Thursday, November 3, 2011

Kijiji cha Lilondo wilayani Songea mkoani Ruvuma kinaoongoza kwa kuwa na ndizi nyingi

Hapa ni aina mbalimbali za ndizi ambazo zinapatikana katika kijiji cha Lilondo wilayani Songea mkoani Ruvuma, ndizi hizo zimetoa ajira kwa wanawake wengi wa kijiji hicho hali ambayo imesababisha kupata maendeleo makubwa kiuchumi.

Leo mwenzenu nimekumbuka kweli enzi zili wakati naishi Matetereka. Kijiji hiki na kijiji jirani cha Lilondo kuna ndizi za aina mbalimbali. Wakati ule bei yake ilikuwa ndizi tatu shilingi tano. Halafu watu wa Matetereka pia Lilondo ni wakarimu sana. Licha ya ndizi, kuna magimbi si mchezo, karanga, mahindi, maharagwe, kahawa bila kusahau kinywaji cha ulanzi pia. Halafu kulikuwa na watu walikuwa wakipisha nyama pori...nimeyatamani sana maisha haya... Mtani Fadhy upoooo maana najua hapa vyakula hivi umekua nanyo:-)

13 comments:

  1. NYUMBANI NI NYUMBANI HATA KUWE PANGONI NI NYUMBANI TU!
    -------------------------------------
    Na Yehova Mungu akamchukua mtu na kumweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza._Mwanzo 2:15
    ===================================

    ReplyDelete
  2. nipoooooo juzi jana na leo. ahsante sana da Yasinta kwa ndizi hizi. yaani umenifanya niinuke hapa na kwenda jikoni kula ndizi mbivu maana nazipenda ile mbaya.

    nilipita Lilondo mara sita mwaka 2001. sijapita tena.

    ReplyDelete
  3. Kaka raynjau ni kweli nyumbani ni ni nyumbani na vyakula vya asili ni vitamu muno:-)

    Fadhy! Hujapita Lilondo tangu 2001 duh ni zamani...haya unajua uzuri wa nndizi za Lilondo ni za aina mbalimbali ni chaguo lako...Ha ha ha eti nimekufanya uinuke na na kufuata ndizi watu weweeee. Basi tupo wengi wenye udhaifu wa ndizi:-)

    ReplyDelete
  4. Wadau ni lazima tukubaliane kuwa ndizi mbivu ni miongoni mwa matunda muhimu katika maisha na mafanikio baada ya mikikimikiki ya maisha.
    ==================================
    "PILAU YA JIRANI WEWE WAINUNULIA NDIZI MBIVU"?
    =================================
    "PILAU MWENZAKE NI NDIZI MBIVU"
    =================================

    ReplyDelete
  5. haya wee dada najuwa leo unataka kula pilau ndo kisa ukazikumbuka zile za lilondo mpikie shemeji pilau kesho jumamosi

    ReplyDelete
  6. haya wee dada najuwa leo unataka kula pilau ndo kisa ukazikumbuka zile za lilondo mpikie shemeji pilau kesho jumamosi

    ReplyDelete
  7. Nawaza bado hayo maendeleo ya kiuchumi yaliyoletwa na uwepo wa biashara za ndizi hizo!

    Nipo lakini kijiweni na Ijumaa na WIKIENDI NJEMWA wotewadau wa kijiwe cha Da YASINTA!

    ReplyDelete
  8. @Mtani wangu Ray Njau: <hivi bila BIBLIA unaweza kujitetea weye? Maana DUH ! Kw a kunukuu BIBLIA nahisi utaenda MBINGUNI.

    ReplyDelete
  9. @Mtani wangu Simon;
    Kila kuendako hisani hakurudi nuksani bali shukrani.Biblia ni maktaba kwa ajili ya watu wote.Biblia imesheheni mashauri yote muhimu kwa ajili ya maisha na mafanikio ya mwanadamu baada ya mikikimikiki ya hapa na pale.
    Kifaacho mtu ndiyo chake na wenye ndizi zao ndiyo wanaweza kuelezea hizo manufaa za kiuchumi.

    ReplyDelete
  10. Andiko lote limeongozwa na roho ya Mungu nalo ni lenye faida kwa kufundisha, kwa kukaripia, kwa kunyoosha mambo, kwa kutia nidhamu katika uadilifu,ili mtu wa Mungu awe na uwezo kamili, akiwa na vifaa kamili kwa ajili ya kila kazi njema_2Timotheo 3:16,17.

    ReplyDelete
  11. Ahsante wote mlitoa maoni na mliotembelea TUPO PAMOJA DAIMA.

    ReplyDelete
  12. apa ni lIlondo ira lil,ondo ya leo si ile ya miaka miatatu 4 iriyo pita

    ReplyDelete