Wednesday, September 7, 2011

Made in Mbinga: Kijana wa Kitanzania mwenye elimu ya darasa la saba afanya uvumbuzi, atengeneza magari manne kwa kutumia vipuri vya pikipiki na vyuma

Katika pitapita nimekutana na habari hii ya kufurahisha na nikashindwa kuiacha nimeipata hapa

5 comments:

  1. kweli kijana anaweza na akiwezeshwa zaidi atafanya makubwa!!!!Made in Mbinga!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Enzi zile nilipokuwa Bongo nilisikia aliwahi kutokea kijana mwenye kutengeneza redio ya kwake binafsi. "Walitaka kumkamatia ujasusi kutokana na kwamba matangazo yake yaligongana na matangazo ya Radio Tanzania Dar es-Salaam kimawingu, lakini Nyerere akamtetea alipoona ni mtoto mdogo aliyeyafanya yote hayo bila kukusudia".



    Kama ni ukweli, mtoto huyo aliishia wapi? Na kijana huyu wa magari yake naye ataishia wapi? SI WOTE WATAIBIWA NA NCHI ZA ULAYA ILI WAENDELEZE TEKNOLOJIA ZA WAZUNGU WAKATI SISI WAAFRIKA, WENYE KIPAJI KIKUBWA KULIKO KILE CHA MZUNGU KIAKILI, TUNABAKI TUNAZUBAA TENA NAKUWA OMBAOMBA WA DUNIA KAMA KAWAIDA?

    ReplyDelete
  3. Wadau tuachane na siasa kwenye vibaraza vya taaluma.Kila mdau anayo nafasi kutoa usaidizi ufaao.Hatua ya awali ni ubunifu huu kutibitishwa na mamlaka za uhandisi wa mitambo na kusajiliwa katika mamlaka husika.Baadae usajili huu atafutwe mwekezaji ili aingie ubia na mbunifu huyu na uzalishaji wa bidhaa uendelee kulingana na viwango vya kimataifa.Mbunifu awasiliane rasmi na mkuu wake wa wilaya ili amsaidie kuonana na waziri wa viwanda na biashara na mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji.
    Hongera sana kwa made in Tanzania.
    S.L.B Mbinga Ruvuma Tanzania.
    -------------------
    R.Njau

    ReplyDelete
  4. @Anonymous

    Sidhani siasa utaweza kuikwepa, Ndugu Yangu, upende usipopenda, na hapo nikiwa nakunukuu:

    "...tuachane na siasa kwenye vibaraza vya taaluma...."


    Gari na teknolojia ya Mwafrika Barani Afrika lazima tu vitachangia katika kufufua uchumi wetu na hivyo kuimarisha hali ya kisiasa nchini zetu kotekote Barani.


    Vilevile nimecheki kidogo kamusi ya mtandaoni kuhusu neno "taaluma" na nikaambiwa kwa Kiingera ni "profession".

    Kwani kwa maoni yako unafikiri "siasa" ni "probation"?

    ReplyDelete