Ujumbe huu wa leo naambatanisha na wimbo huu wa Dogo A Matatizo:-(
Ulijua kwamba:- Matatizo ni mazuri kwa vile hukufanya uwe mbunifu. Pili huwezi kukwepa matatizo kama unaishi hapa duniani. Matatizo ni sehemu ya maisha, tatizo kubwa linakuja jinsi unavyoliona tatizo, ukiliangalia tatizo tofauti basi tatizo huwa kubwa zaidi na ukiliangalia tatizo kama sehemu ya ufumbuzi au ubunifu au hamasa ya kufanikiwa na kupiga hatua basi ukipata tatizo badala ya kulalamika na kuona unaonewa utachangamka na kuanza kushughulikia. Nahisi matatizo yangu ninayokutana nayo ni makubwa kuliko yako ila naamini yangu ni yangu na nikiyashinda tu nitakuwa mbali zaidi na nitakuwa mtu wa mafanikio.
Mara nyingi matatizo nayo huwa yanazalisha stress sana kwa hiyo inabidi daima uwe imara kuyatatua lakini siyo matatizo ambayo yanakufanya uumie huku wanaokuumiza hawana chembe ya haki ya kukuumiza angalia usianguke.
Bonge la UJUMBE!
ReplyDeleteAsante sana kwa hili,...
.... halafu nahisi Mubelwa Bandio angekuwa na lakusema kwa kuwa theme ya blogu yake inacheza kwenye ujumbe huu nahisi!
Kweli dada umenena.
ReplyDeletehubiri 6:1-12
ReplyDelete1 Kuna msiba ambao nimeuona chini ya jua, nao hutokea mara nyingi kati ya wanadamu: 2 mtu ambaye Mungu wa kweli humpa utajiri na mali na utukufu, na ambaye, katika nafsi yake, hana uhitaji wa chochote anachotamani, hata hivyo Mungu wa kweli hamruhusu kula kutokana nacho, bali mtu aliye mgeni tu anaweza kula. Hilo ni ubatili na ni ugonjwa mbaya. 3 Mwanamume akizaa mara mia moja, na aishi miaka mingi, mpaka siku za maisha yake ziwe nyingi, lakini nafsi yake haijatosheka na mambo mazuri na hata kaburi halijawa lake, lazima niseme kwamba mtu aliyezaliwa akiwa mfu ni bora kuliko huyo. 4 Kwa maana huyu amekuja bure naye huenda gizani, nalo jina lake litafunikwa kwa giza. 5 Hata jua lenyewe hakuliona, wala hakulijua. Huyu ana pumziko kuliko yule wa kwanza. 6 Hata ikiwa ameishi miaka elfu moja mara mbili na bado hajaona yaliyo mema, je, kila mtu haendi mahali pamoja?
7 Kazi yote iliyo ngumu ya wanadamu hufanywa kwa ajili ya kinywa chao, lakini hata nafsi yao haishibi. 8 Kwa maana mtu mwenye hekima anapata faida gani kuliko mjinga? Mtu anayeteseka anapata nini kwa sababu ya kujua jinsi ya kutembea machoni pa watu walio hai? 9 Ni afadhali kuona kwa macho kuliko kutembea huku na huku kwa nafsi. Hilo pia ni ubatili na kufuatilia upepo.
10 Chochote ambacho kimekuja kuwako, jina lake tayari limetangazwa, na imejulikana mwanadamu ni nini; naye hawezi kujitetea mbele ya mtu aliye na nguvu kuliko yeye.
11 Kwa sababu kuna mambo mengi yanayosababisha ubatili mwingi, mwanadamu ana faida gani? 12 Kwa maana ni nani anayejua mwanadamu anapata mema gani maishani kwa hesabu ya siku za maisha yake ya ubatili, anapozitumia kama kivuli? Kwa maana ni nani anayeweza kumwambia mwanadamu litakalotokea baada yake chini ya jua?
==================================
R.Njau
-----------------------------------Stress=mikazo/shinikizo?
Mhubiri 6:1-12
ReplyDelete-----------------------
1 Kuna msiba ambao nimeuona chini ya jua, nao hutokea mara nyingi kati ya wanadamu: 2 mtu ambaye Mungu wa kweli humpa utajiri na mali na utukufu, na ambaye, katika nafsi yake, hana uhitaji wa chochote anachotamani, hata hivyo Mungu wa kweli hamruhusu kula kutokana nacho, bali mtu aliye mgeni tu anaweza kula. Hilo ni ubatili na ni ugonjwa mbaya. 3 Mwanamume akizaa mara mia moja, na aishi miaka mingi, mpaka siku za maisha yake ziwe nyingi, lakini nafsi yake haijatosheka na mambo mazuri na hata kaburi halijawa lake, lazima niseme kwamba mtu aliyezaliwa akiwa mfu ni bora kuliko huyo. 4 Kwa maana huyu amekuja bure naye huenda gizani, nalo jina lake litafunikwa kwa giza. 5 Hata jua lenyewe hakuliona, wala hakulijua. Huyu ana pumziko kuliko yule wa kwanza. 6 Hata ikiwa ameishi miaka elfu moja mara mbili na bado hajaona yaliyo mema, je, kila mtu haendi mahali pamoja?
7 Kazi yote iliyo ngumu ya wanadamu hufanywa kwa ajili ya kinywa chao, lakini hata nafsi yao haishibi. 8 Kwa maana mtu mwenye hekima anapata faida gani kuliko mjinga? Mtu anayeteseka anapata nini kwa sababu ya kujua jinsi ya kutembea machoni pa watu walio hai? 9 Ni afadhali kuona kwa macho kuliko kutembea huku na huku kwa nafsi. Hilo pia ni ubatili na kufuatilia upepo.
10 Chochote ambacho kimekuja kuwako, jina lake tayari limetangazwa, na imejulikana mwanadamu ni nini; naye hawezi kujitetea mbele ya mtu aliye na nguvu kuliko yeye.
11 Kwa sababu kuna mambo mengi yanayosababisha ubatili mwingi, mwanadamu ana faida gani? 12 Kwa maana ni nani anayejua mwanadamu anapata mema gani maishani kwa hesabu ya siku za maisha yake ya ubatili, anapozitumia kama kivuli? Kwa maana ni nani anayeweza kumwambia mwanadamu litakalotokea baada yake chini ya jua?
Huu ujumbe unawakilisha hisia za jamii kwa ujumla.
ReplyDeleteHongera sana dada Yasinta.
Imetulia sana hivi huwa unakopi sehemu au unatunga kutoka kichwani?
ReplyDeleteok jpili njema wasomaji.
Take care!!!
Shukrani kwa wote kwa kuungana nami hapa kibarazani...wote mnapendwa:-)
ReplyDelete