Na hapa ni mti wa kako na hizo unazoona zimeningínia ndizo kakao zenyewe hapo bado hazijaiva bado.
Ukimwa mdadisi basi utajifunza mengi ...Yaani nina maana tuliuliza kama kakao zinaliwa kkama zilivyo ..hapo ni matokeo yake tukatafutiwa maoja iliyoiva ikabanguliwa na tukaonja ..sikuwahi kuonja kakao freshi maishani ...ulikuwa msafara ambao tulijifunza mengi sana....
Hapa ni kako zimeanikwa na baadaye zitakuwa tayari kwa kuwa kakao ya unga ..tulishindwa kusubiri mpaka kunywa...Safari nyingine labda.... tembea uone mengi, uliza jifunze mengi nk nk, haya ndio maisha ... kuna mengi yanakuja!!!
Hapa ni kako zimeanikwa na baadaye zitakuwa tayari kwa kuwa kakao ya unga ..tulishindwa kusubiri mpaka kunywa...Safari nyingine labda.... tembea uone mengi, uliza jifunze mengi nk nk, haya ndio maisha ... kuna mengi yanakuja!!!
"MAMBO YA KILIMO KWANZA KWETU TZ."
ReplyDeleteNi kweli maisha bila kila hayatakuwa maisha. Hata kama una kazi ya ofisi lazima kilimo kiwe mstari wa mbele.
ReplyDeleteNa Yehova Mungu akamchukua mtu na kumweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza._Mwanzo 2:15
ReplyDeleteZao hili Afrika Magharibi linadaiwa kushurutisha watoto kiutumwa sana tu lakini!
ReplyDeleteNa maajabu ya Musa ni kwamba nchi maarufu kwa kunywa kakao, kutengeneza chokoleti nk.... wala hazina mashamba haya ya kakao
Tembea ujionee, ... lakini ukishaona kama kifunzwacho hakigeuki tatuzi kivitendo,...
.. mtu usishangae USWISI au tu UBELIGIJI ,.... ndio wasifikao kwa kakao na machokoleti hata baada ya miaka mia kutoka sasa wakati Tanzania au Ivory Coast waongozao kwa zao hili bidhaa zao hazionekani sokoni.... kama tu katika kahawa ilivyo kuanzia katika makapuchino ,.. malate .. na vikorokocho vingine kuwa na majina ya KIITALIANO ambao kwenye kahawa hawana shamba.
Ni mtazamo tu!