Leo tarehe 19-08-2009, nilikumbuka tukio moja lilitokea tarehe 25-3-2008, tukio lenyewe lilikuwa hivi:
Dunia hii ni duara, na watu kama tulivyo, kukutana ni wajibu, tofauti na milima. Katika kukutana ndipo tunapojenga urafiki, udugu na hata uchumba, ndio ni kweli hata uadui pia. Lakini tusisahau kuwa kama binadamu tulivyo, kukoseana na hata kujengeana uadui kupo, lakini hili ni nadra, na linapotokea huwa lina sababu, kwani ibilisi huja na visa vyake ili viwe fundisho kwetu.
Diana baada ya kukaa kwenye kampuni moja kwa muda mrefu, alipata bahati ya kuomba sehemu nyingine. Alifanya hivi ili kupata sehemu itakayokidhi mahitaji yake, lakini pia alishachoka kufanya kazi na meneja wake ambaye kila siku waliishia kugombana. Siku alipopewa barua ya ajira sehemu nyingine, ambayo ilimuahidi kipato kikubwa, alitamani dunia yote ijue kuwa yeye sasa hivi, sio yule Diana waliyemjua ni Diana mwingine. Kwa raha aliyokuwa nayo, aliingia ofisisni kwa taksi, na akiwa amechelewa.
Alipofika asubuhi ofisini, aliwasabahi wale waliokuwa karibu naye huku akiwapa mkono wa kwaheri. Alimwendea bosi wake ambaye walikuwa hawaivani, na alipoulizwa kwanini kachelewa alijibu kwa dharau, `tatizo la usafiri,’ Bosi alipotaka kuja juu akaona huo ndio muda muafaka wa kumpa bosi vipande vyake, na kweli alimpa bosi vipande vyake, na kumwambia sasa hivi yeye na kampuni yake basi.Bosi wake Mr. JeuriMbaya ambaye licha ya ukali wake katika kazi, kitu ambacho wengi walimuona ana roho mbaya, alikuwa muungwana pale panapohitajika, alichofanya ni kumtakia kila-laheri, na kumwambia kama katika utendaji wake wakazi walikwazana, basi anaomba msamaha, kwani yeye alikuwa akitimiza wajibu wake tu. Diana alimwangalia kwa jicho la dharau, akageuka na kuelekea kwenye meza yake, huku moyoni akisema, bosi wa namna yako hastahili kufanya kazi na mimi.
Hapo mezani alitumia muda mwingi kuwajulisha marafiki zake kuwa yeye sasa atakuwa katika ofisi za Kampuni kubwa ya Kimarekani, ambapo pia ameahidiwa kupekwa masomoni.Ilipofika jioni, Diana alichukuliwa na taksi, ya mshikaji wake na moja kwa moja walielekea Kaunta. Huko alikunywa kama amesingiziwa. Waliondoka maeneo hayo usiku akiwa hajitambui. Njiani kwa vile walikuwa wamelewa chakari, wakapata ajali mbaya, ajali hiyo ilimvunja Diana mguu na kujikuta anapelekwa Muhimbili.
Kwa vile Kampuni yake mpya ilishaingia mkataba naye, ilimsaidia na kumhakikishia kuwa ajira yake bado ipo ingawaje alikuwa hajaanza kazi. Hii ilimpa faraja sana Diana, na akaendelea na matibabu yake huku akijua hawezi kumrudia meneja JeuriMbaya.. Hapo Muhimbili alikaa miezi miwili. Alipotoka, alipewa mapumziko ya mwezi mzima nyumbani.
Siku ikafika, na hali ya mguu wake ilisharejea vyema, ikabidi aripoti ofisini kwake, kwenye ofisi mpya. Alikariribishwa kwa bashasha na kila mmoja akimpa pole kwa huruma na upendo. Hali hii hakuizoea huko alikotoka. Alifurahi moyoni, na kusema `hapa ndipo nilipokuwa nikapataka…
`Diana tuna bahati kubwa sana, kwani tumepata meneja utawala mpya, ambaye utakuwa katibu muhtasi wake, naye kaajiriwa karibuni, kwahiyo twende ofisini kwake ukatambulishwe’ Aliambiwa na Ofisa utawala.
Akiwa na bashasha ya kumuona meneja wake mpya, ambaye alihisi atakuwa Mzungu, alitabasamu akamtafadhali Ofisa Utawala na kuchepuka kwanza chooni ili aweze kujikwatua. Hii ilikuwa sehemu ya mambo ambayo alifundishwa kuwa anatakiwa apendeze ili kumvutia bosi wake pamoja wageni.
Aliongozana na ofisa utawala, mama wa makamo, mama ambaye aliijua kazi yake vilivyo. Na kwa uzoefu wa siku nyingi, aliona amuelekeze yule binti wake mambo kadhaa kabla hajampeleka kwa bosi wake mpya. Diana alijisikia vibaya, hakupenda kukosolewa, lakini alijikaza akijua kuwa anabembeleza ajira.Kabla ya kuingia kwa meneja huyo ilibidi wapitie kwa meneja wengine mbalimbali, na kila sehemu alipokelewa vizuri na kukaribishwa ofisi mpya.
Mwishowe walifika kwenye ofisi iliyoandikwa `Meneja utawala’ Waligonga mlango wa Meneja Utawala na kukaribishwa ndani.Walipoingia walimkuta meneja Utawala akiwa ameinama na kugeukia upande mwingine, kwahiyo sura yake ilikuwa haionekani vizuri.‘Karibuni tafadhali, natafuta faili moja hapa, la huyu katibu wangu Mhtasi, unasema anaitwa nani vile…’
Aliwakaribisha huku akitaka kulifunua lile faili, bila kuwaangalia.‘Tafadhali bosi hatutaki kuchukua muda wako mwingi, yeye kwa vile mtakuwa naye karibu atajitambulisha kwako vizuri, kama unavyojua alikuwa anaumwa, kabla hata hajaanza kazi hapa….’ Aliongea ofisa utawala.
‘Oooh, karibuni sana,..’ aligeuka akiwa amenyosha mkono.Mshangao alioupata Diana ulimfanya aishiwe na nguvu, na kama asingekuwa ameegemea meza angejikuta kadondoka chini. Hakuamini macho yake…
‘Ahsante, sh-shi-kamoooo bosi’ Alijikuta akitoa salama ambayo hajawahi kumsalimia bosi wake kabla.Aliyekuwa amesimama mbele yake si mwingine ila ni bosi wake wa zamani, ambaye waliachana naye kwa mizengwe, sasa ni bosi wake mpya, Mr.Jeuri Mbaya.JE KAMA WEWE UNGEKUWA NI DIANA UNGEFANYAJE
Makala hii nimeipenda na nimeona si vibaya nikiiweka hapa ili wengi wajifunza nimeipata toka hapa.
Ni kisa cheye ujumbe mzuri, kwani tunaonywa kuwa tusitukane wakunga wakati uzazi ungalipo!
ReplyDeleteShukurani dada yetu kwa kuukumbushia ujumbe huu murua!
kwani bosi kitu gani?? si arudi kwenye kazi yake ya zamani tu?
ReplyDeleteMmmmmmh!
ReplyDeleteKweli kama ingekuwa mimi nigerudi kuomba kazi sehemu ile ya mwanzo, kwasabbu bosi huyo hayupo tena!
ReplyDeleteNilipoanza kusoma I knew right away kwamba siyo wewe uliyeandika because you don't have the talent and the know how kuandika with such clarity. Na blogu nzima kila siku ni kucopy and paste kazi za wengine tu, mara hii nimeitoa huku mara huku. Entries ambazo umeziandika mwenyewe are very shallow and in most cases don't make any sense but for some reasons people like you and they leave comments day in and day out. Mmmmmmm!
ReplyDeleteMimi naona tusishambuliane kwa ku copy and paste kama ulivyosema wewe anyn. Hiyo pia ni moja ya ujuzi.
ReplyDeleteChukulia mfano unaposoma history au masmo darasani, unafanya nini , unacopy na kupaste waliyofanya wengine...ni elimu, na pia ni moja ya kumpenda yule aliyeiandika mwanzo.
Jambo jema hupendwa na kila mtu, na yule anayelipenda zaidi hulichukua na kulitangaza, ndivyo alivyofanya dada yetu na hii ni moja ya kipaji, hekima. Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe, au mwasemaje/