Si muda mrefu uliopita nimerudi toka katika majukumu yangu. Na nikwa nafikiri nipike nini mchana huu mara naangalia Mwananchi mimi nakutana na hii zawadi. Jamani watu wachokozi kwelikweli...Nimebaki mate yanadondoka maana ile kumbukumbu ya tangu utoto na pia juzi tu nilipokuwa MATEMA BEACH nilikula hawa dagaa tena wale waliovuliwa muda huohuo ila si wabichi kabisa. Waliokwa/chemshwa (lighanda) eeeeehhh, eeehh bwana wewe niliwakula na pilipili (sobola) pia chumvi na limao kwa mbali....sasa leo natamanishwa hivi kweli...kazi kwelikweli AHSANTE KWA ZAWADI MTANI FADHY MTANGA:-)
karibu sana mtani
ReplyDeleteAsanteni kwakututamanisha, lakini nitapika Ugali mkubwa na kufungua hapa kwa blog ugaliutashuka tuu kwa hii picha!!
ReplyDeleteIla mtani kwa kweli je hao dagaa walikuwa wabichi/madafu au?
ReplyDeleteRachel umenichekesha yaani wewe huachi mbwembwe haya labda nifuate ushauri wako... ila katutamanisha mweeh...
Hii kitu BOMBA!
ReplyDeletemimi nilijuwa kuwa kwa wewe utakachofanya ni kuupika ugali na kuanza kuula na picha hii ya dagaa na siku ukuletewa likungu mwee sijuwi lile linafaa kwa ugali au ule ugali wa kulowekwa wa muhugo nasikia kuwa ndiyo haswaa mboga yake. mimi sijawahi kulila ila nasikia ni kitu adimu huwa wanawekewa wageni tuu kama siku ukija huku bongo ndo linatolewa kwenye chombo maalumu kilichohifadhiwa kama freji vile kule nyumbani tunaita mtungi.upo hapo dada
ReplyDeleteCHe Jiah
Simon ni bomba muno je ww mara ya mwisho umekula lini?
ReplyDeleteKaka Che jiah! Yaani ungejua nini nilifanya usingesema ila sasa nadhani hao ni wakavu au wanakaushwa kwa ajili ya kuniletea. Ila ingekuwa wale lighanda mweeee! Likungu linalika kwa ugali na kitu kitamu sana. Hilo nadhani nahitaji kufika kulikuli nilikuzaliwa Lundo:-)
Kitu kizuri kula na ndugu zako na kibaya kula na.................!!!
ReplyDeleteR.Njau
"Kitu kizuri kula na ndugu zako na kibaya kula na.................!!! R.Njau" mwisho wa kunukuu Swali kibaya kula na .......nini?
ReplyDelete