Wednesday, October 5, 2011

Sasa tunakaribia Miaka 50 ya uhuru na mfumo huu wa upishi?

Huyu ni kati ya wanake aliyekutwa katika Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma akipika ugali wa mahindi kwa mtindi wa wa kutumia mafiga matatu,kutumia kuni ambazo zinatoa moshi mwingi kwa mama huyu. Katika karne hii ya 21 ambayo inasisitiza maendeleo katika teknolojia Je? huu ni uungwana kweli? au Je una maoni gani katika hali hii? picha kutoka HAPA

9 comments:

  1. YAANI DADAA WE ACHA TU,NA ITAFIKA MIA KWA MWENDO HUU HUU

    ReplyDelete
  2. Kwa mwendo huu hatujaona mafanikio ya miaka 50 ya uhuruuhuru

    ReplyDelete
  3. Mapishi ni mapishi tu. Mimi sioni tatizo hapa ni nini: tena ugali ule ni mtamu kuliko ninaopika mimi kwa kutumia umeme na kama huyu mama akitaka kutengeneza chipsi, pale ni mambo chapuchapu kabisa!


    Labda tungeuliza kihalali kwamba: "Wanaume wako wapi ili wamsaidie huyu mwanamama?"


    Lakini kusema eti kwasababu siku nyingi tumepata uhuru kwa hio asiwepo anaepika namna ile ndio kudai haki isiekuwepo hata katika nchi za Ulaya.

    ReplyDelete
  4. Nimechungulia mara moja, ndugu yangu!

    ReplyDelete
  5. Mhhh hii mada ni nzito sana hasa ukizingatia kuwa ni tathimini ya miaka 50 ya uhuru.Hapa napata kigugumizi kwa kuwa miaka 50 ya uhuru ni maisha na mafanikio ndani ya changamoto kwa watanzania wote.

    ReplyDelete
  6. Hata tukiendelea sana hadi tuwe sjui kama nini, Lakini yahsinta mtu asikwambie kitu, ugali wa dona na tena ummeusongea kwenye mafiga ni mtamu na una raha yake.

    ReplyDelete
  7. kwani hapo cha ajabu nini.. hiyo ni sehemu ya maisha acheni ujinga

    ReplyDelete