Picha hii imenikumbusha enzi zile miaka arobaini na saba familia nzima inajumuika pamoja na kushika chakula iwe cha asubuhi, mchana au jioni. Hakika hii ilikuwa safi sana. Ila hapa naona watatu wanatumia vijiko na mmoja anatumia mkono... Halafu unajua kitu kimoja ukishazoea kula chakula mkiwa wengi huwa kinanoga sana kuliko kula peke yako...je wewe nawe umekumbuka nin?
IJUMAA NJEMA NA UKIPATA NAFASI KULA NA JIRANI YAKO AU RAFIKI.
hii ilikua fursa nzuri sana ambayo mpaka leo ni moja ya sababu iliyotupa watz umoja upendo na mshikamano usioweza kuvunjwa na mtu yeyote,hakuna kitu kizuri kama kula pamoja kama hivi.kwanza inakusaidia unakua na appetite ama hata kama huna itabidi ulazimishe maana wenzio watakuachia sahani tupu.
ReplyDeletena hasa ni nzuri sana kwa watoto kujifunza heshima na adabu saa ya kula maana akizembea anakuta wenzie wamemmalizia na hakuna chakula kingine
kumbukumbu nzuri sana hii.
Kaka Isaack! Ulichosema ni kweli kabisa. Kwani kuna kitu nimegundua ya kwamba niwapo peke yangu huwa sili chakula ile eti kinanoga lakini nikaapo na wengiii weeee mpaka inabidi sufuria ya ugali ubandikwe tena na matembele yakachumwe... Halafu hili pia ni kama zoezi fulani vile.... Hivi kwa nini ulapo na mkono chakula kinanoga zaidi kuliko na kijiko/kisu na umma?
ReplyDeleteUnaitwa `mkao wa kula'...safi sana, kweli huu ni moja ya utamaduni wetu..mnaweza kukaa kama familia au kujumuika kwenye sherehe na shughuli mbalimbali...
ReplyDeleteMila hii nzuri hata hivyo inakufa. Sasa watu wako bize na eti ni vigumu kwa familia nzima kukaa na kula pamoja. Sasa mtu anachukua kisahani chake na kwenda kukaa mbele ya TV peke yake ili shoo yake aipendayo isimpite.
ReplyDeleteMtu ukienda kijijini, ng'ombe akachinjwa, familia nzima na majirani mkakusanyika na kula pamoja - angalau unaweza kuuhisi ule umoja na upendo tuliokuwa nao miaka michache tu iliyopita.
Kwingineko, mila hii sikuipenda hasa kwa watoto wadogo. Kule kwetu usukumani, wewe ukiwa mtoto basi ni wajibu wako wa kurudia kitoweo jikoni. Tatizo ni kwamba ile tu unaweka sahani ya kitoweo chini unakuta kwamba nyama zote zimeshachukuliwa. Na kabla hujakaa sawa, kundi jingine la wanaume nalo linataka liongezewe mboga. Basi unanyanyuka tena kwenda kuleta kitoweo jikoni na mambo ni yale yale. Ukizubaa unaweza ukaishia mchuzi tu na usionje nyama. Tulikuwa tunaambiwa kwamba eti huo ulikuwa ndiyo uanaume na kwa mvulana wa miaka sita au saba nadhani hii haikuwa sahihi kwani wakati huu mtoto ndiyo anahitaji protini kwa wingi.
Kumbukumbu nzuri Da Yasinta.
Kaka Matondo hapo umenikumbusha tena hasa hapo pa kutumwa kuongeza kitoweo na wewe mwenyewe usiambulie kitu. Nakumbuka nilipokuwa mdogo kulikuwa na kamtindo kwamba angalao kila mtoto agawiwe kipande cha nyama ili kuepuka huko mtindo wa kupunzwa. Kama ulivyosema ni kweli kabisa katika umri huo mtoto anahitaji sana protini. ... Nasikitika kusikia utamaduni huu unaelekea kupotea ...Sijui haiwezekanai kupanga au KUAMUA HAKUNA KUTAZAMA TV WAKATI WA CHAKULA???
ReplyDeleteminaona kama siyo kweli kula pamoja inadumisha upendo ,nk sanasan a inawezekana wakati huo kulikuwa na uhaba wa sahani za kutosha? ndo maana watu wakala pamoja. anyway niuchokozi tu mimi mwenyewe nimepitia hilo zoezi kuna utamu wake,hasa watoto wanapoonekana kuwa na spidi kali ya nyama,wazee watatumia kila mbinu usifanikiwe kula nyama.sisi tulikuwa namchezo siku ya nyama lazima awekwe mtu maalumu wa kuzima kibatali,kikija kuwashwa nyama zote kwisha,lakini wakubwa kwa hasira walitembeza makonzi kama kujipoza. Da Yasinta ila hao jamaa kama wana tumia vijiko vile au macho yangu. Kaka S.
ReplyDeleteNyeehh! hapo wamesahau kombe kubwa la bati, lenye maji ya kunywa wote mnashea pia. hao vijiko hapo si pake ni mwendo wa mkono tuu,kama wewe unacheza mbali na nyumbani,Asiyekuwepo na lake halipo,ugali wa kengele huo!.Binti wa Ngonyani leo umetuweza dada!!!!!
ReplyDelete@Da Mija vipi yule aliyekuwa anakanyaga sahani/sinia ya chakula? hahahahhahaha.
Hii ilikuwa nzuri. Tatizo lilikuwa KABLA na BAADA ya mkao huu. Ule ustaarabu wa watu kumi "kukalawia" beseni moja la maji.
ReplyDeleteInanifanya niwaze kama mtu wa mwisho alikuwa ananawa ama anajichafua zaidi?
Asante dear. Nawe na familia muwe na muda mwema
Kwa bahati mbaya sikukulia katika familia ambayo tulikuwa tunakula mkao huu. Na kwenye sherehe nilikuwa nakoma maana kabla hata sija finyanga vizuri tonge nastukia nyama zimeisha!
ReplyDelete:-)
Ila Hoja ya Mzee wa CHANGAMOTO nimeikubali aisee kwa kuwa ilikuwa inanikaa akilini kila nikitokea sehemu ambao kung'ata nguna inabidi ukae mkao huuu!
ReplyDeletehii vilevile inasaidia kwa watoto wasiopenda kula waite watotowenzake walepamoja kulekunyanganyana kunamfanya mtoto afanye bidii ya kula.Yasinta kula kwamkono ndio safi zaidi kwamaana kuna utaalamu yakuwa ukiweka mkono kwenye mchuzi kesho yake mboga inachacha,wataalamu wanasema kunaaina fulani ya vijidudu vinafanya chakula kichache au kuua baadhi ya vimelea ambavyo vipo kwenye chakula
ReplyDeleteMimi imenikumbusha juzi nilikuwa nyumbani nikawa nakula na familia yetu nilijisikia vizuri sana kwani inanifanya nipate hamu ya kula zaidi kuliko nikiwa peke yangu nashindwa kula vizuri. Kwa hiyi nimefurahi sana kuona picha hii.
ReplyDeleteHabari za siku;
ReplyDeletepicha hiyo ya kula pamoja inanikumbusha enzi hizo na mafundisho yaliyomo ndani yake na kile kinachotokea siku hizi katika jamii yetu.
Somo na fundisho lililopo la kula pamoja ni kujenga zana ya sisi kuwa wamoja na kugana kile kilichopo kwa faida ya wote na kuwa na uvumilivu na kuwajali au kuwakumbuka wengine.
Babu na bibi zetu walikuwa wanafalsafa ya kudumisha familia na jamii kwa umoja na mshimkamano kinyume na siku hizi ndiyo maana hata katika maisha ya siku hizi katika sehemu mbalimbali mashuleni vyuoni na hata makazini katika Tanzania yetu kuna migomo na kuvurugana kwingi kutokana na kukosekana msingi wa kuwa wamoja kuazni angazi ya familia
kila la kheri kazi njema
4 “Sikiliza, Ee Israeli: Yehova Mungu wetu ni Yehova mmoja. 5 Nawe lazima umpende Yehova Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote na kwa nguvu zako zote. 6 Na maneno haya ninayokuamuru leo lazima yawe moyoni mwako; 7 nawe uyakazie kwa mwana wako na kuyasema unapoketi katika nyumba yako na unapotembea barabarani na unapolala na unapoamka. 8 Nawe uyafunge kama ishara kwenye mkono wako, na yawe kama utepe wa kipaji katikati ya macho yako; 9 nawe uyaandike juu ya miimo ya mlango wa nyumba yako na juu ya malango yako.[Kumbukumbu la Torati 6:4-9]
ReplyDelete