Thursday, April 14, 2011

AJALI YA RESTIELI

Restieli.

Gari lao lililohusika na ajili hiyo.

Mama na baba Restieli.

Kama mnakumbuka niliwahi kuweka ushuhuda wa binti mmoja aitwae Restieli Moses Mbwambo akieleza kisa chake cha kuungua na mafuta akiwa mdogo (ukitaka kujikumbusha waweza kubofya hapa). Juzi nimepata taarifa kuwa familia ya binti huyo akiwemo mwenyewe Restieli, walipata ajali katika maeneo ya Lembeni mkoani Kilimanjaro.



Ajali hiyo ilihusisha gari lao dogo aina ya Toyota RAV 4 waliyokuwa akisafiria kutoka Upareni kurejea Moshi hapo mnamo siku ya Jumanne ya tarehe 5/04/2011. Ajali hiyo ilitokea baada ya tairi la mbele la gari hilo kupasuka na hivyo kupinduka mara kadhaa. Habari nilizozipata ni kwamba wote walisalimika katika ajali hiyo isipokuwa walipata majeraha kadhaa mwilini ambapo walitibiwa na kuruhusiwa.



Mleta habari amebainisha kwamba kutokana na ajali hiyo gari lao limeharibika vibaya, na ukiliangalia hutaamini kama waliokuwa ndani ya gari hilo wote wamepona.



Blog ya Maisha na Mafanikio inapenda kuchukua nafasi hii kuwapa pole wote walionusurika katika ajali hiyo, na ninaamini Mungu ataendelea kuwalinda.

6 comments:

  1. Nawapa pole sana, jambo jema la kushukuru ni kuwa wote waliokuwemo kwenye gari walitoka salama. Niwatakie afya njema na maisha yenye amani na furaha.

    ReplyDelete
  2. Poleni sana,na tunamshuru Mungu kwa kuwa mmepona na mnaendelea vyema!.

    ReplyDelete
  3. Tunashukuru sana.

    Hata yakitokea majaribio ya namna gani ya kutisha, kama siku haikuandikwa basi hiyo siku haikuandikwa tu!

    ReplyDelete
  4. Tena!, Jamani poleni sana wapendwa, yote ni mitihani ya Mwenye enzi Mungu.

    Duh! Restieli una mengi ya kusimulia wanao na wajukuu zako.

    ReplyDelete
  5. God is good all the time, majaribu ni kipimo cha imani yetu kwa Mungu, Mama na Baba Restiel, songeni mbele bado Mungu yupo pamoja nanyi hata mjapopita katika bonde la uvuli wa mauti. Zaburi 23:4, liwe ndilo fungu leni kuu.

    ReplyDelete