Tuesday, November 2, 2010

Fikirisho la jumanne hii(Kapulya mdadisi)

Nipo katika Fikra hapa

Leo nimeamka huku nikiwa na fikra kama hizi ni hivi :- Je? umewahi kufikiria kwanini watu hatuli chakula aina moja tu kila siku?
Au kwanini hatuvai nguo moja tu kila siku?
Na halafu kwa nini tuwe/tuitwe (na) jina moja tu wakati wote? kwa nini tusibadili majina yetu pia kila siku?
Baada ya kuwaza hivi sikutaka kuwaza tu, au kuwaza peke yangu nimeamua kuwashirikisha nanyi ndugu zangu/ wasomaji wa Maisha na Mafanikio. Haya tufikiri/Tutafakari kwa pamoja.......

8 comments:

  1. Hatuli chakula aina moja kwasababu unapokula kinapokwena hatupajui, labda kile cha haja kubwa au ndogo, nacho kinapokwenda hatujui, labda shambani na kuwa mbolea, na mavuno yake hatuyajui labda mboga na mapilipili hoho.
    Ama kwa nguo twabadili kwasababu twataka kuonekana , twataka kusifiwa ,...je kuna asiyependa kusifiwa, mmmh, sijui.
    Lakini kwa majina, ukibadili leo na kesho tutakusahau, hata kama ulikuwa ukila kila siku vinono, lakini jina ukaliita manono,kesho machips, kesho kutwa maubwabwa, mmmh, hatutakukumbuka kwa hilo, tutakukumbuka kwa lile la asili.
    Hivi uliuliza nini vile?
    Mhhh, ni hayo tu kwa leo

    ReplyDelete
  2. jawabu ni moja tu ukisha juwa tafauti ya sisi na wanyama itakuwa jawabu umeipata dasinta sisi binaadamu tafauti na wanyama moja ni kuwa tumeumbwa na akili sidhani kama kuna punda anataka kubadilisha chakula au kuva nguo sijuwi nimwjibu?

    ReplyDelete
  3. unauhakika kama sivai chupi moja tu tangu nilipoanza kuvaa chupi?

    ReplyDelete
  4. yaaani hata sijui kipenzi umefikiria nini nice one umenifanya nimekaa nafikiria

    ReplyDelete
  5. Ahsanteni wote kwa majibu yetu, kuna wakati mtu unaweza tu ukafikiri kitu bila kufikiri na mimi huwa nafikiri na ninapofikiri hata kama ni usiku basi naamka na kuandika. Na hapa sijui nilikuwa nafikiri nini..lol Hivi huwa tunafikiri kwanza halafu tunawaza au kinyume?

    ReplyDelete
  6. obat telat bulan i think your blog very informative cytotec thanks for sharing obat cytotec

    ReplyDelete