Ni wiki moja sasa imepita tangu uchaguzi ufanyike Tanzania yetu pia Zanzibar. Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuufanya uchaguzi kuwa wa amani pia utulivu. Kwani katika uchaguzi kunaweza kutokea mengi.
Ni ujumbe mzuri Yasinta, japo ni dhahiri kuwa watanzania wote ni wapenda umani japo wakati wa kampeni kulikuwepo na propaganda chafu za kuwahadaa watanzania kuwa wakichagua upinzani amani itavunjika. Hili kamwe haliingii akilini kwangu kwasababu sikuona kama kuna mgombea yeyote aliyekuwa akinadi vita au udini.
Huu usemi wa udini na ukabila ulikuwa ukihubiriwa na chama kimoja tu cha siasa na sijui lengo lao ilikuwa ni nini haswa.
Hii misamiati wa udini na ukabila ni ngeni miongoni mwa watanzania watanzania kwani tunaheshimu na kufuata maadali mazuri tuliyoachiwa na muasisi wa nchi yetu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Nyerere alikemea waziwazi suala la udini na ukabila, lakini leo hii ni nani mwenye nguvu ya kufanya hivyo.
Matokeo ya uchaguzi huu yametufundisha mengi,kura zilipigwa kwa kuangalia udini wa mgombea wala siyo sifa za uongozi bora.
Hata hivyo, sitapenda nizame ndani zaidi maana nikiendelea kufanya hivyo nitachokonoa mambo mazito ambayo watanzania hawajui hadi sasa kuhusu udini na mgawanyo wa madaraka ndani ya serikali ya Tanzania.
Ni rahisi sana kusema, na ni rahisi sana kumnyoshea mwenzako kidole, lakini twasahahu kuwa vidole vingine vinakuelekea wewe! Udini , na ukabila sidhani kama kuna chama chochote kimeandika katika ilani yake, lakini wagombeaji walikuwa wakituhumu kuwa wengine vyama vyao vina itaikadi hiyo, sasa wapi pameandikwa? Cha muhimu ni kuwa kila mtu ana akili ya kufikiri, na mwisho wa siku `kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe..' Kuna jamaa mmoja alisema `mwizi anaogopa sana kuibiwa na akiibiwa analalamika sana, je ni kwanini, wakati yeye ndiyo tabia yake...' kwasababu mkuki kwa nguruwe tu, kwa binadamu nini vile?
Kweli tunapaswa kumshukuru MUNGU, kwani pamoja na CCM kuchakachua sana matokeo (KURA), lakini bado Watanzania wamenyamaza!!! Lakini pamoja na ukimya wa Watanzania, CCM na Serikali yake wamepata ujumbe kuwa wananchi (WATANZANIA) kwa sasa wameanza kuona thamani ya kura zao, na tena hawapo tayari kuendelea kudanganywa na CCM na Viongozi wake wanao fisadia nchi na kufanya waishi maisha ya taabu na dhiki kubwa kwa maslahi ya MAFISADI wachache!! WATANZANIA sas wameanza kuipigia honi CCM ili ipishe njia waweze kuingiza chama mbadala kuendesha nchi! Tusubiri na tuone mabadiliko chanya yatakayo tokea ndani ya miaaka sio zaidi ya kumi ijayo!
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu sana kwa mema aliyo tujalia katika kipindi chote hicho. Asante sana Baba Mungu. Jumapili njema Dada Yasinta.
ReplyDeleteNi ujumbe mzuri Yasinta, japo ni dhahiri kuwa watanzania wote ni wapenda umani japo wakati wa kampeni kulikuwepo na propaganda chafu za kuwahadaa watanzania kuwa wakichagua upinzani amani itavunjika. Hili kamwe haliingii akilini kwangu kwasababu sikuona kama kuna mgombea yeyote aliyekuwa akinadi vita au udini.
ReplyDeleteHuu usemi wa udini na ukabila ulikuwa ukihubiriwa na chama kimoja tu cha siasa na sijui lengo lao ilikuwa ni nini haswa.
Hii misamiati wa udini na ukabila ni ngeni miongoni mwa watanzania watanzania kwani tunaheshimu na kufuata maadali mazuri tuliyoachiwa na muasisi wa nchi yetu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Nyerere alikemea waziwazi suala la udini na ukabila, lakini leo hii ni nani mwenye nguvu ya kufanya hivyo.
Matokeo ya uchaguzi huu yametufundisha mengi,kura zilipigwa kwa kuangalia udini wa mgombea wala siyo sifa za uongozi bora.
Hata hivyo, sitapenda nizame ndani zaidi maana nikiendelea kufanya hivyo nitachokonoa mambo mazito ambayo watanzania hawajui hadi sasa kuhusu udini na mgawanyo wa madaraka ndani ya serikali ya Tanzania.
Ni rahisi sana kusema, na ni rahisi sana kumnyoshea mwenzako kidole, lakini twasahahu kuwa vidole vingine vinakuelekea wewe!
ReplyDeleteUdini , na ukabila sidhani kama kuna chama chochote kimeandika katika ilani yake, lakini wagombeaji walikuwa wakituhumu kuwa wengine vyama vyao vina itaikadi hiyo, sasa wapi pameandikwa?
Cha muhimu ni kuwa kila mtu ana akili ya kufikiri, na mwisho wa siku `kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe..'
Kuna jamaa mmoja alisema `mwizi anaogopa sana kuibiwa na akiibiwa analalamika sana, je ni kwanini, wakati yeye ndiyo tabia yake...' kwasababu mkuki kwa nguruwe tu, kwa binadamu nini vile?
waone vilee
ReplyDeleteKweli tunapaswa kumshukuru MUNGU, kwani pamoja na CCM kuchakachua sana matokeo (KURA), lakini bado Watanzania wamenyamaza!!! Lakini pamoja na ukimya wa Watanzania, CCM na Serikali yake wamepata ujumbe kuwa wananchi (WATANZANIA) kwa sasa wameanza kuona thamani ya kura zao, na tena hawapo tayari kuendelea kudanganywa na CCM na Viongozi wake wanao fisadia nchi na kufanya waishi maisha ya taabu na dhiki kubwa kwa maslahi ya MAFISADI wachache!! WATANZANIA sas wameanza kuipigia honi CCM ili ipishe njia waweze kuingiza chama mbadala kuendesha nchi! Tusubiri na tuone mabadiliko chanya yatakayo tokea ndani ya miaaka sio zaidi ya kumi ijayo!
ReplyDelete