Nasadiki kwa mungu Baba mwenyezi/mwumba mbingu na nchi,/na vitu vyote vinavyoonekana,/na visivyoonekana.
Nasadiki kwa bwana mmoja yesu kristu,mwana wa pekee wa mungu.Aliyezaliwa kwa baba tangu milele yote.
Mungu aliyetoka kwa mungu,mwanga kwa mwanga,mungu kweli kwa mungu kweli.
Aliyezaliwa bila kuumbwa,mwenye umungu mmoja na Baba,ambaye vitu vyote vimeumbwa naye.Ameshuka toka mbinguni
kwa ajili yetu sisi wanadamu na kwa ajili ya wokovu wetu.
Akapata mwili kwa uwezo wa roho mtakatifu kwake yeye bikira maria/akawa mwanadamu
Akasulibiwa pia/kwa ajili yetu sisi/akateswa kwa mamlaka ya ponsyo pilato,akafa akazikwa.
Akafufuka siku ya tatu ilivyoandikwa.akapaa mbiguni/amekaa kuume kwa baba
atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu wazima na wafu nao ufalme wake hautakuwa na mwisho
Nasadiki kwa roho mtakatifu/bwana mleta uzima atokaye kwa baba na mwana anayeabudiwa na kutukuzwa
pamoja na baba na mwana aliyenena kwa vinywa vya manabii.
Nasadiki kwa kanisa moja,takaifu katoliki la mitume.naungama ubatizo mmoja kwa maondoleo ya dhambi.
Nangojea na ufufuko wa wafu.Na uzima wa milele ijayo.Amina.
JUMAPILI NJEMA WAPENDWA!!!
Amen. Yasinta unaweza kuniangalizia kwa jicho la ndani hiyo mistari ya mwisho ya kusadiki katika katika Katoliki? huoni kama panahitajika marekebisho? Si unajua siku hizi ilivyo ngumu kusadiki makanisa.....
ReplyDeleteJumapili njema.
Mmmmh!
ReplyDeleteJumapili njema Dada Yasinta!
Nakwako pia, pamoja na familia yako kwa ujumla.
ReplyDeleteDada Yasinta umenikumbusha mbali sana, na sala hii ya nasadiki. Maana nilifeli siku ya mtihani wa komunio ya kwanza...katekista alinifanyia kweli, wenzangu aliwapa sala zile nyepesi nyepesi...mimi akanitwanga na hiyo Nasadiki, mchezo ukaisha...sikupata komunio ya kwanza. Akasema kajiandae vizuri utarudia mwaka kesho...hasira niliyo kuwa nayo mpaka basi.
ReplyDeleteHahaaaa
ReplyDeleteHahaaaa
ReplyDeleteamina.....
ReplyDeleteamina....
ReplyDelete