Tuesday, September 20, 2011

KUMBUKUMBU YA MAREHEMU BIBI YETU VALERIANA NGONYANI!!!

ILIKUWA MARA YANGU YA MWISHO

KUONANA NA BIBI 2005 MWEZI WA NNE

Leo ni tarehe 20/9 ni miaka mitano na miezi minne imepita tangu bibi yetu mpendwa Valeriana Ngonyani atutoke.Alifariki 20/5/2005 katika hospitali ya Liuli. Sisi wajukuu wako wote, watoto wako ndugu na marafiki wote wanakukumbuka daima. Bibi Valeriana ni huyo aliyejifunika kitenge, katikati nadhani mnajua au basi ni mimi na mwishoni ni mama yangu mdogo, mdogo wa mama. TUTAKUKUMBUKA DAIMA KWA NJIA YA SALA ZETU. USTAREHE KWA AMANI AMINA.

8 comments:

  1. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe pole kwani wengi wetu hatuna bibi kama wewe na kama mimi nilikuwa kipenzi cha bibi mzaa baba kwani jina langu ndiyo lile la babu yangu hivyo alikuwa na nipends ksms mume mtarajiwa wake ila nina imani nitakutana nae siku ya mwisho
    Amen
    Che Jiah

    ReplyDelete
  2. Kila lakheri nyingi huko uliko mbinguni Bibi, na Mwenyezi Mungu azidi kukupa pumziko la milele na lenye raha siku zote, amina!

    ReplyDelete
  3. "KIFO NI ADUI MKUBWA WA MAISHA YA BINADAMU"



    ---------------
    R.Njau

    ReplyDelete
  4. Mungu amrehemu huko aliko,tumuombee apumzike kwa amani

    Kila la kheri.

    ReplyDelete
  5. Napenda kuchukua nafasi hii na kuwashukuruni wote kwa kuwa nami katika siku hii ya kumbukumbu ya bibi yetu mpendwa Valeriana Ngonyani. Mwenyezi Mungu na azidi kuwapa moyo wa upendo. Tupo wote Daima. Na upendo utawale mioyoni mwenu.

    ReplyDelete