Thursday, June 9, 2011

Swali la leo:- CHANZO CHA UKOO NI NINI?

Swali langu la leo nimeenda hadi Upareni na kurudi...Nikimaanisha litawalenga hasa ndugu zetu WAPARE. Ila nitaanza na mifano miwili ambayo ni zoefu kwangu:-
Nilipokuwa msichana mdogo nakumbuka niliwauliza wazazi wangu kwa nini twaitwa NGONYANI na ni nana alianzisha na pia kwa nini karibu majina mengi ni ya wanyama? Sikumbuki kama nilipata jibu.
Baadaye nikawa msichana mkubwa na nikaanza maisha na nikaanzia maisha yangu kuishi na WABENA. Kwa kweli walibifanya UDADISI/UKAPULYA wangu uzidi. Kwa vile wao U-KOO wao unaanza na M, mfano:- Mwageni, Mgaya, Mbilinyi, Mgina nk.
Lakini hata hivi si WABENA tu ambao wanaanza na M. Na hili ndilo ambalo lilikuwa kiini cha swali langu zaidi ndugu zetu WAPARE... Yaani koo kama za KIPARE:- Kwanini zinaanza na M?. Mfano MSUYA, MMBAGA, MZIRAYI, MFINANGA, MSHANA,MCHOMVU ......NK. Nina uhakika hapa nitasaidiwa. TUKUTANE TENA WAKATI MWINGINE:-

7 comments:

  1. Dada yetu kweli wewe ni-kapulya kweli kweli..dada Mdadisi, hata mimi nilikuwa natafakari hilo kwanini koo hizi, hususani za kipare zianze na herufi M, kwa kuendeleza majina hayo ya koo za kipare, kuna. MFINANGA, MZIRAYI MCHOMVU, MSUYA, MMBAGA, MSANGI, MGONJA, MSHANA, MVUNGI,MLACHA(KITURURU) NK...nikawaza sana mpaka nikapa nakala moja ya jamaa alijitahidi kuandika historia fupi ya Wapare, isome hapa kwenye face book:
    http://ja-jp.facebook.com/topic.php?uid=19111965542&topic=17249

    ReplyDelete
  2. em-3! Ahsante kwa kutochoka kupita hapa na kuacha elimu yako pia..nitapita huko ulikoshauri...Pia ahsante sana kwa hapo ndani ya mabano(KITURURU) nilikuwa nataka kujua pia maana kama sikosei niliwahi kusikia kaka KITURURU NI MPARE je? iweje yeye aitwa KITURURU SIO MSHANA?

    ReplyDelete
  3. Mie nikifuatilia ni MZAVA upande wa Babu mzaa baba ,na ni Mmbaga upande wa BIBI mzaa Baba!


    Sababu :
    Jibu sina mpaka nimuulize Baba!

    Na sijawahi kujiuliza swali hilo!

    ReplyDelete
  4. Mie Mchaga Bwana, ya Wapare nitayaweza wapi? Labda kina Kitururu na Ramadhani Msangi wanaweza kukujibu...
    Ila mama yangu ni Mpare na nimejaribu kumuuliza hapa lakini hakuwa na jibu la moja kwa moja badala yake kaanza na hadithi ndeeeeefu, mpaka nikachoka kumsikiliza....LOL.
    Yeye jina la ukoo wao ni Mgonja....
    Hata hivyo nitaenda kwa Bibi Koero mwenyewe hivi karibuni, yeye najua atanipa ukweli wa jambo hilo....

    @YASINTA.....
    Na wewe hebu tueleze kisa cha majina ya koo za Wangoni kuitwa majina ya wanyama....?
    Ngoja nikutajie machache hapa chini..
    -Nyani
    -Kiti Moto (I mean Nguruwe)
    -Fungo
    -Tembo
    -Fisi
    -Nyati
    -Chui
    -Simba
    -Komba
    -Punda
    -Twiga
    -Kolongo
    -Kifaru
    -Ng'ombe
    -Sungura
    -Nyoka
    -Kicheche
    -Swala
    -Chura
    -Mjusi
    -Kenge
    -Samaki
    -Mamba.......na mengineyo mengi
    Je sababu ni nini?

    ReplyDelete
  5. @Koero Mkundi

    Zamani enzi zangu za maisha TZ (1985-1994) niliwahi'sikia hawa Wapare na Wachagga ni ndugu. Kama ni ukweli, itakuwaje (NAKUTANIA TU!) usiyajue ya Watani zako?


    Vilevile, kama ni kweli 'Mchagga na Mpare wanaye Babu mmoja upande waBaba yao', basi watakuwa waliachana na kila mtu kujenga nyumba na mila zake kutokana na Wapare kuwoana na Wabantu/ WaDzonga/Watonga/WaZion/WaAzania.


    Nahisi hapo, kwa upande wa mama zao wale waKitonga au Kibantu, ndipo Wapare walipookota hiyo “M-” kama kitangulio (PREFIX) cha ukoo! Jambo hilo (la "M-") ni kawaida sana kwa Wabantu/Watonga kotekote.


    Jamaani nanyi wapendwa wasomaji wengine, Mswahili Barani ndio ni mmoja tu, lakini chimbuko lake aina mbili kubwa!

    Moja yake ni kundi laWabantu; na Mbantu unamtambua (LITMUS TEST) kwa lugha yake anavyotafsiri Kiingerea neno la "PEOPLE". Ikiwepo katika tafsiri yake "m/n" na "t/d" (na mataamshi kama hayo),basi hilo kabila litakuwa ni moja katika Wabantu.


    Mpendwa Dada Koero (nawe Mtanimtu, Kitururu), kwani "mtu" kwa lugha ya Kipare ni nini? Si "mtu" hivyo hivyo? Au wanataamkaje? "Mdu"?


    Na kama hapo nimepata wala sikukosea, basi ile "M-" katika ukoo waWapare ni kama ukumbusho kwamba "huyu, pamoja labda na kutaja mnyama au kitu kwa ukoo wake, hatuzungumzii mnyama alietajwa au kile kitu tu, bali tunamzungumzia Mtu aliepata sifa za mnyama huyo au kitu hicho fulani!"
    (Mfano, ukoo wa Phiri unatafsiriwa kwa "moto", au "mlima", hata "fisi", yote yakitegemea kabila ambamo huyo Phiri anakoishi kwani Phiri ndio ukoo wazamani kuliko yote Barani Afrika na makabila yote yanakuja baada yaPhiri kuwepo! Lakini ile tafsiri ya "moto" ndio karibu ukweli kuliko zote, labda nieleze kuhusu Phiri kwa undani siku ingine).


    ANYWAY, hiyo ya juu ndio hali halisi katika Wangoni (Xhosa, Zulu, Swazi, Ndebele) wa Afrika kusini.

    Nikupe, Dada Koero, mifano ya baadhi ya majina yao ya ukoo:

    Mlambo= "Mtu Mto"
    Mkhatshwa= "Mtu aliesindikizwa"
    Mkhize= "Mtu mwenye mvua ndogo"
    Mkholo= "Mtu mwenye imani"
    Mkhonta= "Mtu anayetoa heshima/ -anayeomba sehemu pakujengea nyumba"
    MaZibuko= "Mtu mwenye Vivuko"
    Masuku= "Mtu mwenye Siku nyingi"
    Mavimbela= "Mtu mwenye Kutia vizuizi"
    Matsebula= "Mtu mwenye kuloga"


    Hapo juu ni ukoo wa Wangoni hapa Bondeni; lakini hata ukoo wa Wasotho (Pedi, Tswana, South Sotho) nao ni Wabantu, yaani wanatumia hio "M", ila tu wao mara nyini huongeza hivi "Mo-". "Mo-" hiyo inatokana na "Motho"='MTu'= "A PERSON" kwa kuwa ni WabanTu.

    Kwa hiyo:
    Mokwena= "Motho oa kwena"= "mtu kama Mamba"
    Moloi= "Mtu anaeloga"
    Motsamai= "Mtu anae tanga tanga"
    Malema= "Mtu anae lima"





    @ Dada Yasinta


    Kila nikikuchukia na gundua hapana: NAKUPENDA! Kwa mfano, swali lako ni zito sana. Kwa hiyo nakushukuru kwa kunisamehe kwa kuwa mrefu kwa mapana hapa, yote kwa madhumuni ya kukujibu swali lako zuri!

    ...Na, sijamaliza...

    "Ninogela kuandika gamahele", ila tu basi NIPE KWANZA RUHUSA!!!

    ReplyDelete
  6. Ahsanteni wote kwa majibu yenu katika historia hii...Koero hujaona kuwa nimesema nilipokuwa mdogo niliwauliza wazazi wangu na nakumbuka sikupata jibu...ndo maana nikaona labda Wapare wana jibu..lakini nipe muda nitauliza ...
    Kaka mkubwa Phiri we usiwe na Wasiwasi endelea tu ni raha sana kujua....

    ReplyDelete
  7. Very Interesting sis yasinta chemsha bongo

    ReplyDelete