoroma ana tatizo hilo. Takwimu husika zimeonesha kuwa, robo ya watu wanaokoroma wana tatizo la kupumua usingizini, na pia kwa wale wanaokoroma na wasio na tatizo hilo, wanaweza kuendelea kuwa na tatizo hilo."
    Bw. Han Fang alisema, hivi sasa kuna mbinu nzuri ya kutibu tatizo la kupumua usingizini, njia moja ni matibabu kwa kutumia mashine ya kupumua, nyingine ni matibabu ya upasuaji. Njia hizo mbili zinaweza kutibu vizuri tatizo hilo.
    Mwisho, tujadili tatizo la kupoteza usingizi. kuna ufafanuzi bayana kuhusu upimaji na matibabu ya tatizo hilo. Tatizo la kupoteza usingizi linawapata watu ambao hawaridhiki na muda au ubora wa usingizi wao na maisha yao ya mchana huwa yameathiriwa.

    Kuna vyanzo vyingi vinavyosababisha tatizo hilo, vikiwemo vyanzo vya kisaikolojia, vya mazingira na magonjwa mengine. Hivyo jambo muhimu katika kutibu tatizo hilo ni kutafuta chanzo halisi. Aidha, ni bora zaidi tatizo hilo likitibiwa mapema zaidi, na watu wenye tatizo hilo lazima waende kupata matibabu hospitalini, wala kamwe wasinunue na kutumia ovyo dawa za usingizi, kwani matumizi ya ovyo ya dawa hizo yanaleta madhara kwa afya.
    -----------------------------------Kwa hisani ya China Radio International.

    ReplyDelete
  3. Dawa ya kukomesha kukoroma ni MAZOEZI.

    Mbarikiwe wote jamani.

    ReplyDelete
  4. @ Mija Shija Sayi

    Hilo ndilo neno Bibi weee!!! Na hamna hata daktari mmoja mwenye kulipinga!!

    ReplyDelete
  5. Heee heee...yaaani nicheke kidogo kwanza.Hii habari kubwa....kweli wenye kukoroma asilimia kubwa wana matatizo ya kupumua macho/usingizi.Mie nakoroma na ubavu wangu a pili hali kadhalika basi ukifanikiwa kutusikia tunakoroma kama vita vya chura!!!Mie mtiririko wa kupumua kwangu sio wa kawaida mpaka tabibu ilibidi anifanyie test kuhakiki kuwa sina asma.Kwa jinsi nilivyoambiwa nakoroma nikiwa nimelala jinsi fulani,lakini nd'o ukiwa umelala inabidi ujigeuze.Na nimeambiwa anayeweza kuondoa kukoroma kwangu ni yule atakayerekebisha breathing pattern yangu.Unene unaweza kuwa unachangia kwa kiasi fulani maana mara nyingi watu wanene wana-short breath wakipelekwa mbio katika muda mfupi sana.Unaweza kumwambia ila sidhani kama ataweza badilisha kitu.Sanasana vikichanganya sana(mkoromo)Mguse akiamka anaacha kukoroma...hataacha ile inapunguza speed...haaa haaaa.Pole mwee

    ReplyDelete
  6. Ahsanteni sana wote kwa ushauri wenu nami nitaufikisha kwa rafiki yangu pia naona umekuwa kwa manufaa ya wengi. Mbarikiwe sana wote.

    ReplyDelete
  7. SIMPLY I CAN SAY IT IS A DISEASE.AND IT HAVE CAUSE MANY PEOPLE TO BREAK THEIR MARRIED.IT IS CAUSED BY DIFFICULTIES OF BREATHING ESPECIALLY DURING SLEEPING TIME(OR RESTING TIME).IF IT CAN BE TREATED WHEN IT STARTS BUT IF LATE CAN NOT BE TREATED.CAUSES MAY BE DRINK OF ALCOHOL,SMOCKING,CONTRACEPTIVES WHICH CAUSE RELAXATION OF AIR PASSAGE MUSCLES ETC.IT IS MOSTLY TO ADULT PEOPLE AND FEW NUMBER IN LOWER AGE.FOR THOSE IN LOWER AGE IT ASSOCIATE ALSO WITH SNEEZING.FEW PEOPLE GET SUCH A PROBLEM FROM THIER PARRENT

    ReplyDelete
  8. Kuna maelezo mazuri sana kuhusu tatizo hili katika tovuti hii:

    http://www.helpguide.org/life/snoring.htm

    NB: Bwana Mwita Hardson. Mimi nilitegemea kusoma maoni yako katika Kikurya kumbe mwenyewe ukaamua kutema "Kimombo".....

    ReplyDelete
  9. Madokezo yote kutoka kwa wadau yanathaminiwa sana.Asanteni sana!

    ReplyDelete