Sunday, November 13, 2011

TAREHE HII 13/11 HAPA LEO NI SIKU YA AKINA BABA/FARS DAG!!

Nami nachukua nafasi hii kwa kuwapongeza akina baba, wa kwanza ni baba yangu mkubwa mzee Lotary Ngonyani, wa katikati ni baba yangu wa kati Efraimu Ngonyani na wa tatu ndiye baba yangu mzazi Mzee Gervas Ngonyani. NAJIVUNA SANA KWA UWEPO WENU. MWENYEZI MUNGU AWABARIKI NA KUWALINDA MUWE NA AFYA NJEMA.

Na hapa ni baba yake Camilla na Erik. Hongera kwa siku ya baba baba yetu pia tunapenda kukuambia ya kwamba wewe ni baba bora hata kama kuna ambaye hatakubaliana nasi lakini huo ndio mtazamo wetu. Kwani pale tunapohitaji msaada wako haupo nyuma kutusaidia kimasoma na pia kwa mambo mengine. BABA SISI WANA TWAKUPENDA SANA NA UWE NA SIKU NJEMA KWA SIKU HII YA AKINA BABA/FARS DAG. Hata hivyo tunapenda pia kuwapa HONGERA AKINA BABA WOTE DUNIANI. Camilla na Erik.

9 comments:

  1. Tunawatakia kila la kheri na baraka baba Yasinta, baba erik na wa baba woootee bila kusahu mablogger wooooteee walio mababa.

    ReplyDelete
  2. Rachel! Salamu zimewafikia akina baba hawa. Na Umefanya vizuri kuwakumbuka na akina baba mablogger woteeee NIMEPENDA HII!

    ReplyDelete
  3. Hongera baba mimi. kaka s

    ReplyDelete
  4. Hongera kwa akina baba muhimu sana kutokana nafasi yao katika familia.
    Swali:
    JE NI KWA KADRI AKINA BABA TUMEENDELEA KUTIMIZA KWA UKAMILI MADARKA YALIYOWEKWA MBELE YETU KATIKA FAMILIA NA JAMII KWA UJUMLA?
    ------------------------------------11 Vivyo hivyo wanawake wanapaswa kuwa wenye kuchukua mambo kwa uzito, si wenye uchongezi, wawe wenye kiasi katika mazoea, waaminifu katika mambo yote.

    12 Watumishi wa huduma na wawe waume wa mke mmoja, wakisimamia kwa njia nzuri watoto na nyumba zao wenyewe. 13 Kwa maana wanaume wanaohudumu kwa njia nzuri wanajipatia wenyewe msimamo mzuri na uhuru mwingi wa kusema katika imani kuhusiana na Kristo Yesu.
    ----------------------------
    Vivyo hivyo wanawake wanapaswa kuwa wenye kuchukua mambo kwa uzito, si wenye uchongezi, wawe wenye kiasi katika mazoea, waaminifu katika mambo yote.
    Watumishi wa huduma na wawe waume wa mke mmoja, wakisimamia kwa njia nzuri watoto na nyumba zao wenyewe.Kwa maana wanaume wanaohudumu kwa njia nzuri wanajipatia wenyewe msimamo mzuri na uhuru mwingi wa kusema katika imani kuhusiana na Kristo Yesu.1Tim 3:11-13

    ReplyDelete
  5. Mimi naamini kuwa mashauri ya biblia ni mazuri yenye manufaa zaidi kuliko nadharia na falsafa za kibinadamu.Lakini kwa kuwa kila mtu ana uhuru wake binafsi nami sipendi wala siyo lengo langu kuingilia uhuru binafsi wa mdau yeyote katika tasnia ya habari na mawasiliano kwa jamii kupitia blogu.
    Uchangiaji waweza kufanyika kwa kutumia aina nyingine ya uandishi na ujumbe uwakawafikia wadau kwa kiwango kinachokidhi kiu ya walengwa.Nawatakia wadau wote wa blogu ya maisha na mafanikio siku njema na tulivu kabisa.

    ReplyDelete
  6. Mungu azidi kumpa hekima huyu mzee,

    ReplyDelete
  7. Wote Ahsanteni kwa kuwa na kuadhimisha siku hii ya akina baba. HONGERENI AKINA BABA WOTE.

    ReplyDelete