LEO NI KUPE KILE KISA CHA RAFIKI YANGU AITWAE FULKO KOMBA NA WATANI WAKE AKINA NJAIDI NA MASASI HAWA KAMA MAJINA YAO WOTE NI WATOKA KUSINI MWA TANZANIA MASASI NA RUVUMA HAWA NI WATANI WA JADI HALISI,.BASI SIKU MOJA HUKO ZAMCARGO KURASINI SASA MJI HUU UMEVUNJWA NA KUPISHA MRADI WA UPANUZI WA BANDARI. ILIKUWA SIKUKUU YA KRISMASI, KWA KAWAIDA HAWA AKINA KOMBA WALIKUWA NA KIKUNDI CHAO CHA NGOMA YA HUKO NYUMBANI SONGEA. HAWA WANATOKA PALE NJIA PANDA YA SONGEA NA PERAMIO KAMA UNAKWENDA CHIPOLE. JINA LIMENITOKA KIDOGO NIKIKUMBUKA NITAKUTAJIA .,BASI KILA MWISHO WA MWAKA AU KRISMASI HUWA WANAPIGA NGOMA ZAO NA WANAKESHA .BASI ...BWANA ..MWAKA HUO MKESHA ULIKUWA NA MVUA NYINGI KIASI KUWA MPAKA SAA TISA USIKU
WATU WALIKUWA WAMELALA, ILA KWA HAWA JAMAA WA MASASI KULIKUWA NA KIGROSARI NA KULE KURASINI KULIKUWA NA SIFA YA KUUZA MAFUTA YA MAGENDO YAANI PETROLI AU HATA MAFUTA YOYOTE HATA YA KULA ILIKUWA NI DILI. VIJANA WA KILEO NDIYI LUGHA YAO, BASI HAPO KWA MASASI WALIKUWA WALEVI WOTE NDIYO KISEBULE CHAO HATA USIKU WE GONGA TU NATAKA BIA UNAFUNGULIWA.
NA UNAPEWA UNACHOTAKA KWANI SIKU DILI IKIKUBALI BASI HAPATOSHI. KWAHIYO SIKU HIYO WATU WALIKUNYWA MPAKA MANANE. NA UJUWAVYO MLEVI ANAPOKUWA AMEPATA MARA ATOKE KWENDA HUKO MARA KULE BASI NJAIDI ALIKWENDA KUFUATA SIGARA PALE ZILIISHA , ALIPOTOKA MBELE KIDOGO ALIKUTA MNAZI, NA KUKUTA KINYAMA KOMBA ,, KINAPUMUA KWA MBALI ... KIMELALA ..BASI ALIRUDI NDANI NA KUWAAMBIA KUWA JAMANIEEE KOMBA KALALA PALE ,KOMBAAA,,,, NDIYO KOMBAA ANAUMWA AU ,,,JAMAA AKAJIBU SIJUWIII...TWENDE .. WAKAENDA KUMWONA WAKAKUTA KALE KANYAMA ..BASI MMOJA WAPO AKAWAAMBIA WALE WENZAKE KWAVILE HUYO KOMBA NA NDUGU ZAKE WAPO KARIBU BASI TWENDE ZETU TUKAWAAMSHE WAMPATIE MSAADA ,AU SIYO JAMANI.EEE WAKA JIBU ,,SAWAAA BASI WOTE WALE VIJANA WA MASASI WAYAO WAKAENDA KWA WANGONI ,,,NGOO NGOOO HODI ...MLANGO,,, NANI WEE ... AKASEMA ALOO KOMBA, FUNGU ...NDUGU YENU KOMBA KALALA PALE HAJIWEZI ,,,AKAULIZA KOMBAAA... NDIYO
YUPO WAPI ,,,PALE KWENYE MNAZI ,,,,,YEYE BILA KUHOJI ZAIDI AKAENDA KUMWAMSHA FULKO, NA NDUGU YAKE BOSCO WAO NAE AKAMFUATA THEO ILA KWAKUWA ENEO LILE WALIKUWA FAMILIA ILE WANAKAA PAMOJA WAKASEMA BASI TUKAMWAMSHE MUJESHI ,,KAKA YAO ,HUYU ALIKUWA MWANAJESHI ,BASI WOTE TIMU MZIMA WALIONGOZANA NA WALE VIJANA MPAKA PALE ALIPOLALA KOMBA ,..YUPO WAPI???? ...SWALI .. HUYU HAPA,,,, WAKAONYESHWA KOMBA MNYAMA, NDIYO HUYU?? ..NDIYO ,,,,,,HUYU NDIYO ,,,,,,,,,,,,
KWANI HUYU ANAITWA NANI??? WOTE WAKAJIBU KOMBA .........BASI NDIYO HUYO NDUGU YENU ,,,,,,,,,,WALE WAYAO WAKAONDOKA NA KUIACHA TIMU MZIMA YA WANGONI NA MAJINA YAO YA WANYAMA NA NDUGU YAO KOMBA MLEVI WA TEMBO,...... KUMBE KOMBA ANAKAWAIDA YA KUPANDA JUU YA MMNAZI NA KULINYWA TEMBO LA MNAZI HIVYO NAE SIKU ILE ALIBAHATIKA KUPATA POMBE YA MNAZI AKASHEREHEKEA VIZURI SIKUKUU YA MWAKA MPYA NA KUWAFANYA NDUGU ZAKE AKINA KOMBA WAACHE VITANDA VYAO NA KWENDA KUMWANGALIA NA KWAMAWAZO YA WANGONI KWANI WALIPOSIKIA KOMBA KALA WALIJUA KUWA NDUGU YAO KOMBA
AMEPIGWA BILA KUCHUNGUZA NI KOMBA GANI ??? HUYO ,
HIVYO NDICHO KISA CHA KOMBA NA AKINA KOMBA
NA IPO SIKU ITATOKEA KISA KAMA HICHO CHA NYANI NA AKINA NGONYANI................KWANI HAKUNA MAJINA YOTE YALIISHA ,,,,,,,,,,,, KOMBA, NYOKA , NDANDALA, MAPUNDA.,,,N.K POLENI WATANI ZANGU WA PALE LIPOKELA KITAI , NTYAN"GIMBOLE, LIPUMBA MATILI, HALALI PALE KIGONSERA , NGOMBO AU MBAMBABAY POLE KILOSA AKINA NCHIMBI ,MBUNDA KULE UMATENGONI
ASANTE MIMI MYAO SIYO MUYAO MAANA KWETU PALE NI MUHOGO UNAITWA MAYAO YAKIWA MENGI
HUU NI UTANI WA MAKABILA MAJINA NILIYO TUMIA NI YA KWELI YAWATANI ZANGU ILA HAIKUWA HIVYO NA WALE WA MASASI NI BINAMU ZANGU KWELI WANAITWA MAJINA HAYO.
-------------------------------------------------------------------------------------------------
KISA HIKI NIMETUMIWA NA MSOMAJI WA MAISHA NA MAFANIKIO KWA JINA LA ISSACK CHE JIAH KWA VILE ALIONA JINA LANGU NI NGONYANI AKAPENDA "KUNITANIA" NAMI HUWA SIPENDI KUFAIDI MAMBO KAMA HAYA PEKE YANGU NIKAONA NIWEKE HAPA ILI NANYI WENZANGU MFAIDI.
JASIRI HAACHI ASILI NA MUACHA ASILI NI HASIDI NA HANA AKILI.
ReplyDeleteR.Njawa
Ngonyani,mbawala,mapunda, sasa sijuwai nahili la kwangu mbogo nalo limetoka wapi? safisan haya ndo mambo ya utani wa makabila,mngoni nimtani wangu,mzaramo pia ni mtaniwangu,msambaa nimtaniwangu nk wakati wa misiba ndo utajuwa uzuri na ubaya wa utani wa makabila. asante dada ngo- nyani.Kaka S.
ReplyDeleteR.Njwa! Nimeupenda usemi wako. Ahsante sana
ReplyDeleteKaka S..au Mbogo ..unaujua ule msomo usemao kazuka mbogo..Kwa hiyo wewe nawe una jina la mnyama mbogo au kwa urahisi zaidi ni NYATI. Ambaye ni mkali kwelikweli ungekuwa mwanamke ningekuita Na-nyati..:-)
Kumbe komba yupo hivi macho yake? Yani mtu akikwambia macho ka Komba una haki ya kukasirika.
ReplyDeleteCHE JIAH
ReplyDeleteNasema kweli majina mengine kwakweli sijuwi yalikujaje hivi kweli wangoni mmetoka Afrika kusini hamkuwa na majina mengine isipokuwa ni yale mliyokuwa mnatafuna nyama yake kama babu yake kapulya alizidi katafuna nyani wote toa bondeni mpaka songea akajipa NGONYANI si bora mputa mpambalyoto,songea,hayo ndo majina ila haya ya wanyama duuu .Lakini mimi historia aliyoniachia babu yangu ni kuwa hawa akina komba ,mbawala,n.k isipokuwa ngonyani tuu .hawa walikuwa washukiwa wa wake za watu yaani waliwatorosha kule south hivyo ili mahakama ya icc isiwatafute ilibidi baada ya kutia nanga pale songea ,wabadilishe majina yao ,
USIKASIRIKE KAPULYA NGONYANI HAUSIKI.
NI MIMI MMAKONDE CHE JIAH
Niwasumbufu
ReplyDelete