Wednesday, January 5, 2011

LEO NI SIKU YANGU YA KUZALIWA

Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda salama mpaka kufika siku hii ya leo na kuongeza limwaka limoja zaidi. Namshukuru kwa kuniepusha na mambo mabaya, magonjwa na pia vishawishi. Kijana wangu Erik amepata nafasi kuchagua hii picha anasema ameipenda.

kutimiza miaka bila mziki hapana. Haya wote UNGANENI NAMI NA WIMBO WA TUSELEBUKE NI KITOTO/LIZOMBE....


Namshukuru Mungu kwa yote, familia yangu pia ninyi marafiki zangu!!!

39 comments:

  1. Kudadadadeki siku zinaenda! Si majuzi tu ilikuwa siku yako ya kuzaliwa? Haya rafiki yangu naomba Mungu azidi kukulinda hivi hivi hadi uone vitukuu vyako...

    Hongera sana kwa siku hiii...umenishinda vijisiku vidooooogo..Vinginevyo ningekuwa dadako.

    Bless you!

    ReplyDelete
  2. Hongera dada kwa siku yako ya kuzaliwa.Mungu akuzidishie heri na baraka zake.

    ReplyDelete
  3. Dadi Witu nakuombea maisha mema na marefu mpaka miaka 100 kila la kheri.

    ReplyDelete
  4. Hongera kwa siku yako ya kuzaliwa dada Yasinta! Mungu akuzidishie mema katika maisha yako uishi miaka miiiingi sana yaani hata 100 upite kabisa! Hehehe! Baraka kwako dada, Happy Birthday

    ReplyDelete
  5. Kumbe "sem dei" na "mai papa"?
    Good one. Watu wawili wenye umuhimu ndani ya siku moja iliyo muhimu
    UNAPENDWA PIA.
    UNASHUKURIWA MNO
    NA
    UNATHAMINIWA SANA

    Happy EARTHDAY

    ReplyDelete
  6. Happy birthday mamito
    whr is a party?

    ReplyDelete
  7. Hongera dada yangu na Mungu akulinde na kukuzidishia mema!!

    ReplyDelete
  8. Unauhakika au umekosea...kila la kheri binti maringo. Mungu akujalie uishi sana na uwe na watoto wengi kama mwana wa mfalme!

    ReplyDelete
  9. Hiyo picha ya mkonyezo imeniacha hoi..wee haya weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  10. Happy birth day Mama Maisha tunauombea Mafanikio zaidi.
    Mungu akubariki

    ReplyDelete
  11. Hakika ni furaha
    Iliyochanganyika na raha
    Mwaka mwingine kwa Yasinta
    Neema zizidi kujikita
    Miaka izidi kukatika
    Hepi Besidei da' Yasinta!

    ReplyDelete
  12. Hata mimi siamini dada yetu juzijuzi tu ulikuwa ukisherehekea kulia ng'aa ng'aa...leo tena.
    Hongera sana twakutakia maisha mema, yenye baraka na fanaka, mungu akuzidishie uhai uwaone watukuu wako!

    ReplyDelete
  13. Hongera sana Da Yasinta kwa siku yako ya kuzaliwa,Mungu na akulinde ili ufikishe miaka zaidi ya mia moja.

    ReplyDelete
  14. hongera sana kwakuzaliwa, mama! <3
    i hope you'll have a great day :)

    ReplyDelete
  15. Grattis Mamma !
    ha en trevlig och rolig dag.

    ReplyDelete
  16. Hongela sana...ntakuletea ugimbi tugide kidogo bana!

    ReplyDelete
  17. Heri ya siku ya kuzaliwa mama wa maisha na mafanikio. Mungu akuzidishie miaka mingi mingine yenye amani, upendo, furaha na ,mafanikio tele.

    ReplyDelete
  18. Hongera sana dada mpendwa kwa siku yako hii muhimu!Mungu akubariki sana pamoja na familiya yako!

    Da Yasinta hako kawimbo kananikumbusha mbali sana nimempenda mwenyewe hihiiii hapo ndiyo!

    kamwali cheketua cheketuuu!!! hahahaha nipo hoi kwa kucheza.

    ReplyDelete
  19. hongera dada mkuu kwa kuchana kalenda. mungu akulinde uchane kalenda kibao mbeleni

    chacha o'wambura usinisahau kwenye idadi ya ugimbi nami nimo. nadhani na simon kitururu tusimsahau

    Eric ana jicho kali sana. hapana shaka kama ameweza kuchagua pozi kama hili basi naye atachangua kifaa huko mbeleni

    ReplyDelete
  20. Was looking for Kiswahili blogs and then, on this auspicious occasion, got myself glued on yours. A very happy birthday indeed from Manyanya

    ReplyDelete
  21. Hongera sana kwa siku yako ya kuzaliwa.pia ahsante kwa lizombee!!!
    God bless you.
    xx

    ReplyDelete
  22. Hongera bibie! Mungu akuzidishie maisha marefu na yenye baraka Tele.

    ReplyDelete
  23. Mpendwa Dada Yasinta,

    Heri sana kwa Siku yako ya kuzaliwa.
    Asante kwa shughuli unayofanya ya kutuelimisha na kutuhabarisha daima.
    Ujaliwe maisha marefu na heri na baraka daima.

    Nduguyo,

    Pd. Novatus Ngonyani - München.

    ReplyDelete
  24. hongera kwa siku yako ya kuzaliwa,mungu akuzidishie.pia ahsante kwa wimbo mzuri umenikumbusha mbali sana.

    ReplyDelete
  25. hayaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  26. happy birth day to you sister, may god help u to live a hundred years,

    ReplyDelete
  27. Wakati unazaliwa jana nilikuwa kwenye basi naelekea Musoma, hongera mpendwa, nitakutumia zawadi nzuri itakayoimarisha uzalendo wako kwa Tanzania yako, katika mwaka huu. Happy B.D!

    ReplyDelete
  28. Basi hongera sana

    ReplyDelete
  29. Hongera
    nilikuwa nje ya Njombe.
    Kila la kheri na maisha mema na yenye mafanikio na baraka tele
    Kumbuka maisha ni safari na katika asfari hiyo kuna vikwazo na changamoto zote zinatakiwa kuwa somo badala ya kuwa kizuizi na kuwa sehemu y akukufanya kukosa furaha

    ReplyDelete
  30. Ahsanteni sana wote kweli hapa ndipo ninapoamini kuwa sisi sote ni ndugu na ni watoto wa baba mmoja. Hakika ni furaha ya pekee kusherekea siku hii pamoja nanyi. Najikuta naandika na machozi yananidondoka kwa furaha. Nina swali moja kwa Mija Kudadadeki ni lugha gani? Ahsante sana saaana na wote mnapendwa sana:-)

    ReplyDelete
  31. Happy returns though belated on you birthday!
    You are a great woman and we are proud of you and your blog is entertaining, educative and we look forward to reading more from you...........

    SIKU YAKO LEO!
    SIKU YAKO LEO!
    FURAHIA, SHANGILIA, SIKU YAKO LEO!

    ReplyDelete
  32. hongera kipenzi ijapokuwa nimechelewa love u sanaaaa

    ReplyDelete
  33. Mlongo hongera sana kwa kushelekea siku yako ya kuzaliwa. natumaini ulikuwa na siku nnzuri kwako. na asante sana kwa kutukumbusha kunyumba ubarikiwe sana.

    ReplyDelete
  34. Hongera kwa siku yako ya kuzaliwa.

    Kwa kweli Blog yako ina nivutia sana. Ni kati ya watu ambao huwa tunazunguka blog mbali mbali.
    Nakutakia mafanikio mwaka huu kwako na familia yako.
    Hongera sana kwa siku kubwa hii.

    ReplyDelete
  35. MWAKA HAUJAISHA,
    MAISHA YANAKUJA,
    SIKU ZINAPITA,
    UPENDO NENO MOJA,
    FAMILIA NZIMA,
    IWE AMANI DAIMA,

    SIJACHELEWA MAMA,
    SIKU HII NJEMA,
    YEYE MAULANA,
    AJUA YA MAANA,

    NISAMEHE MAMA,
    LEO NAKIRI SANA,
    SIKU HIIIWE NJEMA,
    MUNGU AKUPE PENDO JEMA,
    FAMILIA IWE NA RAHA NA NEEMA.

    ReplyDelete