HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KAKA DISMAS
Sijui ni uzee au kutingwa? Nilitaka kusahau kuwa kuna kaka anatimiza miaka leo. Nimerudi toka kazini nafungua kitabu changu cha kumbukumbu na kukuta kuwa tarehe ya leo kuna binadamu alizaliwa. Hapo juu ni kaka yangu Dismas akiwa na mjomba wake Erik mwaka huu mwezi wa saba. Wakichezea simu nadhani. Siku kama ya leo kijana huyu alizawa kwa hiyo anapenda kumshukuru Mungu kwa kuwapa nguvu wazazi wake kwa kumlea mpaka kufikia miaka 31 leo. Ukizingatia kwamba na yeye sasa ni baba wa watoto wawili. HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KAKA DISMAS AU SIKU HIZI TUNAMWIITA BABA NOELA AU PIA BABA GIVEN.!!!!!!!
Hongera sana,mungu akuzidishie tena miaka kama hiyo. ombi langu da Yasinta pamoja nakaka yako(bwanamdogo) hapo juu ya meza naziona bunduki mbili/safari pombe inabidi awe ana ziangalia zisizidi zaidi sana maana nazo zina changia sana kupunguza furaha ya mtu katika maisha yakilasiku ukizidisha.kula tana!! kaka s.
ReplyDeleteKwa niaba ya kaka mdogo Disi(bwana mdogo ) ahsante sana kwa pongezi. Kaka Sam! hizo safari hazikuwa kwa ajili yake kwa hiyo usiwe na wasiwasi .
ReplyDeleteHongera. Kumbe siku ile nilipokuwa Songea kama ningesogea hapa Ruhuwiko, kabia kamoja ningeambulia :-)
ReplyDeleteKila la heri.
Prof.Mbele yaani sio kabia tu kwani nilimwambia hata baba akaandaa gujogoo. ila basi safari nyingi...
ReplyDeleteHongera sana kaka Dismas, Mungu akubariki kwa kila jambo.
ReplyDeletehongera ya siku ya kuzaliwa mjomba Dis.
ReplyDeleteHongera Mkuu!
ReplyDeleteheri kwa siku ya kuzaliwa,
ReplyDeleteHongera sana Kaka Disman, Mungu azidi kukulinda kaka.
ReplyDeleteSalamu kwa wote.
Hongera sana, Dismas (Na hapo ni raha tupu kucheza na wajomba!)
ReplyDeleteNachukua nafasi hii na kuwashukuruni wote mlioungani nami kwa kusherehekea siku hii ya kuzaliwa kwa kaka Mdogo Dis. Mbarikiwe sana kwa kuwa na moyo wenye UPENDO.Nami nasema WOTE MNAPENDWA:-)
ReplyDelete