Saturday, October 22, 2011

Je umewahi kukisikia kisa cha mnyamwezi kupigwa na mzungu???!!!

Mzungu alikuwa hajuwi aendako yupo kwenye gari alipofika njiani akaona aombe msaada wa mtu wa kumsindikiza kule aendako. Basi mzungu alipoona wamekwenda mbali kiasi akamuliza kijana bado kilometa ngapi" akamwambia twente tu ,basi mzungu akaongeza mwendo kwavile bado kilometa nyingi alipiga mwendo kilometa 22 zikapita akamwuliza tena,bado kilometa gapi ?? Yule kijana kama kawaida akajibu twente tu ,, akiwa namaanisha twende tu hapo mzungu akakasirika akashuka na kumshusha mnyamwezi na kupiga makofi akimwambia kilometa ishirini na mbili ngapi zimepita kila mara unaniambia twenty two why fulish man go out akamwacha pale na mzungu akaendelea na safari akilalamika njia mzima. Nakwambia nimecheka yaani na nadhani hata wewe utacheka na JUMAMOSI YAKO ITAKUWA MURWAAAAAAAAAAA. JUMAMOSI NJEA JAMANI...

8 comments:

  1. Hiki ni kicheko cha Jumamosi,wadau wangu nishikeni mbavu.
    Nasikia waliwahi kukosa ujira wa siku kwa mzungu kwa kila akiuliza jina anaambiwa onani/onene[mimi] naye akaandika hivyo na kujaza orodha yake.Ilipofika jioni akaanza kuita onani/onene hadi mwisho bila mtu kujitokeza kupokea ujira wa siku.
    =====================================
    "JASIRI HAACHI ASILI NA MUACHA ASILI NI HASIDI NA HANA AKILI"
    -----------------------------------
    Njii hii bwana!!

    ReplyDelete
  2. kwakweli hao wakwe zetu wanamambo sana kwani kiswahili ni chao ila hata ukamkuta kaenda shule lafidhi yao ni hiyo hiyo ila nimewapenda kwavile wanathamini uzalendo wao siyo wale kama kaka zako akina ....wakisoma lafidhi ni ile ya kizungu ndiyo maana walipokwenda loliondo kunywa kikombe kwa babu walisema haloo give me mrija man yaani apewe mrija wanywee dawa ya Mzee wa loliondo .nawafagilia wanyamwezi na wasukuma kwa hilo WABEJA SANA.....WABEJA KULUMBA.
    BY
    CHe Jiah

    ReplyDelete
  3. Hahahaa Da Yasinta umenivunja mbavu zangu.Jumamosi njema kwako pia.

    ReplyDelete
  4. Jamani wanyamwezi wanaonewa jamani...Haya kaka S upo hapo? Una la kujitetea?

    ReplyDelete
  5. Kka Raynjau! si uwongo ni kicheko cha jumamosi kweli:-)

    Che Jiah.:-)

    Edna! hiyo ndiyo ilikuwa sababu kubwa kuvunja mbavu...Jumamosi njema nawe pia.

    Mija! sio kuwaonea bwana...haya tuone kaka S atasema nini?

    ReplyDelete
  6. YASINTA UNATAKA KURUDI KITANDANI TENA? WEWE LETA ZAKO ZA KULETA!!?I. KAKA ,S

    ReplyDelete
  7. Kaka S. Ndo umechukia au ha ha haaaa kurudi kitandani tena? sijui kama nimekuelewa kaka

    ReplyDelete
  8. USIKONDE,HIYO INAITWA TISHA TOTO,LAKINI NAONA UKO NGANGARI KINOMA.KUSEMA UKWELI HATA MIMI NIMECHEKA,KWA SABABU SIKUMOJA NAMIMI NILIKUWA NA SAFIRI,TOKA TABORA KWENDA MPANDA KWA GARI,TULIFIKA SEHEMU,TUKAULIZA NDUGUZANGU TENA MIMI KIMBELEMBELE NILIULIZA KWA KILUGHA. JIBU NILILO LIPATA HAKIKA LINAFANANA KWA KIASI FULANI NA HILI LA MZUNGU.MIMI NILI ULIZA JE KUTOKA PALE TULIPOKUWEPO NA KIJIJI KINACHO FUATA KUNA UMBALIGANI. AU NITAPITAVIJIJI VINGAPI ILI NIFIKE,JIBU LILIKUWA ,WENENDA TU MOJAKWAMOJA SIYO MBALI SANA MTAFIKA!!? HAYA TULI ENDA KIASI CHA KAMA DAKIKA 5O HIVI NAKILA UKISIMAMA NA KUULIZA JIBU LINA BAKI NILILELILE WE NENDA MOJAKWAMOJA SIYOMBALI.LAKINI KUNA KITU NIMEJIFUNZA AMBACHO NA MIMI PIA NINACHO KAMA MUHUSIKA JUU YA MASWALI YA UMBALI NA INAMAANA GANI KUJIBU NAMNA HIYO,TUNA AKILI SANA NAMAJIBU YETU HAYA....... SASA MNABISHA? KAKA

    ReplyDelete