Tuesday, November 15, 2011

LEO NIMETAMANI KULA MLO HUU/KULA NJUGU!!!!

Nimetamani kweli kula njugu leo, wengi nadhani mnajua njugu ni nini...ni aina ya karanga na zinalimwa kama karanga. Mimi napenda /pendelea zaidi za kuchemsha. basi leo nimepata HAMU na nimeishi kuangalia tu picha hii...Ni zamani mno nilizila

Hapa zimepikwa na viungo....lakini mimi napenda zaidi zile zilizongólewa tu na kuchemshwa kama vile karanga za kuchemsha ila kwa sasa ningapata hizi hapa ningekula ..mmhhhh. Duh ngoja niache kuota... Haya jamani kila la kheri .......

4 comments:

  1. Mapishi maridhawa ni taji lenye thamani kubwa sana katika utendaji wa mwanamke ndani ya familia.Kizuri kula na uwapendao na kibaya kula na......................!
    Swali kwa wadau:-
    Kwa nini wanawake na wapishi wazuri sana katika familia zetu lakini kwenye hoteli wapishi wazuri ni wanaume?Na katika harakati za mwanamke ndani ya mchakato wa maisha na mafanikio kwa nini wanawake hawasikiki wakipaza sauti katika tasnia hii?

    ReplyDelete
  2. Hata mimi huwa nazitamani kweli.

    ReplyDelete
  3. Ray! Ulichosema ni kweli na sijui kwa nini hao akina baba wasiwe wapishi nyumbani pia?...Nafikiri hapa wao fikra zao kuwa wapo kazini na nyumbani ni mwanamke kwa vile inasemekana mwanamke kazi yake na kufua, kuzaa/kulea, kupika ..nk nk. Ila sasa naona kama mambo yanaanza kubadilika na wanawake wanaanza kuwa wapishi katika mahoteli.

    Edna! Mara ya mwisho umekula lini?Pole na mwenzangu pia:-)

    ReplyDelete
  4. "Dada mbona ukutinogesa tavayaku njugu hizi? Nene mata gamemili topu mumulomo kwa hamu ya ve vindu hivi! njugu nikuvifuna sana kwa kweli!"

    ReplyDelete