Monday, May 9, 2011

TOFAUTI ZETU:MWANA​MKE NA MWANAUME

Wiki iliyopita niliweka mada hii hapa na baadaye nikakumbuka kuwa nina kitabu cha Maisha Na Mafanikio kilichoandikwa na Marehemu Munga Tehenan. Ambacho nilikuwa nimekisoma nikaona nikipitie tena na nikakuta mambo mazuri ambayo nina uhakika wengi tutafaidika, tutajifunza na pia kujitambua. Nikaona ni bara ninukuu kidogo hapa na pale na hapa chini ni nukuu kutoka kitabu hicho haya karibuni sana kusoma.






"Tofauti za kijinsia zinatokana homoni, homoni za kike humfanya binaadamu kuwa mwanamke na zile za kiume humfanya binaadamu kuwa mwanaume.
MTU ANAJULIKANA KUWA MWANAUME AU MWANAMKE KWA KUTAZAMA SIFA FULANI ZA KIMWILI ambazo ni matokea ya kazi za homoni. Tofauti za kihisi pia matokeo ya homoni.
Kuna tofauti za kijinsia ambazo zinatokana na mapokeo ya kijamii, nyingi huonyesha kuwa mwanamke kama kiumbe dhaifu.
Kuna mambo yanayoweza kutusaidia kujifahamu vizuri kati ya jinsia hizi mbili yaani mwanamke na mwanaume
Masuala hayo ya tofauti kati ya mwanamke na mwanaume kwa mtazamo tafauti na kibailojia husaidia kuboresha mahusiano. Tulio wengi hatuzielewi au hata kama tunazielewa lakini huwa hatuzikumbuki na mwishowe hupelekea kuyumba katika uhusiano au kutokea ugiligili(kukatishwa tamaa na kushindwa kufikia matarajio yetu katika uhusiano na kuwa na hasira kwa wenzetu na kudhani kuwa wenzetu wanatakiwa kuwa kama sisi. Huwa tunadhani kuwa wenzetu wanatakiwa watake ambacho sisi tunakitaka na kuhisi ambacho sisi tunahisi.
Huwa tunaamini kuwa kama kweli wenzetu wanatupenda watafanya na kuonyesha mambo fulani kwetu, mambo ambayo sisi tunayafanya au tungeyafanya kuonyesha jinsi tunavyowapenda. Kutokana na kutofaoutiana kwetu hayo huwa hayafikiwi na huwa tunavunjika moyo.
Mara nyingi wanaume ,wanawake kimakosa tunatarajia wenzetu wafikiri, wawasiliane, wajibu na kuhisi kama tunavyofanya sisi.
Kutarajia huko kunatokana na kutofahamu au kusahau kwetu kuwa wanawake na wanaume tukotafauti kimaumbile na kihisia. Kwa kutarajia na kushindwa kuyaona matokeo, uhusiano na ndoa zetu zimejaa misuguano na migongano ambayo siyo ya lazima au haina maana.
Hiyo inathibitishwa na kauli zetu za mara kwa mara mfano wanawake huwa wanasema wanaume hawaeleweki na wanaume kusema wanawake wanajua wenyewe tabia zao wala usishindane nao. Katika hali halisi tunashindwa kuukubali ukweli wa hicho tunasema na kumaanisha. Pamoja na kutoa kauli hizi tunashindwa kufahamu tunatofautiana katika nini au kivipi?
Kama kila mmoja wetu atazifahamu tofauti hizi n i zipi migogoro na migongano katika ndoa na uhusiano vitapungua.
Mara nyingi watu kabla hawajaoana au mara baada ya kuaona migogoro na migongano huwa michache kutokana ukamili wa hisia za wahusika ambao penzi bado mbichi, hili ni suala la kibailojia. Tunapokaa na kitu kwa muda mrefu hujitokeza hali inayoitwa uchovu wa hisia au ukinaifu kwenye mapenzi nako ni hivyohivyo. Kuchoka kwa hisia hutofautiana kati na mtu na mtu wengine huchukua muda mfupi na wengine huchukua muda mrefu. KUTOKANA NA KUCHOKA KWA HISIA hutokea kila mmoja kutarajia mwenzake afikiri na kutenda kama yeye. Ndipo tofauti kati ya mwanamke na mwanaume hujitokeza waziwazi na si hatuzioni isipokuwa tunahisi athari zake. Wengi huwa tunadhani kuwa penzi limekwisha, bali huwa tunashindwa kufahamu kuwa sisi ni tofauti. Kwa kuwa tunatarajia kuona wenzetu wakifanya kama sisi na kuhisi kama sisi na hawafanyi hivyo huvunjika moyo na kudhani kuwa hatupendwi tena , na kwa kutokujua hilo migogoro huanza na kuifanya kuwa mikubwa,kila mmoja humwambia mwenzake hunielewi wakati ukweli kuwa wote hawaelewani kwa kuwa hakuna anayeelewa kuwa yu tofauti na mwenzake.
Tofauti za kimaumbile kati ya mwanamke na mwanaume ziko nyingi lakini kuna zile za msingi ambazo huwa tunakumbana nazo kila siku katika uhusiano wetu na wenzetu. Kwa kuzifahamu chache tunaweza kabisa kuzikabili na linapotokea tatizo tutakuwa tayari na ufunguo wa kufungulia mlango wa kufahamu wengine wakoje na sisi tukoje kimaumbile.

1. Wanaume na kufundishwa.
Wanaume ni wababe na hivyo mara nyingi hujiona kuwa ni mashujaa na wala hawataki kuona wameshindwa na kutokana na hali hiyo huwa hawapendi kuelekezwa hasa na wanawake hata kama hawako katika husiano. Mfano katika suala la kutoa ushauri wa kujenga uhusiano na maisha ya baadae mwanamke anaweza kwa nia njema kumwambia mwanaume fedha unazopata tutumie sehemu yake kuweka akiba ili tununue kiwanja halafu tutafute fedha za kujengea nyumba. MWANAUME BADALA YA KUSHUKURU KWA USHAURI ATAJIBU UNADHANI NI RAHISI KIASI HICHO INGEKUWA NI WEWE UNAYETAFUTA FEDHA HIZI WALA USINGESEMA HIVYO. Nyie wanawake ndiyo matatizo. Na kufuatia na maneno mengine mengi ya ajabuajabu hadi mwanamke akanywea. Mwanamke hataona kosa lake na kudhani kuwa mume wake hampendi au upendo umekwisha, hamsikilizi, wala kumjali ni dikteta na haambiliki. Mwanamke ameshindwa kujua kuwa yeye na mwanamke ni tofauti na kuwa mwanaume hataki kufundishwa kama moto au mwanafunzi. Mwanaume anaposhauliwa bila kuomba husikia katika masikio yake kama anaambiwa kuwa hayuko kamili na hajimudu an hivyo analaumiwa.


2.Wanawake na kusikilizwa.
Wanawake wanaongozwa na hisia(Ushauri) na wala siyo majibu au suluhu.
Kwa mfano huwa inatokea mwanamke akamuuleza mume wake kuhusiana na tatizo linalomkabili la kuwa na shughuli nyingi za nyumbani na jinsi anavyochoka hapo huwa anaomba ushauri na siyo kutaka jibu au suluhisho. Kwa kuwa wanaume wamezoea kutoa majibu au suluhisho anakimbilia kutoa jibu au kutoa ufumbuzi wa tataizo . Mfano atasema kwanini usitafute msaidizi na kupunguza kazi kwa mwanaume kauli hii inatoka kwa dhati na kuamini kuwa anafanya kile mke wake anachotaka, wakati kwa mwanamke inakuwa tofauti na hivyo mwanamke kutokumuelewa mume wake,kwa kuwa mwanamke anataka kusikilizwa na siyo kupewa ufumbuzi. Kwa kumwambia oo pole sana kweli umechoka ikafuatia na kauli ya kutafuta ufumbuzi. Kwa kumwambia pole sana na kumsikiliza hufuatia na kauli kutoka kwa mwanamke we acha tu natamani hata kutafuta msaidizi wa kunisaidia kazi za ndani.
2.Wanaume na sifa
Mwanaume siku zote anauawa na sifa huwa anataka kuona mwanamke amuone kwamba yeye ndiye mwanaume bora kabisa na asiyeshindwa na jambo. Adui yake namba moja ni kukosolewa na wala siyo kwamba mwanamke anapokosolewa anafurahi hapana lakini hapati shida kama mwanaume. Mwanamke anapomkosoa mwanaume huwa anamdunga sindano ya sumu anamuuwa kisaikolojia. Na inaaminika katika ndoa amabyo mwanaume anakosolewa sana mwanaume katika ndoa hiyo huweza kupatwa na tatizo la kukosa nguvu za kushiriki tendo l a ndoa. Mwanaume anapokosolewa na mke wake huumia sana. Kuumia huko ambako hutokea katika mawazo ya kawaida na yale ya kina humfanya mwanaume kuona kama amenyanganywa uanaume wake. Maumivu haya huendelea mpaka kitandani.
Kwa mwanamke huwa tofauti kwa kuwa mwanamke amekuwa anakoselewa na kutupiwa lawama tangu enzi za kale kukoselewa kwake hakumpi tabu.
Kwa bahati mbaya wanawake hawalijui hilo na anatarajia mwanaume kuwa kama yeye na anapomkosoa anadhani na kuamini kuwa atambadili mwanaume.

3. Mwanamke na kupendwa/mwanaume kupotea
Mwanamke anajua na kuamini kuwa ni mtu wa kupendwa iwe kwa maumbile au kwa sababu za kimazoea ya mfumo dume.

Wanawake wanataka kujua na kuhakikishiwa kuwa wakati wote wanapendwa na kuhakikishiwa katika ndoa kuwa hawatakosea au kukosea na kusababisha upendo kuisha. Wanaweza kuhakikishiwa kwa kauli au kwa vitendo.

Wanaume hawajui jambo hili na huwa hawajali sana kauli zao na vitendo vyao. Na huwa hawajali kuwa karibu na wake zao..
Kauli za kutojali za wanaume kwa wake zao kama mwanamke anaweza kumtamkia mume wake nakupenda mwanaume akajibu najua.
Kwa upande wa pili wa wanaume huwa wanatamani wakati fulani kukaa peke yao hasa pale wanapokua na mambo mengi kichwani hujikuta tu wakitamani kuwa peke yao kwa muda fulani. Hali hii imepewa jina la kuingia pangoni au kisimani. Soma kitabu cha mtaalamu maarufu wa uhusiano Mmarekani John Gray katika kitabu chake maarufu cha Men are From Mars, Women are From Venus.
Inapotokea hali ya mwanaume kuwa pangoni wanawake hudhani kuna jambo wamewafanyia waume zao na kuanza kubabaika na kuamua kuwahoji waume zao n akuwafuatuafuata waume zao. Hali ya mwaume kuwa pangoni huomyeshwa na matendo kama kutaka kukaa pekee yake sebuleni, chumbani, ukumbini.
Kutokana na hali hiyo mwanaume huonekana kama anamkimbia mke wake wakati si kweli.
Tunatakiwa kufahamu kuwa tuna tofauti kati yetu na kukubali ukweli huo kwa kuufanyia kazi ili kupunguza migogoro na migongano kati uhusiano."

6 comments:

  1. Mmmh!

    Ila pia labda tofauti kubwa ya WANAWAKE na WANAUME ni kwa kuwa WANAWAKE ni WANAWAKE na WANAUME ni WANAUME!

    Na katika TOFAUTI tukitafuta visingizio kwanini wote WANAUME na WANAWAKE wana nyonyo tutapata tu na hilo huwa ni kwa kuwa tunatafuta kupata kisingizio kwa nini kwa kawaida nyonyo la mwanaume ni dogo na nyonyo la wamamke ni kubwa!


    Ndio,...
    ... kwa kawaida UKITAFUTA TOFAUTI za vitu vyovyote viwili UTAPATA.:-(


    Ukitafuta tofauti kati ya wanawake wawili utapata tu!

    Ukitafuta tofauti kati ya WANAUME wawili utapata tu!

    Na si hakuna BINADAMU wawili walio sawa kitu ambacho katika mita hata ya nani ni DUME jike au DUME jike bado tofauti tukizitafuta tutapata ni nani DUME JIKE zaidi?


    Na hivi ni kwanini nahisi BINADAMU hutafuta zaidi TOFAUTI zaidi ya USAWA kitu kifanyacho mpaka MZANZIBARI na MTANGANYIKA unaweza hata kuuawa kwa hilo kwa kuwa kuna watakao ona tofauti hata kama MTANGANYIKA na MZANZIBARI wote majinayao ni SAIDI?
    Nawaza tu kwa sauti wakati nazidi kutafakari TOPIKI hii!

    ReplyDelete
  2. Mhh, hili darasa kali,naona nikalipitie vyema nyumbani, TUPO PAMOJA dada yangu...
    Kwa kifupi nachangia kuwa kila mmoja akubali ujinsia wake, na akubali na jamii ilivyoweka...ukitaka kuuliza sana `kwanini' utachanganyikiwa kwani mwisho wa siku utaingilia ,pango wa bwana God!

    ReplyDelete
  3. dada Yasinta Asante sana kwa mafundisho haya,kwani wewe si mchoyo unapenda kujifunza na wenzio!

    ReplyDelete
  4. Kuna wanaume wenye tabia za kike kotekote kasoro maumbile bondeni. Na pia unawapata wanawake ROUGH kama ngozi ya mamba.

    Hawa wasomi wenye kuandika vitabu nao wanatudanganya wakati mwingine... tue waangalifu jamaani!

    ReplyDelete
  5. Wanaume na misifa pamoja na ubishi, ni hiyo hiyo mihormoni ndiyo inayosababisha. Ni sawa na upande harage uklitegemea uote muhindi.
    Nawazua tu bila kuwaza

    ReplyDelete