Wednesday, January 12, 2011

MASWALI YA LEO:- UPENDO NI KITU CHA AJABU AU?

Mke,mume na mtoto

Mara nyingi nimekuwa nikifikiri/jiuliza:- Je? ni kitu gani kinachotufanya sisi binadamu tupendane na kisha kuamini kuwa tunastahili kuwa mke na mume?

Kumpenda mtu usiyemfahamu na kisha kuwa mume/mke wako na kisha kuishi naye. Yaani kuwaacha wazazi wako na ndugu zako. Na kuamua kufunga pingu za maisha, na halafu kuishi pamoja na mwisho kupata na watoto. Hapa ndipo ninapokuja kujiuliza ni nini kinachotufanya binadamu sisi tuwe hivyo au ni nini udhaifu wake?

Halafu sasa cha ajabu zaidi hao hao waliopendana sana sana na kuwa mke na mume kwanini baadaye hupeana talaka? Na wengine wanaweza wakawa maadui kabisa ha kuongea tu haiwezekani.

Naomba ndugu wasomaji tusaidiane kupata majibu najua palipo na wengi hapaharibiki neno…..au nisema UMOJA NI NGUVU ……KAPULYA WENU.

7 comments:

  1. mada ya leo inafikirisha sana...nasubiri maoni ya wadau nami nipate darasa la kutosha.

    ReplyDelete
  2. "Waliyekuwa mume na mke wanawezaje kuzuwia mambo-sugu haya yatalaka?" ninahisi ndipo utafiti wako unapogusia, Dada Yasinta. Ukiwa ungali unalifikiria jambo la kwolewa na huyo jamaa , KABLA HUJAFANYA UAMUZI HUO fumba macho dakika mbili na mfikirie yeye tayari mumeo (au mkeo, ukiwa msomaji wewe ni wa kiume) na siku moja unatoka kazini ghafla na kumfumania. Yuko kama vile alivyozaliwa na papo hapo karibu na kitanda chako anapiga magoti na kukwomba msamaha. Olewa naye kama jibu lako ni “nitamwonea huruma sana asije kachunika ngozi ya magoti yake bure”. Na kama hutamsamehe musifunge ndoa maana yake hampendani ya kutosha: mnajihusisha na uasherati mtupu mkiwa huku mnajidanganya mnaweza kuwa kama Adamu na Hawa!

    ReplyDelete
  3. Upendo hauesabu mabaya,upendo hautakabari,upendo ni neno dogo lakini lina mapana na marefu!Nafikiri hata wanandoa waachanapo yule aliye na upendo wa kweli ndiyo anaeumia sana,mhhh da Yasinta nashindwa kufafanua ngoja niungane na kaka Mtanga.

    ReplyDelete
  4. kwanza ni udhaifu, ndoa ni ubinafsi, kwamba hii ni ya kwangu tu!!!!!

    ila ndivyo tulivyoumbwa, tukiwa watoto, tunamhitaji mama kwani anattupaziwa, tukikua tunamhitaji babapia, tukikua zaidi tunahitaji demu au mke, then tunagundua kuwa hawa hawatufai, basi tunatafuta watoto ni kutafuta furaha/ridhiko lisilopatikana katika mahusiano / ndoa!

    ReplyDelete
  5. Hivi neno UPENDO linamaanisha nini hasa? Maana yake ni nini hasa ukizingatia kuwa imesemwa/inasemwa/itasemwa kwamba upendo ndio uhitaji mkubwa zaidi wa Wanadamu. Tangu wanapozaliwa hadi kufa, watu hutamani kupendwa, wanaishi kwa furaha wanapopendwa na hata wanadhoofika na kufa wasipopendwa. Bila shaka, watu huongea sana kuhusu Upendo. Hata hivyo, jambo la kushangaza ni kuwa sio rahisi kuelezea maana ya Upendo. Baadhi ya wachambuzi wamefikia kukata kauli kuwa Upendo unaweza kuonyeshwa tu kupitia matendo.
    Kulingana na Biblia, kuna aina nne za upendo. Mosi, ni shauku changamfu, ya kibinafsi kumwelekea mtu fulani; aina ya upendo ulioko kati ya marafiki wa karibu (Yoh 11:3). Pili, Upendo ulioko kati ya washiriki wa kifamilia (Rum 12:10). Tatu, Upendo wa kimahaba ambao mtu anaweza kuwa nao kumwelekea mtu mwingine wa jinsi tofauti (Mith 5:15-20). Mwishowe ni upendo ulio na maana zaidi kuliko hizo aina nyingine tatu. Huo ni upendo mkubwa zaidi kwani huongozwa na kanuni; kanuni zinazofaa-zinazopatikana katika neno la MUNGU (Zab 119:105). Upendo huo, ni kufikiri kusiko na ubinafsi wa kuwafanyia wengine lililo sawa na jema kutokana na maoni ya MUNGU, iwe mwenye kupokea anastahili au la! Zaidi ya yote Upendo huo hauna ubinafsi.
    Tunaweza kupata ufahamu wa ndani wa neno hilo kutokana na maneno ya awali (ya Kiyunani) yaliyotafsiriwa “Upendo” katika Biblia (ya Kiswahili). Neno UPENDO linatokana na kutafsiri maneno manne (ndio aina nne za upendo) ya Kigiriki cha mwanzo/awali. Maneno hayo ni;
    · PHI·LE´O
    · STOR·GE´
    · E´ROS
    · A·GA´PE
    PHILEO: Kitenzi kinachomaanisha kuwa na shauku, kuthamini au kupenda (kama mtu anavyompenda rafiki wa karibu au ndugu). Hutumika mara nyingi katika Agano Jipya baada ya neno Agape.
    STORGE: Upendo ulio kati ya watu wa familia moja. Huu ndio upendo ambao Paulo mtume alisema una/utakuwa haba katika siku za mwisho (2Tim 3:3).
    EROS: Upendo wa kimahaba kati ya watu wa jinsi tofauti. Upendo huu hautajwi katika Agano Jipya bali katika Agano la Kale (Mith 5:15-20).
    AGAPE: Upendo unaoongozwa na kanuni na unatia ndani mambo mengi; unahusisha fikira na una kusudi fulani na hauna ubinafsi. Upendo huu sio hisia tunayokuwa nayo bila kufikiri. Mara nyingi huhusisha uhusiano wa karibu wenye upendo. Agape ndilo neno linaloelezea Upendo kwa njia nzuri zaidi. Aidha kati ya maneno hayo yote kuhusu Upendo; Agape limetumika mara nyingi zaidi katika Agano Jipya.
    Kwa ujumla (mara nyingi) aina zote zinastahili na zinabidi ziende pamoja. Mfano: Ni kweli upendo wa kimahaba (eros) una sehemu yenye maana sana katika ndoa zenye mafanikio; shauku yenye kina kirefu na urafiki (philia) huongezeka kati ya wanandani na huimarishwa na upendo (agape) ambao hustawishwa kumwelekea Mungu, Kristo na Jirani Yetu (Zetu).

    Kwahiyo, neno hilo (Upendo) ni neno ambalo lime/lina/litatumiwa sana na wanadamu. Ni neno ambalo limeandikiwa vitabu, likatungiwa nyimbo riwaya na mashairi mengi mno. Pamoja na hayo mara/ nyakati nyingine halifafanuliwi ifaavyo/ipasavyo. Ni neno ambalo lime/lina/litatumiwa sana hivi kwamba inaonekana (limeanza) kupoteza maana yake halisi (mfano ushoga, usagaji na ukahaba).

    Je wajua kuwa Upendo ndio sifa kuu zaidi ya Mwenyezi Mungu?

    NINA KUNYWA MAJI KWANZA

    ReplyDelete
  6. @Mcharia nimevutiwa sana na ufafanuzi wako!bado hayo maji hayashuka tuu ili uendelee tafadhali nasubri kwa hamu jamani!

    ReplyDelete
  7. Ni kweli upendo ni kitu cha ajabu sana, ukipenda ni kazi kumwelewa mtu yeyote.Wenye ndoa dumisheni upendo wenu kama mlivyo kuwa wachumba. Upendo wa kipindi cha uchumba ni mzuri sana. Eleweni tofauti zenu na mvumiliane ili kudumisha upendo wenu.

    ReplyDelete