Wednesday, May 4, 2011

HONGERA KWA SIKU YAKO YA KUZALIWA KAKA MANYANYA PHIRI!!!

Hongera sana kwa siku yako ya kuzaliwa na kubwa zaidi HONGERA KWA KUTIMIZA MIAKA 50. Kaka huyu siku ya kwenza kabisa kuingia katika blog hii ya Maisha na Mafanikio ilikuwa mwanzoni wa mwaka huu ilipokuwa siku yangu ya kuzaliwa kwa hiyo nami nimeona sina budi kumpongeza kwa siku yake ya kuzaliwa. HONGERA!!! Ukitaki kumzoma kazi zake unaweza kumtembelea:- goodmanmanyanyaphiri.blogspot.com


Najua wengi mtajiuliza huyu Kapulya alijuaje kama Kaka Manyanya anatimiza miaka leo? Ndiyi! nikwamba baada ya kutoa maoni yake katika mada hii ndo nilipogundua hili na nikaona ni kheri tumpongeze. http://ruhuwiko.blogspot.com/2011/04/yale-tuyaitayo-mabaya-ndiyo-hutufunza.html
Goodman Manyanya Phiri said...
Wewe Yasinta unatoka dunia gani? Mbona kila ukitoa kauli ni uhai mtupu? Ubarikiwe sana, Mwanadada!
Umekuwa malaika kwa wengi kutokana na nguvu za kalamu yako. Hasa kwangu nakuona malaika.
Saa iliopita nami nikiwa natangatanga jijini Pretoria kwa matatizo yangu mepya, nilikuwa nawaza: "kwanini maisha yangu Manyanya mie tangu ujana (16) hadi leo... tarehe 4 mwezi ujao (MAY) ninakuwa 50... ni vita tu na vita tupu?"
Hapo nikakumbuka maneno kuhusiana sana na msemo wako [kujifunza katika shida]...maneno kama haya http://pravstalk.com/pravs-world-gods-cup-of-tea/

["WE ARE LIKE TEABAGS, WHOSE STRENGTH COMES OUT WHEN WE’RE PUT IN HOT WATER. SO, WHEN PROBLEMS UPSET YOU… JUST THINK, YOU MUST BE GOD’S FAVOURITE CUP OF TEA!"]
Yule Mungu amekunywa ujana wote wangu... karibu nimtukane: "..Shenzi TYPE!". Lakini sitayasema hayo Kwake kwakuwa Yeye ni Muumba kwangu na malaika wake kama Yasinta wapo chungu mzima kunikumbusha [yote yanania na mwisho Kwake].
Hivi ndivyo nilivyogundua kuwa kaka Manyanya Phiri anatimiza miaka leo 4/5......
HONGERA SANA KWA KUTIMIZA MIAKA 50 MWENYEZI MUNGU AKUONGEZEE MIAKA 50 TENA NA PIA ZAIDI...!!!!!!

7 comments:

  1. Nami nachukua nafasi hii kumpongeza mdau Goodman Manyanya Phiri kwa kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa. Siku hii miaka hamsini iliyopita nafikiri ilikuwa siku muhimu kwa kumpokea duniani mwanaharakati, mpigania haki, msema ukweli, rafiki, baba wa familia, mzalendo, mwanamapinduzi, mtu mwenye upendo, utashi, utu wema....dah! na qualities nyingine kibao, Goodman Manyanya Phiri. Tumuombee azidi kuchanja mbuga na kukata miaka ili mchango wake duniani uzidi kudhihirishika!

    ReplyDelete
  2. Hongera sana kaka, Mungu na akuzidishie miaka mingi zaidi duniani.

    ReplyDelete
  3. Hoingera sana kaka Phili Manyanya kwa kutimiza miaka hiyo 50,Mungu akujalie maisha marefu zaidi na yenye amani pia mafanikio.Hepi bethidei tu yuuuu....

    ReplyDelete
  4. Hongera sana kaka Manyanya! Mungu akuongezee miaka mingi zaidi,uwe na wakati mwema.

    ReplyDelete
  5. Masihara hayo kaka! Miaka 50?..

    Hongera sana kaka na Mungu azidi kuwa nawe.

    ReplyDelete
  6. Happy birthday Manyanya, May God guard always

    ReplyDelete